Zitto akerwa na kauli ya Pinda

Sawa kabisa mzee maana PM wako siku hizi kauli zake zina utata mkubwa sana, tunashindwa kumuelewa hata kidogo, maana hata aseme vipi bado tunaendelea kuona kuwa CCM wanabaka demokrasia Tanzania
 
Mkuu huko kubandikwa jina "mtoto wa mkulima" unadhani ni kwa sababu gani? Si kwa sababu waziri mkuu aliyetoka Edward Lowassa alikuwa na skendo kibao na kila mtu alikuwa anajua ni tajiri sana. Sasa kumchagua Pinda ili kumtofautisha na EL ndiyo hiyo kupachikwa "mtoto wa mkulima" ili watu waone nae ni mwananchi wa kawaida. Kwa mshahara wa wabunge na mirupurupu mingine unadhani kuna mtoto wa mkulima mule? Yote ilikuwa tu politics ya kumuuza Pinda kwa wananchi.

Mtoto wa mkulima hakumegewa milioni 5 za EPA wakati wa uchaguzi 2005 zilizokuwa zikitolewa kwa kila mbunge?:eek:
 
Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majungu

Kama pinda kifaa naona kinakufaa wewe.......nyambafu!!
 
Miye nadhani huyu Zitto anapewa umaarufu ambao hata haumstahili. Zitto amepewa kichwa tu kutokana na kuwa msemaji kwa jazba ndani ya Bunge etc lakini hana upeo wowote mkubwa kisiasa kuweza kumjibu Waziri Mkuu kama ilivyoelezwa na mwandishi wa habari hiyo!

Eti:

“Kuhusu Pinda kunishambulia bungeni jana kauli yangu ni hii. Ninamheshimu sana Pinda na sitaki malumbano nae. Namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia,” alisema Zitto.

Hivi kweli kati ya Pinda na Zitto nani anayeelewa zaidi demokrasia kuzidi mwenziwe?!

Kati yao wote wawili ni nani amesomea demokrasia? Jibu ni hakuna. Si PM wala Zitto aliye hitimu shahada ya demokrasia kwa hiyo akili ya mtu binafsi kutafsiri demokrasia ni nini ina play role kubwa hapa.

CCM haijui kitu kinaitwa demokrasia, wao wanajua serikali ni ya CCM, basi.
 
Hilo lekundu sio kweli. Hayo mengine ni mawazo yako na ninayaheshimu.

hahahaha duh haya sasa BoraMaisha umeona jibu hilo?
Unajua watu iwa hawajui mtu anaposisitiza kitu unatakiwa uongeeaje.
 
WanaJF,
Bwana Pinda amekuwa na kauli nyingi zenye utata, lakini hiyo tu inaonyesha jinsi nchi ilivyo na umasikini wa uongozi. Kwani hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa kuongea irresponsibly, mmewasahau kina Mramba(watanzania watakula majani), Msuya( kila mtu ataubeba mzigo wake), Chenge (vijisenti), Ngasongwa (mikataba kuwa siri ni best practice), hata President (ukitaka kula sharti uliwe) .Mawaziri wanawadharau wabunge hasa wa upinzani- juzi Sumari badala ya kujibu hoja za Slaa anatoa kauli za kuattack.... ''halafu na wewe tafuta hoja nyingine''. Hivi Sumari anasahau Slaa anawakilisha wananchi? Kwa tafsiri nyingine alikuwa anawakaribia wananchi wanotaka haki itendeke- to bring culprits to justice.


Anyway- to summarize, democracy is still under infancy stage (if this is not an exagerration) in Tanzania- ukitaka kujua angalia nchi za Ulaya (good example UK, people are resigning just for failing to account 5GBP!) Hapa mtu anaiibia nchi, anatukana wanachi, prime minister anasimama kumtetea tena katika bunge, na wabunge wa CCM wanashangilia!.

Hata hivyo, Zitto deserves an applause- nafurahi na kupata matumaini kwa kazi yake bungeni- tuzidi kuwahamasishana vijana tugombee nafasi- If you know kijana mwenye uwezo wa kuongoza encorage them to kugombea- tujipenyeze u taratibu one day nchi yetu itaongozwa na wazalendo!
Zitto- big up
icon14.gif
- i like the statement aliyompa PM'.....''namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia,”

jioni njema wana JF- God bless us, God Bless Tanzania and Africa!
Laibon
 
Back
Top Bottom