Zitto akataa posho ya mil. 238

Zitto akataa posho ya mil. 238

Huko kwenye vyama vyenu, Nani mwenye uwezo wa kujitolea na kufanya Kama zzk.

Mbowe alisema gari la serekali silitaki na bado analitumia Hadi kubebea magendo kenya, lakini yeye kufanya hivyo ni sawa
 
Leta ushahid hapa unaoonyesha kafukuzwa na chagadema
Hivi wewe unaongea nini,hivi Una akili timamamu kweli?
chama kikisema noo to mbunge au diwani,that's final,wahusika huwa wanakimbilia mahakamani ,that's why wana kuwa wabunge wa mahakama.
sasa wewe process IPI unayo iongelea hapa, kijana usizanie wote ni mbumbumbu Kama wewe.
alafu chunga maneno yako,kwa uandishi huu,ingekuwa jf ya zamani ungelamba ban ya week.
 
Nimemuelewa Zito kuwa kusingekuwa na ".....fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa Sheria ...."
asingetoa hiyo misaada.
 
haa haa zitto anawachanganya sana wafuasi wake. hapa kasema atachukua.je zitto alipaswa kuchukua? mbona alijiuzulu ubunge? zitto ataendelea kudanganya misukule yake mpaka lini? zitto ni laghai tu hana jipya.
 
Nimemuelewa Zito kuwa kusingekuwa na ".....fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa Sheria ...."
asingetoa hiyo misaada.

kwa maoni yangu zitto hapaswi kuchukua hata senti tano kwa malipo ya wabunge. mbona alishajiuzulu ubunge? anachukua kwa msingi gani? huu ni ufisadi kama ufisadi mwingine
 
Which line is he in?
1. Zitto atapokea posho hiyo, or
2. Zitto atakataa posho hiyo
Hiyo Habari ya kwamba atatumia vipi is not a current up front business!
 
Kama kawaida huyu kijana ni mtu wa kutenda si maneno! Haya sasa wabunge wa UKAWA mufuate nyayo otherwise nyie ni wachumia tumbo tu kama wale wa CCM.

mkuu lipi hapo la kumuiga zitto? labda unafiki tu.wa kuchukua mafao yasiostahili hata kidogo...
 
Which line is he in?
1. Zitto atapokea posho hiyo, or
2. Zitto atakataa posho hiyo
Hiyo Habari ya kwamba atatumia vipi is not a current up front business!

mkuu kiukweli zitto kakiri atapokea malipo hayo haramu. nimeamini wanasiasa wakiaminiwa hawaaminiki. ule uzalendo anaohubiri ni maigizo tupu.
 
Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?

haa haa hilo nalo neno mkuu..n
 
Kwa upande wa Upinzani hakuna hata mtu mmoja anayeweza kufikia hata robo ya akili ya Zitto. well done zitto.

Kuna zaidi ya taaluma 2600 duniani, ZZK ana akili ya kitu gani, ameinvent kitu gani hapa nchini au ni uzuzu wetu unaotusumbua sisi wapambe! Binafsi sio hiyo akili ya ZZK inayotajwa kila mara kuwazidi wanasiasa wenzake, ni wa kawaida bali mkakati wa kumpamba tu hata hivyo mpango unaelekea kufail.
 
taratibu mkuu zitto hakufukuzwa, zitto alijiuzuru hivyo malipo ni halali yake. kama nahisi alifukuzwa leta ushahidi

kumbe ukijiuzulu ni halaliyako kulipwa? tuwekee sheria inayoruhusu hilo hapa mkuu.
 
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.


Zitto ni kiongozi tofauti sana. Anaendana sana mapendekezo ya katiba ya Warioba. Big up! Tupo pamoja nawe.
 
Kumbuka hakustahili kupata hata senti moja huyo bwana baada ya kujitoa chadema na kuaga bungeni . hana haki ya senti tano acheni kuchezeshwa nahuyu bwana muongo . Ni rahisi kuwadanganya wabunge si wananchi huku uraiani.Mpendazoe alipewa sh ngapi? mbona yeye kwakuwa pro-CCM wamemuahidi kumpa wakati hayupo bungeni? Ndio maana CCM wanatuchezea watanzania hatuko critical ni kushangilia na kucheza ngoma basi. Zitto anakuambia tusiamini wanasiasa anajijua. Kama kuna vijana hawawajui wanasiasa jifunzen kwa mrema

shukrani mkuu wangu...
 
Huyu Yuda Iskariote kumbe anachukua mafao? Huyu si alijiuzulu Ubunge? Anachukua mafao kama nani?

Huu ni ufisadi mkubwa kama ule wa akina Chenge.
 
Huyu tumeshamzoea mnafki na mzungumzaji kwa kile asichokitenda....wenye majina ya wafilisi nchi walitaja hadharan yeye kaweka kwapan majini ya uswisi...
Ni mtu ambaye analikana jambo sasa hivi baada ya dakika tatu analikubali...namfaninisha na ndezi yule mnyama ambaye akikoswakoswa risas hapa anakimbia baada ya sekunde mbili anarudi tena...
 
Back
Top Bottom