Posho hizo ni kwa mujibu wa sheria so atapokea maana ni mafao kwa mujibu wa sheria ......awadanganye wajinga , zile za posho alisema hatapokea mara atapelekea kwenye NGO yake huko Kigoma , muulizeni ziko wapi ? NGO yake ilipokea ngapi? Mnafiki sana huyu ....
acha chuki binafsi mkuu iyo posho una ushahidi anachukua, mbona rahisi kujua anazo stahli ni zile za mwanzo alipojiuzuru ubunge hizi 230 zinazotaka kusainiwa ndo atapeleka aliposema. HUYU NDO MZALENDO WA KWELI.Zitto, anasema atachukua zile anazostahili kwa mujibu wa sheria , sasa yeye ambazo hastahili ni ngapi? Vipi kuhusu posho ya kukaa ambayoalisema aliacha kuchukua , mbona aliendelea kuchukua ?
By Zitto,
Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.
Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.
Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.
Source: His facebook page.
Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.
Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?
Huo ndo unafiki. Zipi ni halali na zipi ni haramu?Nadhani ni zile alizotakiwa kulipwa katika utumishi wake bungeni kwa miaka yote 10 zile za nyongezo ni haramu!
Kwa nini walipwe mahela mengi namna hiyo?
Kwa nini hayo mahela yasitumiwe kwenye mambo mengine yaliyo muhimu zaidi kuliko matumbo ya hao wabunge?
Nakubaliana na weweHivi Mbunge aliyefukuzwa ubunge anasitahili kupata kiinua mgongo cha ubunge in the first place?
Maana huenda hata hicho kidogo anachodai huenda hasitahili, anasitahili kupata ZERO SHILINGI.
I reckon Mpendazoe alipoacha ubunge 2010, hakupewa kiinua mgongo. Inakuwaje Zitto yeye apewe. Kama ni suala la sheria na principle Zitto anatakiwa kukataa hata kidogo hicho atakachopewa.
Kwani Zitto anafahamu fika kwamba ma-CMM YAMEPINDISHA SHERIA kumpatia kiinua mgongo wakati hasitahili kwa mujibu wa sheria.
jamani hamjamuekewa zzt,kasema fedha zoto za ziada.
sasa kwenye hiyo amount ya 238 atuambie za ziada ni ngapi?
Au hizo 238 zote ni za ziada ??
zitto you can fool some people some time but you can't fool all the all the times.
kawadanganye mwandiga na lwiche sio humu.
By Zitto,
Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.
Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.
Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.
Source: His facebook page.
Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.
Akiwa anatoa msaada atasema zimetoka wapi?Lazima atajibu kwenye mafao yangu au?Anatafuta sifa kwa fedha anazoziita haramu.
Wengine tumechoka kudanganywa.Alisema mwenyewe msituamini wanasiasa,ni kweli waongo kwa asilimia 100.
Sasa si kasema ziada hachukui au ulitaka hata haki yake agomee??!!!Posho hizo ni kwa mujibu wa sheria so atapokea maana ni mafao kwa mujibu wa sheria ......awadanganye wajinga , zile za posho alisema hatapokea mara atapelekea kwenye NGO yake huko Kigoma , muulizeni ziko wapi ? NGO yake ilipokea ngapi? Mnafiki sana huyu ....