Zitto amkanya ndugu Jussa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Zitto Kabwe
Ndugu Jussa, Kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif Kama kiongozi thabiti. Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia Kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF. Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe unajua alishinda Urais wa Zanzibar iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid?

Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi Bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya.

That is my appeal to you as a friend and a fine politician.
 
Zitto,
CUF ni kama vile unavyoiona ManU, Liverpool, Blackburn,...., hivi ni vilabu vya England lakini wamiliki wake sio WAINGEREZA. CUF sio ya WATANZANIA ingawa kuna akina Lipumba, Mtatiro,..., na umefanya vizuri kumwomba Jusa na sio Lipumba. Tafakari.
 
HR anajua analolifanya na ametarajia matokeo ya aliyoyafanya alishaichoka Cuf muda mrefu na ameshajipanga kuanzisha chama kipya CCM C, anavuta pumzi tu kidogo. Wala msiumize kichwa.
 
Zito anaomba hekima zitawale pia CDM kwa vile anategemea kugombea Urais 2015, ukitilia maanani ndani ya CDM hakuna upana wa demokrasia
 
Zitto Kabwe
Ndugu Jussa, Kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif Kama kiongozi thabiti. Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia Kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF. Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe unajua alishinda Urais wa Zanzibar iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid? Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi Bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya. That is my appeal to you as a friend and a fine politician.

Nafikiri Zitto inambidi afikirie vingine.

CUF nafikiri ni chama tofauti sana na ni chama cha wananchi sio cha watu wacheche ambao wanakuwa na hisa kama Chadema.

Kufukuzwa kwa hamad Rashid sio jambo geni. Kwani walishawahi kufukuzwa watu maarufu kuliko Hamad rashid, akina Naila Jidawi, Mapalala na Msabaha n.k.

Kinachofuatwa ni haki na sio upendeleo.

Sio kama ulivyo fanyiwa wewe mizengwe uliyowekewa wewe ulipotaka kugombea uenyekiti wa taifa chadema.
 
@mr ziro.................. kila mtu anajua maalim seif alishinda ule uchaguzi wa awali na salmin, hadi channel 10 by then kwa sababu ilikua inamilikiwa na mzungu haikuogopa kutangaza kua seif ameshinda only the following day matokeo kugeuzwa!
 
zitto,
cuf ni kama vile unavyoiona manu, liverpool, blackburn,...., hivi ni vilabu vya england lakini wamiliki wake sio waingereza. Cuf sio ya watanzania ingawa kuna akina lipumba, mtatiro,..., na umefanya vizuri kumwomba jusa na sio lipumba. Tafakari.

hilo nalo neno!
 
Nafikiri Zitto inambidi afikirie vingine.

CUF nafikiri ni chama tofauti sana na ni chama cha wananchi sio cha watu wacheche ambao wanakuwa na hisa kama Chadema.

Kufukuzwa kwa hamad Rashid sio jambo geni. Kwani walishawahi kufukuzwa watu maarufu kuliko Hamad rashid, akina Naila Jidawi, Mapalala na Msabaha n.k.

Kinachofuatwa ni haki na sio upendeleo.

Sio kama ulivyo fanyiwa wewe mizengwe uliyowekewa wewe ulipotaka kugombea uenyekiti wa taifa chadema.
Kuna namna ya kumwondoa Maalim Seif angalau kwenye Ukatibu Mkuu tu?
 
Zito anaomba hekima zitawale pia CDM kwa vile anategemea kugombea Urais 2015, ukitilia maanani ndani ya CDM hakuna upana wa demokrasia
Kauli zako hizi....ukiwa muongo basi angalao uwe na kumbukumbu.ulichoandika mwaka jana kuhusu chadema ,kinakinzana na ulichoandika hapa.
 
Zitto ni "mwenyekiti wa vyama vyote vya upinzani" lol
Hapana. Kama Mtanzania anayekerwa na wimbi hili la kufukuzana uanachama ili mtu aukose Ubunge. Sema tu amechelewa mno kuutoa ushauri huu kwa rafiki yake Jusa ili umfikie Maalim.
Zitto, ongea na Tendwa juu ya suala hili.
 
Kufukuzana uanachama kumefanyika kwa vyama vyote kuanzia CCM, Chadema, NCCR, na sasa CUF

Tunaikula hasara ni wananchi kwa kugharamia chaguzi kila leo, kwa maamuzi ya wachache kwenye vyama
 
Mbona Zitto hakumwambia Slaa awavumilie WALE MADIWANI wa Arusha? Same ol' shit!
 
Nafikiri Zitto inambidi afikirie vingine.

CUF nafikiri ni chama tofauti sana na ni chama cha wananchi sio cha watu wacheche ambao wanakuwa na hisa kama Chadema.

Kufukuzwa kwa hamad Rashid sio jambo geni. Kwani walishawahi kufukuzwa watu maarufu kuliko Hamad rashid, akina Naila Jidawi, Mapalala na Msabaha n.k.

Kinachofuatwa ni haki na sio upendeleo.

Sio kama ulivyo fanyiwa wewe mizengwe uliyowekewa wewe ulipotaka kugombea uenyekiti wa taifa chadema.

kama cuf ni chama cha wananchi mbona hao wananchi hawakikuchagua!? Kwani Profesa Abdallah Safari cuf walimdanyiaje alipogombea uenyekiti!? Kwani kilichomfukuzisha Hamad Rashid si huo ukatibu mkuu! Wewe ni Dr lakini nashangaa huwa unafikiri chini ya kiwango!
 
kuwa na jina la chama cha wananchi kakumaanishi hicho chama ni cha wananchi kweli. Ukisema Zitto kawekewa zengwe kugombea uenyekiti CDM, alichofanyiwa HR kisa tu kutaka kugombea ukatibu wa CUF sijui utaitaje?
Nafikiri Zitto inambidi afikirie vingine.

CUF nafikiri ni chama tofauti sana na ni chama cha wananchi sio cha watu wacheche ambao wanakuwa na hisa kama Chadema.

Kufukuzwa kwa hamad Rashid sio jambo geni. Kwani walishawahi kufukuzwa watu maarufu kuliko Hamad rashid, akina Naila Jidawi, Mapalala na Msabaha n.k.

Kinachofuatwa ni haki na sio upendeleo.

Sio kama ulivyo fanyiwa wewe mizengwe uliyowekewa wewe ulipotaka kugombea uenyekiti wa taifa chadema.
 
Hivi kwanini zito anamwambia Jusa badala ya maalim Seif? Hata hivyo HR wakati anaanza kampeni yake ya kunia ukatibu mkuu cuf alijua kama atashindwa atafanyiwa nini ndo maana ameshatangaza kuanzisha ccm c
 
Back
Top Bottom