Zitto amlipua Rugemarila wa Escrow

Zitto amlipua Rugemarila wa Escrow

Nabado mwakahuu mpaka mtawekewa drip za maji, inapanda inashuka du! Ztt go,go,go, wataelewa tu team wazalendo
 
Leo hii namwomba ruge agawe tena mihela kama njugu bila escrow kuwepo.
 
Cha kujiuliza hiyo VIP ina ujuzi na uzoefu wa mambo ya ujenzi hasa kwa kandarasi kubwa namna hiyo?je bodi ya makandarasi ina rekodi ya kampuni ya VIP kuhusu miradi ya ujenzi,mimi sijawahi kusikia VIP wakisimamia ujenzi wowote haalali hapa Tanzania,kama kuna mtu yupo anajua kandarasi zilizofanywa na VIP basi atuwekee hapa,kwanza kwa kile tu kitendo cha kuwahonga watumishi wa umma kinamuondolea sifa bwana Ruge na kampuni zake kushiriki katika tenda zozote za kiserikali ilitakiwa awe blacklisted !!,na kwa utapeli anaoufanya huyo bwana hiyo bandari haitajengwa na hata inflate gharama ,na baadaye ataipeleka mahakamani serikali ili imlipe fidia na huku hajafanya chochote,mtu aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
 
Hata Zitto mikutano ya ACT lukuki anatoa pesa wapi kama si hizo hizo za escrow.
 
Ni sahihi, ni USD($) 33bn,itakua ni kutanua bandari ya tanga na kuongeza urefu wa kina mpka mita 24,watajenga bandari huru na heavy haul standard gauge railway mpaka bahari ya Atlantic, kwa hiyo itakua railway pekee itakayo unganisha bahari ya Hindi na Atlantic


Mkuu na mimi nifuatilia nimegundua kua hizo figure ni kweli, dah nchi hii kuna watu wanajua kutafuta dili za hela.
 
Cha kujiuliza hiyo VIP ina ujuzi na uzoefu wa mambo ya ujenzi hasa kwa kandarasi kubwa namna hiyo?je bodi ya makandarasi ina rekodi ya kampuni ya VIP kuhusu miradi ya ujenzi,mimi sijawahi kusikia VIP wakisimamia ujenzi wowote haalali hapa Tanzania,kama kuna mtu yupo anajua kandarasi zilizofanywa na VIP basi atuwekee hapa,kwanza kwa kile tu kitendo cha kuwahonga watumishi wa umma kinamuondolea sifa bwana Ruge na kampuni zake kushiriki katika tenda zozote za kiserikali ilitakiwa awe blacklisted !!,na kwa utapeli anaoufanya huyo bwana hiyo bandari haitajengwa na hata inflate gharama ,na baadaye ataipeleka mahakamani serikali ili imlipe fidia na huku hajafanya chochote,mtu aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.


Mkuu Rugemarila ni Tycoon siyo mfanyabiashara wa kawaida. Mimi tokea nipate akili sijawai kusikia mbongo aliyepata tenda yenye thamani ya trion moja lakini huyu amepata tenda yenye thamani ya tr.54. Huyu jamaa ana nguvu ambayo hatuioni na siyo mtu wa kawaida kabisa, mtu anayewekeza kwenye mradi kama huu akitaka kumpoteza mtu ni suala la mda tu.
 
Sasa watz imefikia mahala suala linalohusu taifa,maovu yanayofanywa na serikali mnayatetea kwa kuwa aliyewaambia watanzania ni mzalendo wa nchi na ww humkubali. Sijui taifa linaelekea wapi. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABARIKI WAZALENDO. sisi sote ni wamoja na taifa letu ni moja, tuungane pamoja kutetea maslahi ya taifa letu.
 
Sasa watz imefikia mahala suala linalohusu taifa,maovu yanayofanywa na serikali mnayatetea kwa kuwa aliyewaambia watanzania ni mzalendo wa nchi na ww humkubali. Sijui taifa linaelekea wapi. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABARIKI WAZALENDO. sisi sote ni wamoja na taifa letu ni moja, tuungane pamoja kutetea maslahi ya taifa letu.

Inasikitisha kwamba wote mliochangia mpaka sasa mnazidi kuthibitisha uvivu wenu wa kusoma. Hakuna aliyejenja hoja, ni milio, kelele na kejeli. Hamuwezi kuisaidia nchi kwa namna hii. Ndiyo maana mnadanganywa kwa urahisi na watu walaghai kama Zito, shame!
 
1. Watanzania tunadanganyika kwa urahisi sana! Na Zito yote anayoyafanya ni kwa kujua kwamba nchi hii inalo kundi kubwa la watu wanaomuamini kwamba ni mzalendo. Ni kwamba anajua hamsomi sana sana vichwa vya habari za magazeti na mnaamini moja kwa moja bila kufikiria zaidi na kufanya uchambuzi. Tatizo ni kubwa.

2. Watanzania tupende kusoma ili tuweze kujadili mambo kwa weledi. Zito aliyoyafanya kwenye Escrow ni kwa kutambua kwamba hatupendi kusoma. Kuthibitisha kutopenda kusoma kwetu, Mtanzania mmoja Bw. Salim Khatri, kwa kujitolea, alijihusisha kusoma taarifa zote yaani ile ya CAG na PAC amekuja na uchambuzi wa kina kuhusu hizo taarifa na akabainisha jinsi ZITO KABWE alivyo handisi taarifa ya PAC.

3. Huo uchambuzi wa kitaalam wa Bw. Khatri, uliwekwa wazi kwa Wahariri Wakuu wa vyombo vya habari nchini kwenye Semina ulioandaliwa na VIP Engineering & Marketing Ltd., kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika kwenye hoteli ya Stella Maris mjini Bagamoyo, tarehe 3 - 4 Aprili, 2015.

4. Wakati wa Semina hiyo Bw. Khatri, akiwa patia wahariri wakuu fursa ya kuuliza maswali. Wahariri waliuliza maswali yao na kujibiwa. Hitimisho la Mada hiyo washiriki wote walikubali kwamba ZITO KABWE alihandisi taarifa yake kwa manufaa yake. Hii ni bila kujali taharuki aliyolisababishia taifa na kuhatarisha kuiangusha serikali.

5. Wiki moja baadaye, Zito katika hali ya kutahayari, bila kutafuta ukweli, akaamua kumshambulia binafsi Bw. James Rugemalira wa VIP. Baadhi ya magazeti yameandika uzushi wa Zito kwa kuhusisha waliyoyasema wahusika wa MWAPORC, kwani Wahariri wa magazeti hayo walikuwa wanazo taarifa za kina kuhusu mradi huo na wahusika wake. Wapo pia walioziandika habari za Zito kama kabisa hawana wajualo!

6. Juzi iliwekwa hapa JF taarifa ya uchunguzi ya Bw. Khatri, kutuonyesha UONGO wa taarifa ya PAC. Badala ya watu kuisoma kwa makini ili waichambue na kuikosoa, kwa kutojua wakatenda dhambi ya kukataa kusoma. Ninashindwa kuamini kwamba mtu ambaye hajasoma taarifa anavyoweza kusimama na kuikataa! Msemo wa Mao "no research no right to speak" hapa unakuwa na maana kubwa sana.

7. Watanzania wenzangu ninawasihi tuache uvivu wa kusoma. Hii ndiyo sababu kubwa ya kukimbilia kwenye umbea na kuhadaika kwa wepesi kwa watu aina ya Zito. Mkiisoma Kazi aliyoifanya Bw. Khatri, ninaamini mtaona jinsi wanasiasa wadanganyifu na wasaliti wa nchii wanavyo iangamiza nchi yetu na Zito akiwa ni mmoja wao.

8. Kazi ya Bw. Khatri, inadhihirisha kwamba Bunge linatumiwa na wanasiasa wabaya, walaghai, wazandiki na mafisadi kuihujumu nchi. Kazi ya Khatri, inaweza kuwa ndiyo mwanzo wa kukomesha huu uhuni ambao waheshimiwa wanatumia pesa zetu ili kuihujumu nchi.

9. Tusipokuwa makini, tujue kwamba tunajikaanga kwa mafuta yetu. Zito anatahayari badala ya UONGO wake alioufanya akiwa M/Kiti wa PAC kuhusu Ripoti Maalum ya Akaunti ya Tegeta Escrow kugundulika. MWAPORC haujawahi kuwa mradi wa Serikali kama alivyowaeleza Wahariri Wakuu kule Bagamoyo. Zito ana tapatapa za mwizi arobaini zimetimia. Wanasema, "you can fool some of the people all the time but you cannot fool all the people all the time". Watanzania, someni taarifa ya Bw. Khatri, kama kuikataa iwe ni kwa hoja na siyo milio kama niliyoisoma hapa JF.

Mungu Ibariki Tanzania!

Mkuu,naomba link ya taarifa hiyo ya bwana Khatri.
 
Rugemaila yuleyule alietoa pesa kama zawadi kwa wanasiasa? Sasa unaweza pata picha kumbe pesa alizowahonga ilikuwa kwa ajili ya kupata tenda kama hyo aliyopewa. Nadhani huko Stanbic wamepewa mawaziri wa wizara husika ndio maana.

Kinachoshangaza wale waliochukua pesa kwa lumbesa kutoka benki ya Stanbic mbona hawatajwi kama wale wa Mkombozi? Hata wapinzani naona kama vile wamelisahau.
 
Moto umeshawaka,hakuna tena wa
kuuzima,wale waliukuwa wanatumiwa
na Mafisadi walidhani wamemaliza
Zitto ili mafisadi waendelee kutafuna
nchi bila kisumbuliwa.
Sasa watanzania tunaujua mchezo
wote uliokuwa na lengo la
mumnyamanzosha Zitto.
Ninyi mawakala wa wa Majizi
mnapoteza muda kudhani mnaweza
kurudhisha nyuma harakati za
kukamata wezi.
Suluhisho ni kuwa wezi wa taifa
wahame nchi,na juzi tulionya
kuendelea kumpa tenda Rugemalila ,ile
tenda ya Tril 54 hatuta ifumbia macho.
Tutaendelea kuungwa mkono na
wanyonge wa nchi hii ,ninyi kuweni
upande wa mabeberu lkn kamwe
hamtatushinda.
 
Huyo ndio zzk hongera sana lkn pamoja na haya vicjaa wanokaririshwa pia wataponda

Safi sana Zitto Kabwe,jitu limekaa bungeni lenyewe ni kupinga tu kila kitu eti ni upinzani,nchi inakufa kila siku lakini sioni upinzani ukileta hoja za msingi za kufichua maovu,tunataka upinzani wenye tija wa kuleta maendeleo ya nchi na watu wake.

Kwani zzk hakuwa mbunge wakati zabuni hiyo unapita? Kwa hiyo nae alikaa kimya tuuu? Aache ubwege wake. Alisubiri hadi aingie act ndo aseme?

Alishindwa nini kulipua akaunti ya Stanbic!?? mnafiki tu huyu!!

Act daima tukopamojaa


Salamu zenu!
Huyu Zitto ananitia wasi sanaa!! Katka kipindi chote hiki sijawahi kusikia akimkosoa Kikwete kwa utendaji mbovu! Kwa hili analosema bado mtindo ni huo huo. Huwezi kulaumu mwizi kama Rugemalira wakati ukifahamu hiyo ndo kazi yake. Rugemalira ni mwizi siku zote na ndivyo tumekuwa tukionyeshwa ktk historia ya maisha yake. Tumlaumu kiongozi wa nchi kwa kumfanya rafiki.

Haya yote yanayotokea yako kiwango cha juu na ni wazi yanafahamika kwa kiongozi wa nchi. Bahati mbaya tuliyopata ni kuwa na Rais asiyejua mema na mabaya kwa urahisi.
 
Inasikitisha kwamba wote mliochangia mpaka sasa mnazidi kuthibitisha uvivu wenu wa kusoma. Hakuna aliyejenja hoja, ni milio, kelele na kejeli. Hamuwezi kuisaidia nchi kwa namna hii. Ndiyo maana mnadanganywa kwa urahisi na watu walaghai kama Zito, shame!


Baada ya siku chache tu utasikia Zitto kapewa na Rugemalira milioni kadhaa. Ndo madili ya Zitto hayo! Anakamata kama traffic Police na kupewa chochote hapo hapo!
 
Jamani, napata wasiwasi na magreat thinkers huku ndani, wengi ni watu wa kudandia hoja bila kufanya uchambuzi au kusikiliza upande wa pili, VIP Haijapewa tenda ya ujenzi, sasa hivi serikali inaingia katika ujenzi wa miundo mbinu kwa kutumia PPP kama inavyofanyika katika nchi za ulaya, Private investors wanamobilize resources wanajenga miundombinu halafu wanacharge watumiaji kama litakavyokuwa daraja la Kigamboni. Kina Rugemalila wanakusanya fedha kwa ajili ya kujenga bandari na standard gauge railway kwenda DRC na Burundi, watakaosafirisha mizigo kupitia bandari na reli hiyo watalipa. Mfano wa kitu kama hiki ni Njia ya Reli ya chini ya bahari inayounganisha Uingereza na Ufaransa, hii ilijengwa na makampuni binafsi. Pia serikali inatafuta kampuni ya kujenga njia nne kwenda Chalinze ambapo watumiaji watalipa.
 
Mpanzi nafikiri issue hapa ni kwa nini Rugemalila na asiwe mwingine? Ukichukulia kuwa ana skendo inayohusiana na utendeji wake wa kazi. Kama aliweza kugawa fedha juu ya IPTL inawezekana pia kahonga ili apewe hiyo nafasi ya kukusanya fedha za ujenzi wa hizo bandari akijua kuwa zitakapomalizika atapata faida maradufu??
 
Mpanzi nafikiri issue hapa ni kwa nini Rugemalila na asiwe mwingine? Ukichukulia kuwa ana skendo inayohusiana na utendeji wake wa kazi. Kama aliweza kugawa fedha juu ya IPTL inawezekana pia kahonga ili apewe hiyo nafasi ya kukusanya fedha za ujenzi wa hizo bandari akijua kuwa zitakapomalizika atapata faida maradufu??

Kampuni inayojenga hiyo bandari ni Mwambani Port and Railway Corridor Company (Mwaporc) Mkurugenzi wake ni Mr Cuthbert Tenga, na project sio ya serikali, Mwaporc wanachofanya ni kutafuta wabia wa kushirikiana nao. Serikali sio iliyowaambia Mwaporc washirikane na VIP. Huu ni mradi binafsi. Hata wewe ukiwa na Mradi wa kujenga bara bara ya juu kutoka Tegeta mpaka mjini kupunguza foleni utapewa, tuache siasa kwenye mambo ya maendeleo.
 
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto kabwe, ameshutumu watuhumiwa wa Akaunti ya Tegeta Escrow kupewa kazi(zabuni) ya ujenzi wa bandari ya Mwambani mkoani Tanga bila kufuata taratibu.

Zitto amesema Rugemarila amepewa zabuni hiyo yenye thamani ya shilingi trilioni 54 bila kufuata taratibu za zabuni ikiwa ni pamoja na zabuni hiyo kutangazwa.



My take:
Hivi hii nchi ina laana?

Kama tuhuma hizi ni za kweli,viongozi wa nchi hii mko wapi na mnafanya nini maofisini?!

Tusiwaamini wanasiasa sio kila atakachosema ni kweli ZZK anatafuta kick hana uzalendo wowote.
 
ZITTO ni mpiga madili hanajipya.tusiwaamini wanasiasa tufanye upembuzi kwanza ndo tuwaamini.
 
Back
Top Bottom