Zitto akataa posho ya mil. 238

Zitto akataa posho ya mil. 238

acha chuki binafsi mkuu iyo posho una ushahidi anachukua, mbona rahisi kujua anazo stahli ni zile za mwanzo alipojiuzuru ubunge hizi 230 zinazotaka kusainiwa ndo atapeleka aliposema. HUYU NDO MZALENDO WA KWELI.

ngapi mkuu anazostahili?
 
Which line is he in?
1. Zitto atapokea posho hiyo, or
2. Zitto atakataa posho hiyo
Hiyo Habari ya kwamba atatumia vipi is not a current up front business!

Kama amepanga kuipeleka huko anakokujua ni wazi kua ataipokea tu. Maana ataipeleka vipi huko bila kuipokea kwanza?

So line #1 ndo sahihi
 
Hivi Mbunge aliyefukuzwa ubunge anasitahili kupata kiinua mgongo cha ubunge in the first place?

Maana huenda hata hicho kidogo anachodai huenda hasitahili, anasitahili kupata ZERO SHILINGI.

I reckon Mpendazoe alipoacha ubunge 2010, hakupewa kiinua mgongo. Inakuwaje Zitto yeye apewe. Kama ni suala la sheria na principle Zitto anatakiwa kukataa hata kidogo hicho atakachochukua.

Kwani Zitto anafahamu fika kwamba ma-CCM YAMEPINDISHA SHERIA kumpatia kiinua mgongo wakati hasitahili kwa mujibu wa sheria.

liked mkuu
 
Hivi kuna mbunge mwingine aliyelaani malipo haya hadharani zaidi yake? wabunge wote (CCM & CDM) wapo kimya katika hili, wote wanaona sawa walipwe tuu...
 
haa haa zitto anawachanganya sana wafuasi wake. hapa kasema atachukua.je zitto alipaswa kuchukua? mbona alijiuzulu ubunge? zitto ataendelea kudanganya misukule yake mpaka lini? zitto ni laghai tu hana jipya.

Ccm wanaposhindwa na hoja wanamuandaa Lusinde ili atoe matusi. Watu wa jamii ya ccm why mnapenda lugha chafu?
 
Hivi kuna mbunge mwingine aliyelaani malipo haya hadharani zaidi yake? wabunge wote (CCM & CDM) wapo kimya katika hili, wote wanaona sawa walipwe tuu...
Hakuna, wote kimya. Wamebaki kudanya watu.
 
ZTO hajakataa kuchukua hela ila kwa wenye mahaba na zto ndo wanajitoa ufahamu mbna hapo panajieleza vizuri tu? jamani!
 
Huyu Yuda Iskariote kumbe anachukua mafao? Huyu si alijiuzulu Ubunge? Anachukua mafao kama nani?

Huu ni ufisadi mkubwa kama ule wa akina Chenge.

mkuu nitashangaa sana kama bunge litamlipa zitto mafao hayo..
 
Hivi kuna mbunge mwingine aliyelaani malipo haya hadharani zaidi yake? wabunge wote (CCM & CDM) wapo kimya katika hili, wote wanaona sawa walipwe tuu...

haa haa hivi zitto amelaani lini malipo hayo?mbona amekiri kuwa atapokea?
 
Ccm wanaposhindwa na hoja wanamuandaa Lusinde ili atoe matusi. Watu wa jamii ya ccm why mnapenda lugha chafu?

mkuu hapo lugha chafu ni zipi? mkuu zitto kakiri kupokea pesa hiyo muda ukifika wakati hakustahili. hakuna namna nyingine zaidi ya kusema ni usanii.
 
Kweli nimeamino zito ni akili kubwa,
Hongera zito zuberi kabwe.
 
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Haki yako zzk ni rushwa ya nssf?
 
Ingawaje cmdis jepesi ila nna wasiwasi na uwazi kwenye hili la kiasi cha ziada mbona hajasema ni sh.ngapi(nawaza kimoyomoyo!!!!!!!!!!)
 
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Kiongozi Zitto na wabunge wengine wote wenye nia ya dhati na taifa hili kuna usemi usamao hivi:- Huwezi chukua fedha za unga (haramu) ukaijengea msikiti. Fedha haramu haiwezi kutakaswa..

Nakushauri na nawashauri wote wenye Uzalendo wa kweli wasichukue fedha hizo kama wanaona ni DHULMA na sii kuweka sababu za kuchukua ili kujenga hoja ya nguvu kwani fedha hizo zitahesabika kama mchango wako ilihali sii fedha zako bali imetokana na dhulma! Ni ushauri wangu tu....

Ramadhan Kareem.
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Najua huo ni wivu tu!hujawahi kuikamata hata mil5 ya pa1 ndoma ya zitto yanakukera
mkuu kiukweli zitto kakiri atapokea malipo hayo haramu. nimeamini wanasiasa wakiaminiwa hawaaminiki. ule uzalendo anaohubiri ni maigizo tupu.
 
Back
Top Bottom