Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Hata kesi ya babu seya mlipiga kelele HIV HIV mwishowe jamaa wanapiga tu bend ya magereza,kuwa na busara ni kitu muhim katika maisha
 
Zitto kwanini na wewe umekuwa hv? umewauliza mawakili wa Lema kwanini kanyimwa dhamana na walicho kifanya jana mahakamani?

Zitto dhamana haitolewi kienyeji eti kisa tuu kosa lina dhamana kuna taratibu zake za kufuata endapo upande wapili unapinga muhusika kupewa dhamana. Mawakili walishindwa kufata taratibu na upande wa jamhuri ukaona udhaifu huo na kuutumia na hakimu akaona wanayo hoja.
Mbona Lissu alipewa dhamana yeye na wenzie walipo jenga hoja na kuwa makini? huo ulikuwa mkono wa nani?

Zitto usijiingize kwenye upumbavu na ulofa dhamana haitolewi kama unapo kwenda kununua karanga dukani hasa kama kuna wanaopinga...mawakili makini hujenga hoja na hakimu huwa ni kama refaree.

Zitto acha upumbavu na ulofa najua Bavicha watakuunga mkono kwenye hili.
Acha kujiona muerevu kwa mambo yaliowazi. Kuwaita wenzio malofa na wapumbavu, wewe je? Au umejitoa ufahamu?
 
Kweli Lema alikosea lakini kitendo cha mahaka kuingiliwa huu ni mwendelezo wa mfumo mbovu ambao watendaji wakuu wa vyombo muhimu Kama hivi kuteuliwa.
Mkuu mahakama imeingiliwa na mtu gani unaweza kutusaidia kuthibitishia kauli yako pasipo chembe ya shaka?
 
Hivi Harry Kitilya aliwahi kufikiria atakaa mahabusu, achana na siku moja kupita tu karibu na gereza? Huyo hakimu na wamshurutishao zamu yao yaja.
Ndio, si alipiga dili? Kila mpiga dili anakaa kimachale.
 
Hujiulizi ni kwa nini Mandela alipotoka Gerezani alipokelewa na Winnie Mandela na siyo kina Oliver Thambo. Vitu rahisi namna hii kueleweka vinapokuwa vigumu kwenu ndiyo inayotufanya tujue ni kwa nini mnawashabikia wale jamaa!!
Mandela Mandela ... Unamjua Mandela wewe.
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine leo (jana) amenyimwa dhamana na imeamriwa na mahakama kuwa akae mahabusu mpaka Februari mwakani kesi yake itakapotajwa tena.

Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kuridhishwa na vigezo vya kisheria ambavyo vilitolewa na mawakili wa Jamhuri ambao waliweka pingamizi Lema asipewe dhamana.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alimtembelea Lema gerezani leo na haya ndiyo ameyaandika kuhusu Lema, kesi yake na hali ya kunyimwa dhamana.

ZITTO KABWE:

Leo (jana) Ijumaa Desemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza la Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati za kutafuta na kulinda haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa sana na ukiukwaji mkubwa wa haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona ni bora akae ndani mpaka hapo dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa mke jasiri anayempa moyo na ndio ngome yake kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka haki kutendeka katika uendeshaji wa nchi yetu. Siku zote haki hushinda.

CHANZO: Maandishi Genius
Hivi?
Zitto hajamshawishi Lema ili ajiunge na ACT?
 
Ulidhani siasa ni uadui?
 
Huwa najifunza mengi sana kwa zitto kabwe ni mtu mstaarabu na pia mvumilivu na ni mwanasiasa wa kweli aisekuwa na lepe la unafki
Wewe bila kumsifia zzk huwezi kupata usigizi
 
Zitto ni mtu safi sana, siasa zake za kistaarabu sana. Sijui ana roho ya namba gani huyu jamaa. Hana visasi hata siku moja.
 
Halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Kila atakayeleta za kuleta ni lazima ajutie maneno au vitendo vyake. Ubatizo wa maji umepita, uliobaki sasa ni ubatizo wa moto. (We have to change our mindset )
 
alichokosea jamaa ni kushika sharubu za no 1 wakati mwenzie alishasema hataki mtu ajaribu kuchezea sharubu zake
 
Hapa ndo wapinzani wananifurahisha kila kitu wanageuza fursa
 
Halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Kila atakayeleta za kuleta ni lazima ajutie maneno au vitendo vyake. Ubatizo wa maji umepita, uliobaki sasa ni ubatizo wa moto. (We have to change our mindset )

Rais wa Gambia amekubali kushindwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom