Zitto akataa posho ya mil. 238

Zitto akataa posho ya mil. 238

Mbona hakukataa zile 3bln za wenye migodi ya madini kule kanda ya ziwa?
 
alizohongwa na ccm ni zaidi ya 238 mara 4 kwa hiyo asiwa danganye watu hyo yuda nyepesi ayatwallah aka supreme leader
 
By Zitto,

Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Msaliti, msalitii ,msaliti,msaliti,msaliti,yuda,yuda,yuda
 
Maana yake atazichukua. Kutoa ocean rd etc mbona hata wengine nao watachangia hivyo hivyo? Sanaaa
 
Huko kwenye vyama vyenu, Nani mwenye uwezo wa kujitolea na kufanya Kama zzk.

Mbowe alisema gari la serekali silitaki na bado analitumia Hadi kubebea magendo kenya, lakini yeye kufanya hivyo ni sawa

anabebea hadi pesa za escrow
 
Akili ya kuambiwa changanya na zako. Amesema ziada ya ile anayostahili ndo ataipeleka Ocean Road. Ina maana kama hiyo 230mil kisheria ni halali yake basi ataichukua, ila kama wakijichanganya wakamuwekea excess (sitegemei itokee) ndo itaenda ocean road.
 
Wangefanya hivyo hivyo wabunge wote tungepiga hatua.
......... viva Zitto zuberi kabwe.
 
Last edited by a moderator:
zito anamtazamo wa hali ya juu tena mtazamo wenyewe kwa maslai ya wananchi safi sana zito
 
kwani act wana shida ya pesa? Tafakari chukua hatua
act inauza kadi, tshirt na michango ya kila mwezi ya wanachama,

hakuna anayetegemea hizo posho za chadomooooooooo
 
Zito ndio mwanasiasa pekee anayetenda anachokiongea,wengine wote hasa yule mwenye makengeza kwake ni pesa mbele maslahi ya wananchi baadaye
 
Wangefanya hivyo hivyo wabunge wote tungepiga hatua.
......... viva Zitto zuberi kabwe.

kipi cha ajabu hapo?

Mbona mbowe ametoa vitu kibao jimboni kwake mfano Ambulance na magari ya taka....si ni fedha za kwake zile?

Baadhi ya Watanzania ni bendera fuata upepo
 
kadi wanauzaje? wameuza ngapi? t shirt je? kama kwa muda mfupi wameuza kadi na tshirts kiasi kwamba wametosheka hawahitaji sh 230m, basi kadi na tshirt zao zitakuwa very expensive, may be kadi na tshirt ni sh milioni moja kwa makadirio. congrats lakn
 
ni unafiki kukataa posho kwa mkono mmoja na kupokea kwa mkono mwingine ,huyu anatumia NGO yake kupokea posho na rushwa kwa mgongo wa ufadhili kumbe anatumia katika chama chake cha act
 
Mpendazoe HAJALIPWA mafao yake hadi leo!Dr Ndembela Ngungangwa hadi anafariki hakulipwa mafao yake!

Zitto analipwa mafao yake yote daaah
 
Atuonyeshe na stakabadhi ya matumizi ya hiyo pesa. Halafu kitu kingine kibaya ni kuachia pesa CCM waitafune ni kheri kuchukua hiyo pesa na kwenda kusaidia shughuli za maendeleo au kwenda kujenga chama kwa wananchi. Kitendo cha UKAWA kususia bunge la Katiba ilipelekea CCM kufanya kufuru ya matumizi kwa pesa yote ambayo UKAWA ilibidi waipate kwa kuhudhuria vikao
 
Mbona hakukataa zile 3bln za wenye migodi ya madini kule kanda ya ziwa?

alizohongwa na ccm ni zaidi ya 238 mara 4 kwa hiyo asiwa danganye watu hyo yuda nyepesi ayatwallah aka supreme leader

Msaliti, msalitii ,msaliti,msaliti,msaliti,yuda,yuda,yuda

Maana yake atazichukua. Kutoa ocean rd etc mbona hata wengine nao watachangia hivyo hivyo? Sanaaa

Ukimfata zitto utapotea

ni unafiki kukataa posho kwa mkono mmoja na kupokea kwa mkono mwingine ,huyu anatumia NGO yake kupokea posho na rushwa kwa mgongo wa ufadhili kumbe anatumia katika chama chake cha act

Mpendazoe HAJALIPWA mafao yake hadi leo!Dr Ndembela Ngungangwa hadi anafariki hakulipwa mafao yake!

Zitto analipwa mafao yake yote daaah
Husuda chuki binafsi choyo na uvivu wa kufikiri ndio tatizo lenu
 
Zito ndio mwanasiasa pekee anayetenda anachokiongea,wengine wote hasa yule mwenye makengeza kwake ni pesa mbele maslahi ya wananchi baadaye

Muulize HUYO ZZK katumia pesa ngapi za Mbowe alipokuwa pale UDSM na kugombea ubunge Kigoma kaskazini na katumia vifaa vingapi vya chadema kama helcopter na vinginevyo. Halafu google upate taarifa za Mbowe kafanya nini HAI bila kufilisi shirika lolote la UMMA kama nalivyofanya yeye kuishinikiza NNSF kuingia mkataba na kampuni yake
 
Back
Top Bottom