Zitto alonga

Zitto anamaanisha nini hasa pale anaposema Katiba haitapatikana barabarani?


Labda alimaanisha kuwa katiba haitapatikana kule walikokutana JK na Lowassa. Lowassa mara nyingi amekuwa akisisitiza kuwa hawakukutana na JK barabarani.........ni mawazo yangu tu.
 
"Watakwenda, watarudi. Hawana mwingine wakumlilia kwa yao ,hawana mwingine wakuomba yao yatimie isipokuwa serikali ya chama cha mapinduzi, ambayo mie ndo rais wake"
Jakaya Kikwete 18-11-2010
 
Anamaanisha CDM iachane na upuuzi wa MAANDAMANO ya kijinga.

Badala yake wahamasishe wafuasi wao wafanye kazi kulijenga taifa letu.
 
"Katiba haitapatikana barabarani bali kwa mwafaka wa Kitaifa. CHADEMA iliomba kukutana na Mkuu wa Nchi kwa sababu maalumu zinazohusiana na mchakato wa Katiba. Kama kuna vyama vingine navyo vinataka kumwona Rais wafuate utaratibu wao. Pia tangu lini CCM ikaanza kusemea vyama vingine? Rais ana taratibu za kukutana na raia wake. CCM na vyama vingine visidandie mkutano wa Rais na viongozi wa chama chetu @Nape" -Zitto Kabwe

Too low from you Zitto! Kitendo cha KK ya CCM kuagiza Rais akutane na vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni ndio hasa mwanzo wa utekelezaji wa ule mpango mahsusi wa kuipotezea muda CDM. Hata hivyo CCM ina haki ya kutoa maagzo kama hayo kwa kuwa huyo mkuu wa nchi yupo pale kwa tiketi ya CCM na mnutano/mikutano na vyama vya siasa ni jambo kuwa linalohitaji baraka za vikao vya chama. Mkakati mzima wa CCM kutaka Rais akutane na vyama vyote ni kuwadhalilisha wapinzani kwa kuwa badala ya kudai katiba mtaanza kuzogodoana wenyewe kwa wenyewe mbele ya Rais kama ambavyo umeanza kwa kutoa kauli "vyama vingine visidandie mkutano wa Rais na viongozi wa chama chetu"

Ni byema na wote mnaopeperusha bendera ya kudai mabadiliko ya katiba mkatambua kuwa without a united opposition CCM itawagaragaza katia kila hoja mtakayoleta mbele kwa kutumia migawanyiko yenu. Nilitegemea kuwa Zitto kama kijana ungelitambua hilo mapema na kuendelea kusukuma ajenda ya vyama vya upinzani kuunganisha nguvu. Angalau hata wewe kidogo inaelekea una mawasiliano na wanasiasa wenzako katika vyama vingine k.m wakati wa ajili ya MV Spice Isander nilikunukuu kuwa Mhe Jussa wa CUF aliwasiliana na wewe kuhusu ajali hiyo. Hi mlilinipa tumaini kuwa angalau siku moja tutaweza kuona vyama vya upinzani mmekaa meza moja.

Badala ya kupoteza muda na kupotezewa muda na mkutano wa Rais, ni vyema vyama vya upinzania mngekutana na kuondoa tofauti zenu ili angalau katika hiki kipindi cha mchakato wa marekebisho ya katiba mkapractice kuwa united front. Nina hakia such a move will pay tremendously rather tham wasting time at the state house.

Mkakati mwingine ambao unaweza kuza matunda ni kwa wabunge mkaanza kutoa elimu katika majimbo yenu kuhus mambo ambayo wananchi wanatakiwa kuyakata katika katiba k.m madaraka makubwa ya rais, uwepo wa wakuu wa mikoa na wilaya, mawziri kutokana na wabunge n.k
 
Anamaanisha CDM iachane na upuuzi wa MAANDAMANO ya kijinga.

Badala yake wahamasishe wafuasi wao wafanye kazi kulijenga taifa letu.


Zito akipewa uwenyekiti wa chadema, kitapoa na kufa kama NCCR Mageuzi. Just a warning from the wilderness...
 
Barabara ndo kila kitu mkuu...historia zipo nyingi sana,majadiliano yana kikomo ikishindikana front road.
 
Nape ndiyo msemaji wa Magamba na hana tofauti na aliyekua msemaji wa "Hayati" Sadam Hussein pale Iraq.
Busara ya kuonana na Rais wa nchi ilianzia chama makini chenye nia ya dhati ya ustawi wa taifa hili. Nini kitakachowasilishwa na hivyo vyama vingine wakati vimeunga mkono mjadala uliowasilishwa na serikali inayotawala sasa? Tofauti ya vyama hivyo na kinachotawala iko wapi mpaka wahitaji tena kukutana na Raisi kwa mgongo wa CDM? Kama kweli Jamaa wa kijani wanataka kuendelea kuwepo wavunje ndoa yao haraka na huyu dogo.
 
Huyu jamaa mara nyingine huwa simulewagi kabisa, nahisi anamaanisha kuwa katiba haipatikani kwa kuandamana. Kwa mtazamo wangu kwa Zitto katiba mpya sio muhimu kwa sasa kwa kuwa hajafikisha umri wa kugombea urais na ameishaprove kuwa hachakachuliki katika ubunge baada ya kushinda mara mbili. Na hata wenzie walipotoka bungeni siku ile JK anazindua bunge yeye alionekana kuwaponda. Lets wait and see but the guy is very controversial.

Zitto nafikiri bado yuko kwenye maruweruwe ya madawa ya usingizi wakti akifanyiwa operesheni kule India!
Katiba nyingi duniani zimepatikana kwa MAANDAMANO. Watu walipinga mfumo fulani mahali fulani na kukafanyika mageuzi yaliyopelekea kuundwa ka Katiba Mpya
.

Tuchukue mfano rahisi tu wa Baba wa Demokrasia duniani. The USA Constitution:

Shays' Rebellion
was an armed uprising in central and western Massachusetts (mainly Springfield) from 1786 to 1787. The rebellion is named after Daniel Shays, a veteran of the American Revolutionary War.
The rebellion started on August 21, 1786, over financial difficulties and by January 1787, over one thousand Shaysites had been arrested. A militia that had been raised as a private army defeated an attack on the federal Springfield Armory by the main Shaysite force on February 3, 1787, and five rebels were killed in the action.
In the aftermath, fear spread that the American Revolution's democratic impulse had gotten out of hand. This fear, combined with the lack of institutional response to the uprising, energized calls to reevaluate the Articles of Confederation and gave strong impetus to the Philadelphia Convention which began on May 17, 1787, which created the United States Constitution.

Shays' Rebellion - Daniel Shays organized farmers throughout New England to protest legislation that increased taxes and demanded immediate debt-repayment. When the state legislature refused to respond, Shays and his armed followers closed the courts in western Massachusetts in protest of foreclosed properties. The rebellion came to a head when Shays was defeated while trying to seize a federal arsenal of weapons in Springfield, Massachusetts, on January 25, 1787. This rebellion demonstrated the weaknesses of the Articles of Confederation, and convinced many states of the need for a stronger central government

Upinzani na maandamano kama haya ya Bwana Daniel Shay na wenzake yalipelekea kufanya mageuzi kwenye Katiba ya Marekani.
Sasa Zitto anaporopoka kuwa KATIBA HAIPATIKANI BARABARANI ni ufinyu wa mawazo na uvivu wa kufikiri. Yeye HAWEZI KUWA JUU YA CHAMA. He is a nut!
 
Nakupenda zitto ili mara nyingi unanikwaza, juzi Stela Manyanya alikujeruhi sana naomba ukipata mda umjibu kikamilifu
 
"Watakwenda, watarudi. Hawana mwingine wakumlilia kwa yao ,hawana mwingine wakuomba yao yatimie isipokuwa serikali ya chama cha mapinduzi, ambayo mie ndo rais wake"
Jakaya Kikwete 18-11-2010

Gadafi aliwaambia walibya maneno kama haya miaka zaidi ya 30 iliyopita, lakini kamalizia maisha yake kwa fedheha ya kuchokonolewa kwa vijiti. Hatutaki haya yaje yamkute rais wetu. Akae, asikilize matakwa ya wananchi na si wana CCM.
 
Hakuna haja ya kudandia mgongoni mwa chadema kama vyama vina hoja viombe kivyao.Wanataka waende na chadema wavuruge kama wanavyofanya bungeni. waende peke yao maana yaliyo pitishwa ni wao walipitisha
 
Zitto na JK huwa wanafanana kwa kuwa vigeugeu. Sitashangaa Zitto akija hapa na kukanusha hii kauli yake kiaina.
 
Zitto nafikiri bado yuko kwenye maruweruwe ya madawa ya usingizi wakti akifanyiwa operesheni kule India!
Katiba nyingi duniani zimepatikana kwa MAANDAMANO. Watu walipinga mfumo fulani mahali fulani na kukafanyika mageuzi yaliyopelekea kuundwa ka Katiba Mpya.
Kauli tata toka kwa huyu mtu hazijaanza leo. Huyu amewahi kuandika humuhumu akiwaambia wenzake wasimsakame na kudai kuwa walimtenda kwa pamoja Wangwe, sijui walimtenda nini.

Amewahi pia kabla ya uchaguzi wa mwaka jana kuandika kuwa wale wanaomwonea wivu nao wajipange, washinde ubunge ili waupate umaarufu. Target hapa alikuwa Mnyika. Hayo ni baadhi tu kwani uchafu aliokwisha post humu ni mwingi sana.

Nina mashaka kama alipokea ushindi wa vijana wa chama chake kwenye ubunge positively kwani anadhani yeye ndiye chama.
 
Zitto kweli ni msela tena kapinda kwelikweli huyu si mtu wa kumwamini kabisa ni mtu aliefilisika kisiasa hana lolote si chochote.Kupitia maandamano baada ya kashfa ya buzwagi ndo CHADEMA ikaanza kukubalika kanda ya ziwa sasa anapodai kuwa katiba inapatikana kwa majadiliano ni nani ni kweli? . .Mimi nadhani zitto bado anakinyongo na viongozi wa Chama chake kwamba analipiza kisasi kwa kupiga vijembe kila anapopata nafasi.Tulipokuwa TOSAMAGANGA haka kamtindo alikuwa nako sana na tulizoea kumuita Popo chakushangaza hadi tunamaliza UDSM haja onyesha kuachana na hii tabia kwani ina mcost sana na ndiomana hata demu wake jack alimtosa si mtu wa kumwamini asilimia mia moja.Waswahili walisema Ngoma ikilia sana basi inakaribia kupasuka hadi kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo kamanda ana zidi kupotea kwenye ukumbi wa siasa. It's a mutter of time let us wait and see. .! !
 
Simuamini kabisa Kabwe, ni mafiki sana.............. TUNATAKA MAANDAMANO period.:embarassed2:
 
"Katiba haitapatikana barabarani bali kwa mwafaka wa Kitaifa. CHADEMA iliomba kukutana na Mkuu wa Nchi kwa sababu maalumu zinazohusiana na mchakato wa Katiba. Kama kuna vyama vingine navyo vinataka kumwona Rais wafuate utaratibu wao. Pia tangu lini CCM ikaanza kusemea vyama vingine? Rais ana taratibu za kukutana na raia wake. CCM na vyama vingine visidandie mkutano wa Rais na viongozi wa chama chetu @Nape" -Zitto Kabwe


Nadhani mtazamo wa Zitto uko sahihi. Hivi chama kama CUF kina haja gani ya kukutana na rais wakati kiliunga mkono na kupiga kura pamoja na CCM kupitisha mswada wa sheria unaopingwa na CHADEMA? Au wana wasiwasi kuwa inawezekana rais akabadilisha msimamo na hivyo wangependa wawepo ili kupinga hoja zitakazotolewa na CHADEMA kwa rais?
 
Zitto kweli ni msela tena kapinda kwelikweli huyu si mtu wa kumwamini kabisa ni mtu aliefilisika kisiasa hana lolote si chochote.Kupitia maandamano baada ya kashfa ya buzwagi ndo CHADEMA ikaanza kukubalika kanda ya ziwa sasa anapodai kuwa katiba inapatikana kwa majadiliano ni nani ni kweli? . .Mimi nadhani zitto bado anakinyongo na viongozi wa Chama chake kwamba analipiza kisasi kwa kupiga vijembe kila anapopata nafasi.Tulipokuwa TOSAMAGANGA haka kamtindo alikuwa nako sana na tulizoea kumuita Popo chakushangaza hadi tunamaliza UDSM haja onyesha kuachana na hii tabia kwani ina mcost sana na ndiomana hata demu wake jack alimtosa si mtu wa kumwamini asilimia mia moja.Waswahili walisema Ngoma ikilia sana basi inakaribia kupasuka hadi kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo kamanda ana zidi kupotea kwenye ukumbi wa siasa. It's a mutter of time let us wait and see. .! !


Ndugu yangu Menny Terry nimesoma andiko lako kwa makini lakini sioni hoja ya msingi unayoijenga kwa yale aliyoyaongea Zitto zaidi ya kumshambulia yeye binafsi. Kama sikosei hoja ya CHADEMA kukutana na Rais ni ya chama chao na siyo ya Zitto na sidhani kama kwenye tamko lao waliondoa uwezekano wa maandamano. Nilichofanikiwa kujua kwenye andiko lako ni kuwa ulisoma na Zitto Tosamaganga na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kimsingi una kinyongo naye ambacho yumkini kimejengeka tokea huko mliposoma naye. Mengine ni hisia na mitazamo yako binafsi kuhusu Zitto. Mwisho nimeshindwa kabisa kuona uhusiano wowote kati ya huyo unayemwita Jack kuachana na Zitto na suala la mkutano wa CHADEMA na Rais. Ushauri wangu kwako ni: Try to be objective when you are commenting on issues related to Zitto because your hatred against him has severely impaired your reasoning.
 
Simuamini kabisa Kabwe, ni mafiki sana.............. TUNATAKA MAANDAMANO period.:embarassed2:

Watanzania ni waoga sana kudai haki zao,sasa sielewi ni kuwa hawafahamu haki zao au,,,?sababu hawaishi kuwa na maneno mengi bila vitendo.Wamisri walipambana wakashinda na sasa hivi wanapambana na na polisi na wanajeshi,sie Watanzania ni maneno tu mengi yasiofuatiwa na vitendo.Deusi Kibamba alitangaza na kuhamasisha maandamano ya amani,jeshi la polisi kuyapiga marufuku tu kanywea simsikii(nnadhani yatakuwa yamefutwa)Ndio maana nnafurahi kuwa ndani ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.Ngoja tumsikilizie ****** hapo magogoni anasemaje.
 
Back
Top Bottom