Zitto amlipua Rugemarila wa Escrow

Zitto amlipua Rugemarila wa Escrow

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,639
Reaction score
164,768
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto kabwe, ameshutumu watuhumiwa wa Akaunti ya Tegeta Escrow kupewa kazi(zabuni) ya ujenzi wa bandari ya Mwambani mkoani Tanga bila kufuata taratibu.

Zitto amesema Rugemarila amepewa zabuni hiyo yenye thamani ya shilingi trilioni 54 bila kufuata taratibu za zabuni ikiwa ni pamoja na zabuni hiyo kutangazwa.

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapatia kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watuhumiwa wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Amesema watuhumiwa hao wamepewa kazi hiyo kupitia Mradi wa Mwambani Economic Corridor (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54, huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji wa zabuni zilizofuatwa na Serikali.

Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika katika miji ya Mafinga na Iringa mkoani hapa ambapo alisema Serikali imeipa kazi ya ujenzi Kampuni ya VIP Engineering and Management inayomilikiwa na James Rugemalira ambaye anahusika katika sakata la Escrow.

Zitto alisema ACT-Wazalendo wanamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.

"Mwambani Economic Corridor Project hapakuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa, na huu mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership (PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.

"Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Bandari ya Mwambani, miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa ‘guarantee' kwa mikopo ambayo inachukuliwa.

"Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni mwendelezo wa miradi ya kitapeli," alisema Zitto.

Zitto ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari unakwenda sambamba na reli ambayo itafika hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Alimtaka Waziri Sitta kutoa taarifa kwa umma kwa kuwa taifa limechoshwa na miradi ya kitapeli.

MWANASHERIA ATOA UTETEZI

Akitoa taarifa kuhusu mradi huo hivi karibuni, msimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, Cathbert Tenga, alisema utamilikiwa na Watanzania wenyewe na si watu kutoka nje ya nchi kama ilivyo katika miradi mingine.

"Sisi hivi sasa tunahangaika kuhakikisha nchi hii inasonga mbele kwani mradi huu hivi sasa upo katika hatua za awali za upembuzi yakinifu kwa kuwa na timu ya wataalamu, na ili jambo hili liweze kusonga mbele ni lazima siasa ziepukwe," alisema Wakili Tenga.

Alisema kutokana na juhudi wanazoendelea nazo hadi sasa wamefanikiwa kupata benki ya Afrika Kusini, DBSA, ambayo itafanya kazi katika mradi huo mkubwa nchini.
Tenga alisema mradi huo wa MWAPORC utakuwa ni moja ya nguzo kwa uchumi wa taifa ikiwa Serikali itaamua ufanyike kwa kuwaunga mkono Watanzania wazalendo badala ya kujali wageni pekee.

MWIGAMBA NA UMASKINI
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.

"Wakati Rais Jakaya Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya, lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi chake cha uongozi, uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.

"Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini, lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki watazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa," alisema
Mwigamba.

Alisema pamoja na tanzanite kuchimbwa nchini, lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini hayo ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.

CHANZO: Mtanzania

My take:
Hivi hii nchi ina laana?

Kama tuhuma hizi ni za kweli,viongozi wa nchi hii mko wapi na mnafanya nini maofisini?!
 
Ivi jamani nani aliyetuloga??
Inamaana toka siku iyo zabuni imeweka sokon na huyu Ruge akaipata bado tu hao wabunge hawakuliona hilo?

kwasasa naanza kuamini katika ile theory ya waandish wa habari kwamba hata kama unaona mtu anauwawa uko radhi kurekodi lile tukio ili upate habari kuliko kwenda kuwa sehem ya kuzia lile tukio.

so sad kuona tunakuwa deceived na watu tuliowaamin af wanakuja kuturudi tena na kuwa watu wa kutuambia kwamba tumeumizwa ilihali themselves are the sources of fire.
 
Rugemaila yuleyule alietoa pesa kama zawadi kwa wanasiasa? Sasa unaweza pata picha kumbe pesa alizowahonga ilikuwa kwa ajili ya kupata tenda kama hyo aliyopewa. Nadhani huko Stanbic wamepewa mawaziri wa wizara husika ndio maana.
 
wabunge wote akili zao wameelekeza kwenye uchaguzi mkuu, hata ile taarifa ya escrow wakati inajadiliwa kuna vitu walikuwa wanaogopa kujadili ingawa Tundu lissu aligusia aliyehusika ni mkuu wa nchi na pia watu wengi walitakiwa waondoke hata kesi zilizopelekwa mahakamani na takukuru hakuna hata moja watakayoshindwa kwa sababu rugemalila na yeye alitakiwa apelekwe kwani mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana makosa
 
Rugemaila yuleyule alietoa pesa kama zawadi kwa wanasiasa? Sasa unaweza pata picha kumbe pesa alizowahonga ilikuwa kwa ajili ya kupata tenda kama hyo aliyopewa. Nadhani huko Stanbic wamepewa mawaziri wa wizara husika ndio maana.

Ruge ni mtu safi bana. Hata wewe unakubali kwamba kuna ufisadi serikalini kweli?
 
I like Rugemalira,Duh.Ina maana mfuko wake ni mkubwa kiasi gani huyu hadi aiweke serikali yote mfukoni?
 
usilaumu watendaji, kosa ni letu, kuwaachia wapuuzi wachache wafanye wanachotaka
Kaka, huu ndio ukweli mchungu ambao hatutaki kuusikia au kuambiana. Tukiweza hapo tu, hii nchi itabadilika. Madereva juzi hapa wametupa mfano mzuri sana.
 
Safi sana Zitto Kabwe,jitu limekaa bungeni lenyewe ni kupinga tu kila kitu eti ni upinzani,nchi inakufa kila siku lakini sioni upinzani ukileta hoja za msingi za kufichua maovu,tunataka upinzani wenye tija wa kuleta maendeleo ya nchi na watu wake.
 
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapatia kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watuhumiwa wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Amesema watuhumiwa hao wamepewa kazi hiyo kupitia Mradi wa Mwambani Economic Corridor (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54, huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji wa zabuni zilizofuatwa na Serikali.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika katika miji ya Mafinga na Iringa mkoani hapa ambapo alisema Serikali imeipa kazi ya ujenzi Kampuni ya VIP Engineering and Management inayomilikiwa na James Rugemalira ambaye anahusika katika sakata la Escrow.
Zitto alisema ACT-Wazalendo wanamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.
“Mwambani Economic Corridor Project hapakuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa, na huu mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership (PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.
“Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Bandari ya Mwambani, miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa ‘guarantee’ kwa mikopo ambayo inachukuliwa.
“Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni mwendelezo wa miradi ya kitapeli,” alisema Zitto.
Zitto ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari unakwenda sambamba na reli ambayo itafika hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alimtaka Waziri Sitta kutoa taarifa kwa umma kwa kuwa taifa limechoshwa na miradi ya kitapeli.

MWANASHERIA ATOA UTETEZI
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo hivi karibuni, msimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, Cathbert Tenga, alisema utamilikiwa na Watanzania wenyewe na si watu kutoka nje ya nchi kama ilivyo katika miradi mingine.
“Sisi hivi sasa tunahangaika kuhakikisha nchi hii inasonga mbele kwani mradi huu hivi sasa upo katika hatua za awali za upembuzi yakinifu kwa kuwa na timu ya wataalamu, na ili jambo hili liweze kusonga mbele ni lazima siasa ziepukwe,” alisema Wakili Tenga.
Alisema kutokana na juhudi wanazoendelea nazo hadi sasa wamefanikiwa kupata benki ya Afrika Kusini, DBSA, ambayo itafanya kazi katika mradi huo mkubwa nchini.
Tenga alisema mradi huo wa MWAPORC utakuwa ni moja ya nguzo kwa uchumi wa taifa ikiwa Serikali itaamua ufanyike kwa kuwaunga mkono Watanzania wazalendo badala ya kujali wageni pekee.

MWIGAMBA NA UMASKINI
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.
“Wakati Rais Jakaya Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya, lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi chake cha uongozi, uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.
“Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini, lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki watazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa,” alisema
Mwigamba.
Alisema pamoja na tanzanite kuchimbwa nchini, lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini hayo ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.
 
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto kabwe, ameshutumu watuhumiwa wa Akaunti ya Tegeta Escrow kupewa kazi(zabuni) ya ujenzi wa bandari ya Mwambani mkoani Tanga bila kufuata taratibu.

Zitto amesema Rugemarila amepewa zabuni hiyo yenye thamani ya shilingi trilioni 54 bila kufuata taratibu za zabuni ikiwa ni pamoja na zabuni hiyo kutangazwa.

Kwa taarifa zaidi tembelea: Mtanzania-Gazeti la Kiswahili la kila siku

My take:
Hivi hii nchi ina laana?

Kama tuhuma hizi ni za kweli,viongozi wa nchi hii mko wapi na mnafanya nini maofisini?!

Mkuu hiyo figure ni kweli au? maana hizo pesa ni sawa na budget ya tanzania kwa miaka mitatu.
 
Back
Top Bottom