Pia katika Taarifa hiyo ya habari japo kwa mwisho nimekuta Jaji Mkuu Agustine Ramadhani akimalizia kueleza kuwa; "Suala la mabadiliko ya Katiba linawezekana, kwani Tayari nchi nyingi zimefanya na kuzitaja Kenya na Uganda na kusema linazungumzika na lina namna yake ya kujadiliwa," Mtangazaji akauliza iwapo kitendo cha wabunge wa Chadema ni kosa Kisheria, Jaji mkuu anajibu "Siyo kosa kisheria, pengine lingeandaliwa katika kanuni za Bunge lakini pia anaamini kuwa hakuna kosa na ndiyo maana Spika hakusema lolote, lakini sana sana tunaweza kulielezea kama ni swala la maadili tu lakini si sheria".
Hii ni kwa Mujibu wa TBC 1 habari ya saa 2 usiku.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Jamani mbona saa mbili usiku haijafika !!
ni kweli uliyosema halafu kuna njama za kumuandama zitto humu jamvini .zitto ameongea vizuri sana... tatizo humu jamvini tunataka mambo ya upinzani yaende kama mechi ya kinondoni muslim na tambaza
na hayo ya kupingana yangetokea ccm kesho ungesikia mtu katolewa chamani
Huna sababu ya kuwachukia. Kuna watu vichwa vinafanya kazi. Wanamptisha waziri mkuu na wanaomba serikali inayoongozwa na mtu wasiyemtambua asikilize madai yao!!!!! Kuna haja ya kufikiria upya strategies za namna hii. Zitto anatambua wazi kuwa strategy hii ni fake maana February watakuwa bungeni na wanahitaji kujadili hotuba ya Rais. Wakisusa kwa CCM ni mteremko tu maana hata utendaji wa serikali hawataujadili na kwa kifupi CCM watapeta zaidi. Nadhani aliyeshauri strategy hii alisahau kuangalia mbeleni. Mnakumbuka kura za maruhani Zenji? CHADEMA wanayaweza haya?Hivi unajua kwamba naanza kuwachukia Zitto na Shibuda? Haki ya nani vile.
Msaliti dawa yake ni KIFO shen$%%^ kabisa!
Katika kuonesha hali ya masikitiko Mh zitto zuberi kabwe amepingana na kitendo cha chadema kutoka nje ya bunge, akiongea na TBC leo Zitto amesema yeye kama yeye hakubali kitendo cha chadema kuwalk out
Big Up ZITTO :lock1::lock1:hapo umeonesha ukomavu wa siasa
karibu chamani:clap2:
I dont see an issue (hapa tuna make a mountain out of a mole hill) kutokukubaliana ni kawaida kura zikapigwa wengi wakashinda thats normal lakini i think Zitto angekaa kimya tu there is no need awaambie vyombo vya habari what went behind the scenes