Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Uongo na uzushi. Nipeni ushahidi wa hayo maandishi ya Zitto. Kayaandika wapi?
 
Nilipomsikia mtu mmoja anasema eti kuna mhimili mmoja umechimbiwa chini zaidi nilishangaa sana!

Nadhani maana yake ndio hii sasa!
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine leo (jana) amenyimwa dhamana na imeamriwa na mahakama kuwa akae mahabusu mpaka Februari mwakani kesi yake itakapotajwa tena.

Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kuridhishwa na vigezo vya kisheria ambavyo vilitolewa na mawakili wa Jamhuri ambao waliweka pingamizi Lema asipewe dhamana.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alimtembelea Lema gerezani leo na haya ndiyo ameyaandika kuhusu Lema, kesi yake na hali ya kunyimwa dhamana.

ZITTO KABWE:

Leo (jana) Ijumaa Desemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza la Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati za kutafuta na kulinda haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa sana na ukiukwaji mkubwa wa haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona ni bora akae ndani mpaka hapo dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana
.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa mke jasiri anayempa moyo na ndio ngome yake kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka haki kutendeka katika uendeshaji wa nchi yetu. Siku zote haki hushinda.

Zitto kwanini na wewe umekuwa hv? umewauliza mawakili wa Lema kwanini kanyimwa dhamana na walicho kifanya jana mahakamani?

Zitto dhamana haitolewi kienyeji eti kisa tuu kosa lina dhamana kuna taratibu zake za kufuata endapo upande wapili unapinga muhusika kupewa dhamana. Mawakili walishindwa kufata taratibu na upande wa jamhuri ukaona udhaifu huo na kuutumia na hakimu akaona wanayo hoja.
Mbona Lissu alipewa dhamana yeye na wenzie walipo jenga hoja na kuwa makini? huo ulikuwa mkono wa nani?

Zitto usijiingize kwenye upumbavu na ulofa dhamana haitolewi kama unapo kwenda kununua karanga dukani hasa kama kuna wanaopinga...mawakili makini hujenga hoja na hakimu huwa ni kama refaree.

Zitto acha upumbavu na ulofa najua Bavicha watakuunga mkono kwenye hili.
 
Linalofanyika kwa Lema kwa mtu yeyote anayejipa japo dakika kufikiri hawezi kuona ni sawa
 
Huo ni uongo.hakuna mtu yoyote anayefurahia kukaa ndani kunyea debe?Kwanini tunakuwa warahisi kuamini mambo ambayo hata kwa akili za kawaida hayakubaliki?Alafu msemaji mwenyewe huyuhuyu zito huyuuuuu haha simuamini hata chembe.Lema aendelee kufurahia ndani alafu akina Zito wataenda kumsalimia mkewe ....maana ndio halisi.
 
Sasa Inajulikana rasmi kabisa kuwa kosa la Lema lina dhamana kisheria ila this time mahakama imegeuka kuwa kichaka cha kuficha maovu ya watawala.
Yana mwisho haya.
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine leo (jana) amenyimwa dhamana na imeamriwa na mahakama kuwa akae mahabusu mpaka Februari mwakani kesi yake itakapotajwa tena.

Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kuridhishwa na vigezo vya kisheria ambavyo vilitolewa na mawakili wa Jamhuri ambao waliweka pingamizi Lema asipewe dhamana.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alimtembelea Lema gerezani leo na haya ndiyo ameyaandika kuhusu Lema, kesi yake na hali ya kunyimwa dhamana.

ZITTO KABWE:

Leo (jana) Ijumaa Desemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza la Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati za kutafuta na kulinda haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa sana na ukiukwaji mkubwa wa haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona ni bora akae ndani mpaka hapo dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa mke jasiri anayempa moyo na ndio ngome yake kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka haki kutendeka katika uendeshaji wa nchi yetu. Siku zote haki hushinda.

Kwenye swala hili nimejifunza vitu muhimu:
i. Siasa sio uadui: Kwa yaliyompata Zito Chadema yakimhusisha Lema, kwenda kumtembelea gerezani kabla hata ya wakubwa wa Chadema, kuna fundisho chanya.
ii. Unapokuwa na ujasiri wa kusimamia kile unachoamini, basi dhuluma zozote za kukutingisha hazitafaulu kukupotezea focus yako! Lema anaonekana kutotetereka bado licha ya yote.
iii. Kama haya yamewezekana kwa mti mbichi, sembuse kwa miti mikavu? Kama limewezekana kwa Lema, Mbunge, anayetetewa na mawakili wasomi, kwa sababu mwenye nguvu (serikali) kaamua kumkomesha, sembuse kwa mlala hoi atakapokwaruzana na tajiri/kibosile/fogo/kigogo? Kumbe mahabusu zina wengi sana ambao hawakustahili kuwa kule ila wako huko kwa kutiwa adabu na wakubwa!
 
siasa za mahakama...na ukomavu wa lema..ni historia ya kata funua
 
Back
Top Bottom