Zitto hajielewi na haeleweki. Ndo maana nikasema sisi wengine tulishaliona hilo zaidi ya miaka 7 iliyopita. Zamani nilikuwa namuunga mkono lakini akaja kunipoteza. Sasa naona CHADEMA nao wameshindwa kumvumilia na wameamua kumtimua.
Sasa subiri uone huko kwingine atakakoenda (kama ataamua kubaki kwenye siasa). Nako natabiri atawasumbua na watamtimua unless aanzishe chama chake mwenyewe (kama ACT siyo chake). Na hata akianzisha chama chake mwenyewe sidhani kama atakuwa na wafuasi wengi.
Mimi sio mganga wa kienyeji, hizo hadithi za utabiri nitakuachia wewe na hao wa sampuli hiyo. I stick to verifiable facts.
Awesome. Now let's go line by line.
Na matokeo ya hiyo hoja yalikuwa ni yepi? Hakuna mwingine aliyekuwa na hoja kama hiyo?
Matokeo Waziri mkuu alibaki, lakini ilijenga precedent ambayo ni muhimu kwa siasa za Tanzania, kuwa Waziri mkuu can be removed, if deemed incompetent. Sitegemei wewe kuelewa umuhimu wa precedent, kama umeamua kuona hilo ni jambo dogo, Sikumbuki on top of my head, but i can confidently say, hakuna aliyepeleka hoja kam hiyo toka upinzani Tanzania kwa miaka 20 kadhaa ya upinzani. So, yes, for an MP, this is an achievement.
Oh kumbe alishirikiana na wana-CHADEMA wenzie? Mi nilidhani labda alifanya hivyo single-handedly!
Hakuna wabunge wengine waliowahi kufanya hivyo?
Uliuliza Mafanikio ya Zitto, sasa mbona unaanza kusogeza goli?hakuna binadamu anayefanya kazi peke yake, hata mcheza tennis akishinda anashukuru timu yake na sponsors.it's the gentleman thing to do. Wabunge wa CHADEMA waliowahi kuleta hoja za Kitaifa zilizozizima mwaka mzima na viongozi wakuu wa serikali kuwajibika hawajai kiganja kimoja cha mkono, kama unakataa hilo umeamua tu kukataa. Kama unawajua wataje hapa, kinyume na hapo hizo zitakuwa chuki binafsi kwa mafanikio yaliyo wazi.
Hizo reforms unasema alizisimamia yeye na 'wenzake'. Hao 'wenzake' ni akina nani? Again nilidhani labda alifanya hivyo singe-handedly kumbe napo alikuwa na 'wenzake' who shall remain nameless....
Kila kiongozi wa taasisi ana haki ya kimsingi ku-take credit ya mafanikio ya taasisi anayoiongoza, yeye kama mwenye kiti wa PAC, ni haki yake ya kimsingi kuhusishwa na mafanikio ya kamati anayoiongozam unajua kuna kamati ngapi bungeni? unaweza taja kamati 5 tu zenye level ya public impact and awareness kuzidi PAC? humu ndani kila mtu yuko tayari kumrushia JK lawama, wakati anaongoza nchi yenye viongozi maelfu kwa maelfu,kwa nini?kwa sababu siku zote the buck stops at the top. Usijifanye hujui hili, you are better than that. Stop playing dumb please.
Naam, umezipa jina kuntu kabisa kuwa ni 'kelele zake' maana bila kutaja majina mahsusi na kiasi cha pesa walichonacho huko Uswisi ni makelele tu na mimi siwezi kumpa credit kwa kelele tu.
Sometimes, kelele is better than keeping quite, i respect a politician who says what they believe than one that hide behind neutral and party lines. Hizi Kelele kuna taasisi zimeundwa kwa ajili ya kupiga hizi kelele, Twaweza comes ti mind. Kelele ni jambo muhimu sana kwenye demokrasia na utawala bora. Sasa hivi kila kiongozi anayetaka kuweka fedha Uswisi atajifikiria mara mbili, kwangu hii ni hatua na mafanikio ya mpiga kelele.angekaa kimya kusingekuwa na uwazi uliopo sasa ambao hadi head of PCCB yuko obliged kuchunguza hizi fedha na kuzitolea ufafanuzi kwa PAC pamoja na mihimili mengine ya serikali.
Haki za wasanii hata Sugu huzipigania. Kuhusu uwepo wa uwazi wa mikataba nayo wapo wengi tu ambao hujenga hoja kama hiyo. Kupinga rushwa hata CCM wapo wanaopinga rushwa. Sioni kilicho special kwa Zitto hapo.
Shida yako unataka mafanikio ya ZITTO yawe null and void the moment wahusika wengine wakiwa na mafanikio yanayofanana, guess what, the world does not work like that. Federer being a a grandslam champion does not make nadal any less of a champion, it makes them both champions, This is not a zero sum game where only one can and must exists.This is too petty from you.
Una uhakika wabunge wote wa upinzani hakuna waliyoyafanya hayo unayodai Zitto kayafanya?
Wako wachache sana, na hawajai viganja vya mkono nikiwahesabu, kama unadhani nadanganya au siko sahihi si vibaya ukayataja majina yao hapa kila mtu aweke maoni yake, unaogopa nini kuwataja?
Hata Zitto hana tofauti na hao unaowaponda. Pia, naye ana kashfa za tuhuma dhidi yake vilevile.
Hakuna sehemu nimesema ZITTO hana mabaya yake, nimesema mapungufu yake yanazidiwa na mazuri, kutokana na ubora wa mambo mazuri aliyoyafanya kama mbunge wa upinzani na mwanasiasa wa Tanzania.
Nadhani sasa kajua kuwa hata yeye ni expendable.
Politically, this is not a win for CHADEMA, they are not better without him and they know it. We have seen what happened the year after they sidelined him, the best they could do was align themselves with UKAWA, and the best political event of the year came from two politicans they dismissed from CHADEMA, Zitto and Kafulila.
I don't see how ZITTO is being expendable here..,