Zitto akerwa na kauli ya Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto akerwa na kauli ya Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 28, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Muhibu Said

  Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kumtahadharisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kwamba kama anataka kurejea bungeni baada ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani afanye kazi ya ziada, imemchefua mbunge huyo.

  Pinda alitoa kauli hiyo wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa hoja ya hotuba ya bajeti ya ofisi yake katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2009/10, bungeni mjini Dodoma juzi.

  Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema kupitia ujumbe wake mfupi wa maandishi alioutuma kwa Nipashe kutoka Nakuru, nchini Kenya jana kuwa, kitendo kilichofanywa na Pinda, ni cha kumshambulia.

  Hata hivyo, alisema anamheshimu sana Pinda hivyo, hataki kulumbana naye.

  Lakini akamtaka kupima kauli anazozitoa kwa vile zinaweza kuwafanya watu makini wahoji uelewa wake wa demokrasia.

  “Kuhusu Pinda kunishambulia bungeni jana kauli yangu ni hii. Ninamheshimu sana Pinda na sitaki malumbano nae. Namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia,” alisema Zitto.

  Akijibu hoja mbalimbali za wabunge 206 waliochangia moja kwa moja na kwa maandishi, Pinda alisema Zitto alitaka kutumia ujenzi wa barabara za lami alizokwenda kuzizindua hivi karibuni kujipatia umaarufu kuwa kazi hiyo imefanyika kutokana na msukumo wake na wa chama chake cha Chadema.

  Pinda alisema Zitto alitaka kutumia ujenzi wa barabara za lami zilizojengwa mkoani Kigoma kuwa zimetokana na ushawishi wa chama chake wakati si kweli, bali ni mpango wa serikali.

  “Wakati wa uzinduzi, nilikwenda Kigoma, kwa bahati mbaya Zitto hakuwapo, nilipouliza wapiga kura wake kuwa mbunge wenu yuko wapi, wengine walisema amehama, wengine walisema sijui yuko Busanda, ila mimi nasema, kwa hali niliyoiona kule jimboni mwake, 2010 Zitto itabidi ajipange sawa sawa, vinginevyo…,” alisema Pinda na kuibua kicheko kutoka kwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  NIPASHE JUMAPILI
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jun 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,760
  Likes Received: 4,977
  Trophy Points: 280
  ..mipasho-mipasho ya namna hii bora wangeachiwa kina Makamba ,Tambwe Hiza, au Chief Whip wa CCM bungeni.

  ..washauri wa Mzee Pinda mkumbusheni kwamba yeye ni kiongozi wa SERIKALI bungeni, siyo kiongozi wa Chama/CCM bungeni.
   
 3. I

  Ipole JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huo ni ushauri anapaswa kuufanyia kazi na siyo kulaumu nilichokiona mimi Mhe waziri mkuu anampenda na ndiyo maana alimpa ushauri huo Mhe Zito
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hashauriki huyu yaani ni bonge la mzigo, Mimi naamini hakuna waziri mkuu bomu kama huyu Tanzania tuna hasara kwelikweli....halafu waandishi na JF wanampamba sana sijui kwanini?
  a) Aliwahi kuamuru mwezi aachiwe kwasbabu ni CCM leader amekuwa hakimu
  b) Aliwahi kuamuru walioua albino wauawe, aliishia kulia bungeni kulinda mkate wake
  c) Anamtetea hadharani Mkapa (Fisadi) sijui kwanini asikae kimya suburi sheria ifanye kazi
  d) Sijaona alichofanya tangu apewe hiyo kazi statistcally amefungua miradi ya kanisa ya kanisa mara 70 zaidi ya miradi ya serikali ambayo yeye ndio msimamizi mkuu
  Kwa ufupi he is "BOGUS PM, DULL"
   
 5. I

  Ipole JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hujanielewa ambaye hashauriki ni Zito siyo waziri mkuu huyo Zito wenu ameisha sema kuwa anamheshimu Pinda kifaa bwana acha majungu
   
 6. K

  Kieleweke Member

  #6
  Jun 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe, unaweza kutufanya tuamini kwamba Pinda na CCM yake ni watu wa kumshauri Zitto arudi bungeni.

  TUeleze kama una taarifa za Zitto kujiunga na CCM ili arudi bungeni kwa ticket ya CCM kwa jimbo hilohilo.

  Jenga mantiki kabla ya kutumbukia jamvini.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Zitto katoa staha kama kawaida na nadhani hataki malumbano na Mkuu huyu ni wakati sasa wa Mkuu huyu kujua kwamba anaheshimiwa si kwamba ni kifaa hapana ila Zitto ana mheshimu labda kwa kudhania kwamba alikuwa kumbe akawa si kifaa tena .
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hapa Zitto katumia akili kumjibu huyu mzee. Kamjibu indirectly. Pinda lazima aone aibu kamshambulia mtu ambae kaishia kumjibu tu kiustaarabu na kuji kalia kimya.It's embarrasing to Pinda.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi tunaongelea huyu mtu alikuwa anajulikana kama mtoto wa Mkulima wakati sasa anatuumiza wakulima wenzake kwamisafara mizito mikoani ? Ama anasema tu ni mtoto wa Mkulima baba yake na yeye si mkulima ?
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu huko kubandikwa jina "mtoto wa mkulima" unadhani ni kwa sababu gani? Si kwa sababu waziri mkuu aliyetoka Edward Lowassa alikuwa na skendo kibao na kila mtu alikuwa anajua ni tajiri sana. Sasa kumchagua Pinda ili kumtofautisha na EL ndiyo hiyo kupachikwa "mtoto wa mkulima" ili watu waone nae ni mwananchi wa kawaida. Kwa mshahara wa wabunge na mirupurupu mingine unadhani kuna mtoto wa mkulima mule? Yote ilikuwa tu politics ya kumuuza Pinda kwa wananchi.
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lunyungu,

  Waziri mkuu hapingi itifaki ya magari kwenye ziara zake mikoani hivyo suala la mtoto wa mkulima halina nafasi hapo.

  By the way vp hali yako baada ya ajali na je ushafika "Biharamulo?" tunasubiri news live mkuu.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo kubwa ni kwamba wananchi wa Kigoma hawataelewa kitu isipokuwa yale alosema Pinda. Wataendelea kuamini kwamba barabara na maendeleo yoyote ya wilaya au mkoa huo hujengwa na CCM na sii serikali wala kwa nguvu ya uwakilishi wa mbunge..

  Maswala ya kuheshimiana hayahusiani kabisa na Ubunge wa Zitto..Kila mmoja wetu hapa anamheshimu sana Pinda kama Waziri mkuu, kaka yetu na kadhalika, lakini maadam Pinda amevuka daraja na kakianzisha yeye, Zitto ana kila haki ya kumsahihisha maneno ya Pinda hata kama itaonyesha Pinda Waziri Mkuu ana ufinyu wa kuelewa serikali ya demokrasia inafanya kazi vipi..
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sisi tulisema kuwa Kauli za Pinda sasa hivi hazielewiki kabisa
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pinda,
  Mfipa wee umejiingiza mwenyewe kwenye MOTO. Mie nilikuwa ni mtu niliyepingana sana na Mwanakijiji ili kukutetea kwa kauli yako ya kuuwa wale wanaouwa Albino. Nilifikiri umeteleza kumbe ni kawaida yako. Kweli hebu fikiria CHOZI ulilolitoa bungeni. NExt time (na nafikiri itatokea hivi karibuni) utaropoka na huyo Zitto ndiyo atakukalia sasa kooni. Walau ungelituma wabunge wako waseme hivyo, ila wewe PM unakwenda low namna hiyo? Sasa ukija teleza usitegemee CHOZI lako litakusaidia.
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kwa kuongezea jamani huyu mzee pinda nahisi kwamba huwa hafikirii vizuri kabla ya kutamka maneno. Au sijuwi kuna haja ya kumkumbusha kwamba yeye ni waziri mkuu huo ukada anapaswa kuuweka pembeni kwanza.

  Hivi hiyo sheria yake aliisomea wapi Dar? Juzi kanichanganya kabisa kwa kweli kwa msisitizo kabisa anasema mkapa ni msafi lakini serikali itafanya uchunguzi. Sasa mzee Pinda kama umesema Mkapa ni msafi kuna haja gani ya kufanya uchunguzi? Huoni kama unaathiri uchunguzi wooote kwa kusema mkapa ni msafi? Nani unahisi atakupinga wewe? Hiyo pesa ya uchunguzi si ni heri ikanunulie madawati watoto wa darasa la 7 Mbagala wasiendelee kukaa chini wakati wa mitihani?

  La pili, unasema Mkapa hakununua Kiwira kwa kuwa Kiwira imeshindwa kulipa hata mishahara. Kwani umeambiwa na nani kwamba sisi tunahoji uwezo wa kifedha wa Kiwira? Issue hapa Mkapa alikwenda kinyume kwa kujiuzia mradi wa thamani ya 4 billion kwa sh milioni 700 huku akiwa still ni rais. Whether hiyo kampuni yake ina uwezo wa kulipa mishahara au lah si issue kwetu mzee.
   
 16. B

  Bobby JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Masatu hata Sokoine na Nyerere walikuwa hawapangi itifaki lakini the good thing about them walikuwa wakikemea pale wanapoona kuna kufuru kama ya mtoto wa mkulima juzi Iringa. So Pinda anayo nafasi ya kusema no next time jamani sihitaji magari 80 kwenda kufungua ujenzi wa barabara. Bahati mbaya hatujaiona hiyo nia tuliyoitarajia kwa mtoto wa mkulima.
   
 17. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Miye nadhani huyu Zitto anapewa umaarufu ambao hata haumstahili. Zitto amepewa kichwa tu kutokana na kuwa msemaji kwa jazba ndani ya Bunge etc lakini hana upeo wowote mkubwa kisiasa kuweza kumjibu Waziri Mkuu kama ilivyoelezwa na mwandishi wa habari hiyo!

  Eti:

  “Kuhusu Pinda kunishambulia bungeni jana kauli yangu ni hii. Ninamheshimu sana Pinda na sitaki malumbano nae. Namshauri atazame kauli zake maana zinapelekea watu makini waanze kuhoji uelewa wake wa demokrasia,” alisema Zitto.

  Hivi kweli kati ya Pinda na Zitto nani anayeelewa zaidi demokrasia kuzidi mwenziwe?!
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bobby umenena kwamba Sokoine na Nyerere walikuwa wakikemea pale walipoona kuna kufuru ......... Kwa maana nyingine, umemtaja Waziri Mkuu pamoja na Rais wake kwamba walikuwa wakikemea.

  Tutakuwa tunamuonea Pinda kumtaka azuie msafara wa magari wakati Mkubwa wake amekaa kimya hazuii misafara yake wala kupunguza misafara ya kwenda nje. Mie nadhani utashi sharti uanzie kwa Rais mwenyewe na Waziri Mkuu anakuwa anafuata nyayo ama anajua kwamba analofanya lina baraka ya Mkuu wake. Msitake kumponza Pinda hata kama angalikuwa na roho ya mtoto wa mkulima na kutaka kutenda vitendo vinavyolingana na mtoto wa mkulima hatothubutu kufanya hivyo kama anahofu asije akamkanyaga vidole Mkubwa wake ama akaonekana kum-outshine!
   
 19. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi mlitegemea nini? Mkapa alikuwa Rais wa Serikali ya CCM na Pinda ni Waziri Mkuu wa Serikali ya CCM. Kwa maana nyingine ni kwamba akitiwa hatiani Rais Mkapa ni sawa na CCM kutiwa hatiani.

  Anachofanya Pinda ni kuendeleza juhudi za kuhakikisha kwamba CCM inalindwa hata kama ni kwa kucheza foul! Jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa na CCM yenyewe.
   
 20. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #20
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hilo lekundu sio kweli. Hayo mengine ni mawazo yako na ninayaheshimu.
   
Loading...