MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Wakati wa uzinduzi, nilikwenda Kigoma, kwa bahati mbaya Zitto hakuwapo, nilipouliza wapiga kura wake kuwa mbunge wenu yuko wapi, wengine walisema amehama, wengine walisema sijui yuko Busanda, ila mimi nasema, kwa hali niliyoiona kule jimboni mwake, 2010 Zitto itabidi ajipange sawa sawa, vinginevyo…
Huo ni ushauri anapaswa kuufanyia kazi na siyo kulaumu nilichokiona mimi Mhe waziri mkuu anampenda na ndiyo maana alimpa ushauri huo Mhe Zito..mipasho-mipasho ya namna hii bora wangeachiwa kina Makamba ,Tambwe Hiza, au Chief Whip wa CCM bungeni.
..washauri wa Mzee Pinda mkumbusheni kwamba yeye ni kiongozi wa SERIKALI bungeni, siyo kiongozi wa Chama/CCM bungeni.
..mipasho-mipasho ya namna hii bora wangeachiwa kina Makamba ,Tambwe Hiza, au Chief Whip wa CCM bungeni.
..washauri wa Mzee Pinda mkumbusheni kwamba yeye ni kiongozi wa SERIKALI bungeni, siyo kiongozi wa Chama/CCM bungeni.
Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majunguHashauriki huyu yaani ni bonge la mzigo, Mimi naamini hakuna waziri mkuu bomu kama huyu Tanzania tuna hasara kwelikweli....halafu waandishi na JF wanampamba sana sijui kwanini?
a) Aliwahi kuamuru mwezi aachiwe kwasbabu ni CCM leader amekuwa hakimu
b) Aliwahi kuamuru walioua albino wauawe, aliishia kulia bungeni kulinda mkate wake
c) Anamtetea hadharani Mkapa (Fisadi) sijui kwanini asikae kimya suburi sheria ifanye kazi
d) Sijaona alichofanya tangu apewe hiyo kazi statistcally amefungua miradi ya kanisa ya kanisa mara 70 zaidi ya miradi ya serikali ambayo yeye ndio msimamizi mkuu
Kwa ufupi he is "BOGUS PM, DULL"
Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majungu
Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majungu
Hapa Zitto katumia akili kumjibu huyu mzee. Kamjibu indirectly. Pinda lazima aone aibu kamshambulia mtu ambae kaishia kumjibu tu kiustaarabu na kuji kalia kimya.It's embarrasing to Pinda.
Hivi tunaongelea huyu mtu alikuwa anajulikana kama mtoto wa Mkulima wakati sasa anatuumiza wakulima wenzake kwamisafara mizito mikoani ? Ama anasema tu ni mtoto wa Mkulima baba yake na yeye si mkulima ?
Hivi tunaongelea huyu mtu alikuwa anajulikana kama mtoto wa Mkulima wakati sasa anatuumiza wakulima wenzake kwamisafara mizito mikoani ? Ama anasema tu ni mtoto wa Mkulima baba yake na yeye si mkulima ?
Lunyungu,
Waziri mkuu hapingi itifaki ya magari kwenye ziara zake mikoani hivyo suala la mtoto wa mkulima halina nafasi hapa
Masatu hata Sokoine na Nyerere walikuwa hawapangi itifaki lakini the good thing about them walikuwa wakikemea pale wanapoona kuna kufuru kama ya mtoto wa mkulima juzi Iringa. So Pinda anayo nafasi ya kusema no next time jamani sihitaji magari 80 kwenda kufungua ujenzi wa barabara. Bahati mbaya hatujaiona hiyo nia tuliyoitarajia kwa mtoto wa mkulima.
Kwa kuongezea jamani huyu mzee pinda nahisi kwamba huwa hafikirii vizuri kabla ya kutamka maneno. Au sijuwi kuna haja ya kumkumbusha kwamba yeye ni waziri mkuu huo ukada anapaswa kuuweka pembeni kwanza.
Hivi hiyo sheria yake aliisomea wapi Dar? Juzi kanichanganya kabisa kwa kweli kwa msisitizo kabisa anasema mkapa ni msafi lakini serikali itafanya uchunguzi. Sasa mzee Pinda kama umesema Mkapa ni msafi kuna haja gani ya kufanya uchunguzi? Huoni kama unaathiri uchunguzi wooote kwa kusema mkapa ni msafi? Nani unahisi atakupinga wewe? Hiyo pesa ya uchunguzi si ni heri ikanunulie madawati watoto wa darasa la 7 Mbagala wasiendelee kukaa chini wakati wa mitihani?
La pili, unasema Mkapa hakununua Kiwira kwa kuwa Kiwira imeshindwa kulipa hata mishahara. Kwani umeambiwa na nani kwamba sisi tunahoji uwezo wa kifedha wa Kiwira? Issue hapa Mkapa alikwenda kinyume kwa kujiuzia mradi wa thamani ya 4 billion kwa sh milioni 700 huku akiwa still ni rais. Whether hiyo kampuni yake ina uwezo wa kulipa mishahara au lah si issue kwetu mzee.
Miye nadhani huyu Zitto anapewa umaarufu ambao hata haumstahili. Zitto amepewa kichwa tu kutokana na kuwa msemaji kwa jazba ndani ya Bunge etc lakini hana upeo wowote mkubwa kisiasa kuweza kumjibu Waziri Mkuu kama ilivyoelezwa na mwandishi wa habari hiyo!
Eti:
Kuhusu Pinda kunishambulia bungeni jana kauli yangu ni hii. Ninamheshimu sana Pinda na sitaki malumbano nae. Namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia, alisema Zitto.
Hivi kweli kati ya Pinda na Zitto nani anayeelewa zaidi demokrasia kuzidi mwenziwe?!