Zitto amefeli Leadership Qualities

Zitto amefeli Leadership Qualities

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHAEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zito mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama. Huna haja ya kusukuma mzoga uzidi kuzama majini kama unajua kuwa tayari hauna uhai.

Kaka Kichuguu, Hapo CHADEMA hawajakurupuka, ila wamemuwahi Zitto, kwa vyovyote vile ilikuwa ni vigumu kwa Zitto kuendelea kuwa ndani ya Chadema, Zitto haelewani na almost top layer yote ya chama (Slaa, Lissu na hata Mbowe kwa sasa) sasa atafanyaje siasa zake humo,

timing ya Zitto ilikuwa ni yeye kuwapiga chini Chadema na kweli angefanikiwa kwenye hilo yeye ndio angeonekana kaiacha Chadema na kisiasa angalau angepata Kanguvu fulani ka kusimamia,
1. Chadema wamewahi kumfukuza Zitto ili angalau wamzoofishe kisiasa kokote aendako na kwa Wananchi kwa ujumla,
2. Chadema wanaionyesha Jamii kuwa Zitto ni Mwanasiasa Mzuri lakini sio Mwaminifu,
3. Chadema wanaionyesha jamii kuwa wao wanauwezo wa Kufanya maamuzi magumu
4. Chadema wanaionyesha Jamii kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya Chama,
5. Chadema wanaionyesha jamii kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka ya kufunja katiba bila kushughulikiwa
 
mmh kabla ya zitto kwenda mahakamani CDM hawakusimamia katiba!! yaani katiba inasimamia kwa vitu vya ku favor upande huu na inavunjwa kwa vitu ambavyo havi ku fevi

Pole kaka, Ndio Siasa Zilivyo, Najua ulivyoumia kaka

Lakini nadhani ni muda muafaka kwa Zitto kwenda chama kingine, kwa sababu kama wenzie "hawamtaki" kwa sababu yoyote ile kwa nini alazimishe kuwa nao
 
HAKI YA KWELI IPO KWA MUNGU DUNIA NI DHULUMATI.
PUMZIKA KWA AMANI RASTA MAN CHACHA WANGWE, JANA TAREHE 10 ZITTO KAFUTWA UANACHAMA NA WANACHAMA WALIOJIUNGA CHADEMA 2004. WAKATI ZITTO ANA ZAIDI YA MIKA 20 CDM.

Ukiandika hata kwa herufi ndogo tutakuelewa mkuu, inaonyeshwa umeguswa moja kwa moja na kufukuzwa kwa zitto, ila tambua wanasiasa wengi ni waongo sana na zitto ni kati ya hao waongo.
 
Lema amehamia Chadema mwaka 2009 Lakini ana nguvu kupita wakina Slaa na Mdee kisa ni kipenzi cha Mtei na Mbowe

we we kweli hamnazo, hivi warioba,butiku na salimu walijiunga link ccm had I wapuuzwe na wahuni mliopo Leo?
 
Chadema niliikubali sana lakini kwasasa naona wamejipiga bao wenyewe,wanajali maslah binafsi kuliko ushauri wawanachama mtu kushauri mabadiliko ya uongozi wajuu nidgambi?kwakweli hiki chama kijitafakari maana kinafanya maamuzi magumu mno,yanayoweza kukigharim chama
 
Kwa stahili hili hii ya ubabe,Chadema bado sana kuchukua nchi.Bado chama hakijakomaa kidemokrasia.

wananchi tumeishaamua kuwapa CHADEMA nchi, mpaka napoandika post hii sijapata taarifa zozote kutoka CHADEMA zinazodai hawako tayari, labda unipe maelezo ya ziada mkuu.
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k

Kamuulize lowasa kwanini bado kajibanza ccm pamoja na kuitwa fisadi na viongozi wakuu wa chama chake...?? Sababu anajua na kutambua yeye sio chama nawala akitoka ccm itaendelea mbele....
 
Tuingalie kutumia kurunzi ya leadership qualities and skills. Baada ya kwenda mahakamani na kuweka pingamizi, Zito alikuwa amejepiatia muda wa zaidi ya mwaka mmoja kujionesha kama kiongozi mzuri kwa kufanya mambo mawili tu: (a) kuunganisha tena wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamekorofishana kutoka na ule "Mkakati;" halafu, (b) baada ya kukamilisha hilo la (a) hapo juu angekwenda mahakani kufuta kesi na kusema sisi sote na wamoja na tuna lengo moja, malumbano hayafai kwa hiyo hakuna kesi baina yetu. Ila inaonekana Zitto alikuwa ama ana-buy time ili aendelee kuwa mbunge, au alikuwa na confidence kubwa sana kuwa atashinda kesi ambayo sote tunafahamu kuwa ameshindwa. Ku-buy time ili aendelee kuwa mbunge siyo sifa nzuri ya uongozi kwani unakuwa ni kiongozi anayeangalia maslahi yake tu. Vile vile kuwa na overconfidence kuwa utashinda halafu ukashindwa pia siyo sifa nzuri ya uongozi kwa utakuwa ni kiongozi atakayepeleka watu wake pabaya.

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHAEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zito mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama. Huna haja ya kusukuma mzoga uzidi kuzama majini kama unajua kuwa tayari hauna uhai.

Mleta uzi umeleta angalizo muhimu sana na umechambua vizuri. Mimi nadhani kwenye kuathirika ni kila mmoja atapata madhara kutokana na kile kilichotekea jana kwa Zito yaani cdm na huyo Zito wote lazima watapata madhara fulani. Ila nilichokigundua kwa Zitto ni kwamba alikuwa ameshakichoka cdm na cdm kwa upande wake kilifikia mahali kikamchoka pia, kwa hiyo ili kila upande upate kile ukitakacho ni bora kuachana ili mambo yaendelee.

Kwangu mimi kwa upande wa Zitto nadhani yuko na marafiki ambao si sahihi na kwa kiasi kikubwa wamekuwa ni sehemu ya tabia yake. Kwa mfano siku moja alikwenda Star Tv rafiki yake mmoja aitwaye Habib Mchange akiwa na John Mnyika, kwa kweli siku ile ndio niligundua Zitto yukoje maana ndege wafananao huruka pamoja, kwa kweli yule kijana aliongea siasa za kipuuzi na kupakana matope katika hali ya kipuuzi kabisa. Alifikia mpaka mahali akasema waliomua Daudi Mwangosi ni cdm na ushahidi anao!! Hivi katika akili ya kawaida nani ambaye hakujua Mwangosi aliuwawa na nani? Kwa bahati mbaya sana Zitto hawa ndio marafiki zake na wakati wa press conference huwa wako mbele. Sasa katika muktadha huu ulitegemea kwamba Zitto alikuwa ni mtu anayejali haiba ya cdm kukua ama kuanguka? Na kama unaamua wewe na rafiki zako kuchafua haiba ya chama tena kwa approach zile za kiccm unategemea wenzako hawatakuweka katika kundi la wasaliti? Tuchukulie hili limekwisha tuanza maisha mapya, kwa Zitto hili liwe fundisho ili limjenge zaidi huko aendako na ajifunze kulinda haiba ya chama chochote atakachoenda ikiwepo na kuchagua marafiki sahihi.

Kwa upande wa cdm, ni kweli hata wao kwa kiasi fulani hili suala lao na Zitto lilipata maamuzi fulani ya kimihemuko ambayo kwa kiasi fulani kulihitajika busara zaidi ya hiki kilichotokea. Lakini changamoto kubwa ninayoiona na ambayo ni dhahiri hasa huko tuendako ni hiki kifungu cha ukomo wa madaraka. Wapende wasipende ni vyema katiba ikafanyiwa marekebisho na kifungu hiki cha ukomo wa madaraka kiweke wazi muda halisi wa kuachia madaraka na mimi ninashauri isizidi miaka kumi kwa ngazi za juu. Eneo hili ndio hasa kiini cha mgogoro wote uliojitokeza na sidhani kama itakuwa imefikia mwisho baada ya Zitto kuondoka kwani huko mbeleni kutazua tu tafrani. Naamini ukiona mahali panaleta mkwaruzano na kuhoji kwingi na hasa kama kifungu chenyewe kimeondoka kwa utata, kwa sisi ambao dhamira zetu zinatutuma kusema kweli tunabaki na shaka na tutapenda utata huo kuondolewa haraka.

Hitimisho kwangu hapa mimi sioni mshindwa na mshindi bali naona wote cdm na Zitto kunufaika na changamoto hii kwani wote huko mbele ya safari itawasaidia kuwa bora zaidi japo watakuwa kwenye mabasi tofauti.

CC: Dr. W.Slaa, Zitto, Kitila Mkumbo, Betlehem, Pasco, Nguruvi3, Godbless Lema, John Mnyika, Ben Saanane
 
...

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHADEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zitto mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama.

....

Hiyo red; hivi ungekuwa wewe ndiye Mwanasheria Mkuu wa Chadema then baada ya uamuzi wa jana wa Mahakama ukaulizwa na waandishi wa habari juu hatma ya Zito nani ya Chama, ungefanyaje? Ungekaa kimya tu? Tungekuona una kiburi! Tundu Lissu ndiye msemaji rasmi wa Chama juu ya masuala yote ya kisheria na kwa kweli ametimiza wajibu wake kikamilifu. Tatizo lenu mnataka mijitu isiyotimiza wajibu na mioga kuchukua maamuzi hali iliyotufikisha hapa tulipo kama taifa.
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k

Kiongozi mzuri ni yule anayejishusha hilo tu ndugu Yangu. Hata hivyo zitto anayonafasi ya kujishusha kama anataka akumbukwe katika taifa letu. Nampenda Zitto lakini inabidi ajishushe na ndivyo tunavyoishi katika jamii zetu.
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k

ZZK alishaondoka CHADEMA na wenzie Akina Kitila na Mwigamba siku nyingi.. Hata huko aliko tangu mwaka jana (ACT)kunafuka Moshi.. Kuendesha chama cha siasa kwa nchi kama Tanzania na hasa ukizingatia maCCM yanavyoweka nguvu nyingi kwenye fitna za kijinga zaidi ya maendeleo ya wananchi ni shida sana... ZZK ajitafakari upya bado ni potential katika siasa za nchi hii. Ajipange upya ila ACT will never be a gud move for him, Ningekua yeye ningeomba upya uanachama CDM then start afresh!!
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k
Kwa nini ni wana CCM ndio wanaona umuhimu wa Zitto kubaki CHADEMA?
 
Tuingalie kutumia kurunzi ya leadership qualities and skills. Baada ya kwenda mahakamani na kuweka pingamizi, Zito alikuwa amejepiatia muda wa zaidi ya mwaka mmoja kujionesha kama kiongozi mzuri kwa kufanya mambo mawili tu:

(a) Kuunganisha tena wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamekorofishana kutoka na ule "Mkakati;" halafu,

(b) Baada ya kukamilisha hilo la (a) hapo juu angekwenda mahakani kufuta kesi na kusema sisi sote na wamoja na tuna lengo moja, malumbano hayafai kwa hiyo hakuna kesi baina yetu.

Ila inaonekana Zitto alikuwa ama ana-buy time ili aendelee kuwa mbunge, au alikuwa na confidence kubwa sana kuwa atashinda kesi ambayo sote tunafahamu kuwa ameshindwa.

Ku-buy time ili aendelee kuwa mbunge siyo sifa nzuri ya uongozi kwani unakuwa ni kiongozi anayeangalia maslahi yake tu.

Vile vile kuwa na overconfidence kuwa utashinda halafu ukashindwa pia siyo sifa nzuri ya uongozi kwa utakuwa ni kiongozi atakayepeleka watu wake pabaya.

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHADEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zitto mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama.

Huna haja ya kusukuma mzoga uzidi kuzama majini kama unajua kuwa tayari hauna uhai.

mkuu,katiba ya CDM inasema mwanachama akikipeleka chama mahakamani,basi huyo atakuwa si mwanachama tena,hivyo swala la yeye kufuta kesi ile halikuwepo na lisingekuwa na tija kwakwe kwani mwisho wa siku angevuliwa tu uanachama.
 
mmh kabla ya zitto kwenda mahakamani CDM hawakusimamia katiba!! yaani katiba inasimamia kwa vitu vya ku favor upande huu na inavunjwa kwa vitu ambavyo havi ku fevi

Unaweza kutuambia kwa namna ghani chadema hawakufata katiba
 
Tuingalie kutumia kurunzi ya leadership qualities and skills. Baada ya kwenda mahakamani na kuweka pingamizi, Zito alikuwa amejepiatia muda wa zaidi ya mwaka mmoja kujionesha kama kiongozi mzuri kwa kufanya mambo mawili tu:

(a) Kuunganisha tena wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamekorofishana kutoka na ule "Mkakati;" halafu,

(b) Baada ya kukamilisha hilo la (a) hapo juu angekwenda mahakani kufuta kesi na kusema sisi sote na wamoja na tuna lengo moja, malumbano hayafai kwa hiyo hakuna kesi baina yetu.

Ila inaonekana Zitto alikuwa ama ana-buy time ili aendelee kuwa mbunge, au alikuwa na confidence kubwa sana kuwa atashinda kesi ambayo sote tunafahamu kuwa ameshindwa.

Ku-buy time ili aendelee kuwa mbunge siyo sifa nzuri ya uongozi kwani unakuwa ni kiongozi anayeangalia maslahi yake tu.

Vile vile kuwa na overconfidence kuwa utashinda halafu ukashindwa pia siyo sifa nzuri ya uongozi kwa utakuwa ni kiongozi atakayepeleka watu wake pabaya.

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHADEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zitto mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama.

Huna haja ya kusukuma mzoga uzidi kuzama majini kama unajua kuwa tayari hauna uhai.

Mkuu, mengine yote ni sahihi kabisa. Nina wasiwasi na hapo penye RED....hebu tusaidiane kutafakari upya, maana kwa maoni yangu, Chama cha siasa sio kanisa, ambapo leo ukirudi kiimani kesho ukiombas na kutubu unarudishwa kundini.
 
Kwa stahili hili hii ya ubabe,Chadema bado sana kuchukua nchi.Bado chama hakijakomaa kidemokrasia.
Duuhh, kazi kweli kweli. Huku nchi hii inahitaji chama na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi huku Chadema wababe. Kama chama kimefuata Katiba na mahakama ikaridhia ubabe upo wapi?
 
Ngumu kumeza duh! ni vyema wanachama wa Chadema wakaamua kufikiria kuwa ndani ya miaka 7 hadi 10 inayokuja kutokana na hali hii ya kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe hadi kufikia huko hali itakuaje?

Nilitegemea maamuzi yaliyochukuliwa jana yangetoka Chama kingine...............na sio CHADEMA.
 
bye bye zito kaungane na ndugu yako mnafiki mwenzio january kupiga propaganda kwenye radio yenu ya fursa kuwa eti nyio ndio vijana wazalendo, poor zito nenda kajiuguze
 
CHADEMA kimedhihirisha kuwa kimejaa viongozi makatili na wenye chuki,mbaya zaidi kuna ma padri na ma ustadhi.
 
Back
Top Bottom