rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 18,068
- 25,725
hapo ndio utaelewa kwanini dr bukuku alipewa pesa kwenye akaunti ya escrow
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto kabwe, ameshutumu watuhumiwa wa Akaunti ya Tegeta Escrow kupewa kazi(zabuni) ya ujenzi wa bandari ya Mwambani mkoani Tanga bila kufuata taratibu.
Zitto amesema Rugemarila amepewa zabuni hiyo yenye thamani ya shilingi trilioni 54 bila kufuata taratibu za zabuni ikiwa ni pamoja na zabuni hiyo kutangazwa.
My take:
Hivi hii nchi ina laana?
Kama tuhuma hizi ni za kweli,viongozi wa nchi hii mko wapi na mnafanya nini maofisini?!
Tuwekane sawa hapo ni tilioni 56 au billion 56
Sina habari na Zitto.Kilichonichefua ni hilo jina la Rugemarila na huyo mwingine wa Richmond.
Tusiwe kama wabunge wa CCM,sisi tuangalie hoja na si mleta hoja.
Hata hivyo,nakiri Zitto haaminiki ila hapa hoja si zitto bali hoja ni tuhuma za kupeana zabuni kihuni tena kwa watu wenye rekodi ya kunuka rushwa na ufisadi.
Ni aibu mbunge au wabunge kusema uongo kwa makusudi na kwa malengo binafsi.
Kwanza kabisa Zitto Kabwe alishapoteza sifa ya kuendelea kuwasilisha ripoti ya PAC bungeni kama mwenyekiti wake, kuhusiana na sakata la TEGETA ESCROW, hii ni baada ya kutuhumiwa na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde kuwa na yeye alipokea mgao wa ESCROW kwa nia ya kupindisha ukweli au kuficha ukweli.
Zitto hakujibu tuhuma hizi licha ya Lusinde kuzitoa kwa ufasha Bungeni, na cha ajabu Professor Mwandosya alimtetea Zitto na kumtaka aeendelee kuwasilisha eti tuhuma hizo hazikua sehemu ya agenda ya siku hiyo.
Mbona mara nyingi wa Bunge hutoa taarifa au huomba miongozo Bungeni. Je, hizi nazo huwa ni sehemu ya agenda ya mijadala inayokua inaendelea? Zitto alipaswa kujibu zile tuhuma au kujiondoa mara moja PAC na kumuachia mtu mwingine asiye na tuhuma kuendelea na kuwasilisha ripoti hiyo.
Kama muwasilisha ripoti ni mchafu ripoti itakuaje safi? Ndiyo maana ripoti haikumtaja Muidhinishaji mkuu wa kutoa pesa hizo waziri wa fedha, maafisa wengine waandamizi waliohusika na uidhinishaji wa fedha hizo.
Fedha hizo zilipotoka BOT, zilikua safi lakini zilipo fika Stanbic na Mkombozi zikawa chafu, Hizo pesa hizi kutoka BOT siku moja zilitoka kwa awamu na siku tofauti na kwa maombi rasmi yenye baraka za BOT na wahusika wengine wa mambo ya fedha.
Yupo kijana ambaye alikua kinara wa migomo ya wanafunzi alipokua anasoma Muhimbili, ni huyu huyu aliyeingia sekondari kwa kutumia jina la mwenzake mlala hoi, ni huyu huyu mwenye utata kwenye uraia wake , aliyesimama Bungeni bila heshima ya umri, wadhifa na kumuita Professor Muhongo muongo. Je, nani muongo Professor au yeye aliyetumia jina la mwenzake kuingia sekondari?
Vipi Dr Mengi anaweza kuelezea kwa ufupi alivyo lipa deni la ANCHIMWEDU NBC? Je, Mh Mkono anaweza kutu brief yaliyomsibu GAPEX?
Inabidi wa Tanzania tuwe waangalifu na mbinu na maneno ya wanasiasa hasa siku hizi ambazo uadilifu umepungua, wanasiasa wanatumia maneno kuhadaa watu, kupumbaza watu, kuzusha, kutukana.
UFISADI UMEOTA MIZIZI, IMEKUA SIFA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA, WIZI WA MALI ZA UMMA NI SIFA, INAYO ITWA ANA MAENDELEO BWANA.!!!
TAIFA NI LETU TUTALIKOMBOA SISI WENYEWE

Kama huna imani na Zitto kipi kinakufanya uamini Habari zake ?
Tusiingize siasa za CHADEMA na Zitto kwenye kila kitu.
Kumbuka hata Kafulila alipoibua kashifa ya Escrow Bungeni, wabunge na wana-CCM wengi walimpuuza kisa tu kwasababu Kafulila alikuwa mpinzani.
Vivyo hivyo,hoja hii ya Zitto hatuwezi kupiuuza kwasababu tu ya tofauti ya kisiasa kati ya Zitto na CHADEMA.
Haya ndio matatizo yaliyoko hata Bungeni.Mpinzani akiibua hoja CCM wanaipinga tu kisa tu tofauti za kisiasa zilizopo.
Ingekuwa Zitto kaiongelea vibaya CHADEMA hapo sawa.Kauli hiyo niingeichukua katika mtazamo wa kisiasa na niingetilia mashaka kauli hiyo lakini si kwa hii ya ufisadi wa kina Ruge na kundi lake.
Hii "mentality" ya kuchanganya siasa na chuki za kisiasa kwenye kila jambo la kitaifa inatutafuna sana watanzania.
Madudu ya Zitto kwenye hoja hii ya ufisadi hayana nafasi hapa.
Tunapowalaumu wabunge wa CCM kwa kupuuza hoja za wapinzani kwasababu tu za kisiasa sisi wenyewe tunapaswa kuwa mfano katika kusimamia kauli na misimamo yetu hiyo bila kujali tofauti zetu za kisiasa.
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapatia kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watuhumiwa wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Amesema watuhumiwa hao wamepewa kazi hiyo kupitia Mradi wa Mwambani Economic Corridor (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54, huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji wa zabuni zilizofuatwa na Serikali.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika katika miji ya Mafinga na Iringa mkoani hapa ambapo alisema Serikali imeipa kazi ya ujenzi Kampuni ya VIP Engineering and Management inayomilikiwa na James Rugemalira ambaye anahusika katika sakata la Escrow.
Zitto alisema ACT-Wazalendo wanamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.
Mwambani Economic Corridor Project hapakuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa, na huu mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership (PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.
Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Bandari ya Mwambani, miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa guarantee kwa mikopo ambayo inachukuliwa.
Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni mwendelezo wa miradi ya kitapeli, alisema Zitto.
Zitto ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari unakwenda sambamba na reli ambayo itafika hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alimtaka Waziri Sitta kutoa taarifa kwa umma kwa kuwa taifa limechoshwa na miradi ya kitapeli.
MWANASHERIA ATOA UTETEZI
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo hivi karibuni, msimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, Cathbert Tenga, alisema utamilikiwa na Watanzania wenyewe na si watu kutoka nje ya nchi kama ilivyo katika miradi mingine.
Sisi hivi sasa tunahangaika kuhakikisha nchi hii inasonga mbele kwani mradi huu hivi sasa upo katika hatua za awali za upembuzi yakinifu kwa kuwa na timu ya wataalamu, na ili jambo hili liweze kusonga mbele ni lazima siasa ziepukwe, alisema Wakili Tenga.
Alisema kutokana na juhudi wanazoendelea nazo hadi sasa wamefanikiwa kupata benki ya Afrika Kusini, DBSA, ambayo itafanya kazi katika mradi huo mkubwa nchini.
Tenga alisema mradi huo wa MWAPORC utakuwa ni moja ya nguzo kwa uchumi wa taifa ikiwa Serikali itaamua ufanyike kwa kuwaunga mkono Watanzania wazalendo badala ya kujali wageni pekee.
MWIGAMBA NA UMASKINI
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.
Wakati Rais Jakaya Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya, lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi chake cha uongozi, uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.
Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini, lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki watazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa, alisema
Mwigamba.
Alisema pamoja na tanzanite kuchimbwa nchini, lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini hayo ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.