Baadhi ya wanasiasa wanawaaminisha wananchi kuwa gesi asilia itatatua matatizo yote ya wananchi na nchi kwa jumla, na wengine wanaamini kwamba gesi ndo itaweza kulipa deni la taifa,ila gesi ni kama madini itawanufaisha wateule wachache sana................waacheni wananchi waendelee kujitafutia mikate yao na familia zao,msiwajaze maneno wakawaamini,wakiandamana mtawalipua kwa risasi na mabomu.Ukiacha gesi kuna rasilimali ngapi nchi hii jamani?Juzi Prof Muhongo ameitaja nchi kama India ambayo leo hii anaitolea mfano,ila India na baadhi ya nchi za South East Asia hazikuendelea kwa sababu ya rasilimali za asili,ziliendelea kwa kuwekeza kwenye RASILIMALI WATU.
Kuna sera 2 ambazo India iliwekeza
1.Sera ya Elimu
2.Sera ya Viwanda
3.Sera ya ushindani (Haikuwa rasmi)India alikuwa akishindana na China kwa kusomesha vijana na kuwapeleka nje wakasome.
China aliwekeza katika sera 3-4
1.Sera ya elimu
2.Sera ya Kilimo
3.Sera ya Viwanda
4.Sera ya Teknolojia (ambapo yeye na India walikuwa wakinunua teknolojia nje na kuleta nyumbani,huku wakiwatumia vijana wao waliowasomesha ndani na nje kuziendeleza).
Akitokea Kiongozi akatuambia kuwa tutaendelea kwa gesi au rasilimali yoyote ya asili ni Muongo.Nchi huendelea kwa kuwekeza kwenye rasilimali watu "HUMAN CAPITAL DEVELOPMENT"Ndio maana sisi na Malaysia,India,China,South Korea,Hong Kong even Japan we were almost similar by 1970s,leo wametuacha mbaaaaali,naamini miaka mitatu ijayo twaweza anza kuomba misaada MALAYSIA.
Mkoroshokigoli