Zitto akataa posho ya mil. 238

Zitto akataa posho ya mil. 238

But my understanding is ZZK is no longer an MP, anapeweje pension
 
by zitto,

juzi nilipokuwa jijini mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi shule ya buhangija na hospitali ya saratani ya ocean road. Buhangija nilitembelea mwezi aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na miss. Tanzania briggite alfred ambaye anajenga bweni pale. Ocean road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu hajjat shida salum.

Source: His facebook page.

Huyu zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.


hapo mbona hajakataa kaichukua kwenda kujenga hilo bweni.
 
Posho hizo ni kwa mujibu wa sheria so atapokea maana ni mafao kwa mujibu wa sheria awadanganye wajinga, zile za posho alisema hatapokea mara atapelekea kwenye NGO yake huko Kigoma, muulizeni ziko wapi? NGO yake ilipokea ngapi? Mnafiki sana huyu
Kama ungesoma vizuri post yake (ZZK) ungegundua kuwa hakusema kuwa atakataa. Alisema ataitumia katika kusaidi wahitaji kama vile kuchangia ujenzi wa mabweni katika hospitali ya ocean road! Matusi/maneno ya kashfa na kejeli hayakujengi mwana JF; badala yake yanakufanya uonekane kuwa u-mvivu wa kufikiri. Badilika!
 
Lowasa analipwa isivyo halali na huo nao ni ufisadi.Kwani alistaafu lini
kumbe ndo maana tunapishana mkuu, wewe unajua analipwa kiharamu sawa, ila jua alistaafu kwa kujiuzuru
 
Zito alifukuzwa kwa mujibu Wa katiba ya CDM
ingekuwa mnafata katiba mpaka sasa hadi mbowe ashfukuzwa kwa mujibu wa katiba maana kaivunja na kujiongezea mda. ko barua ya ZZK aliandikiwa lini na nani
 
But my understanding is ZZK is no longer an MP, anapeweje pension
kwani penshani anapewa nani, je huyu mbunge wa mwanza aliefariki (r.i.p) is no longer MP ko familia yake haistahili pensheni hahahahhaha
 
zito kama kawaida take alikata posho za kila siku,huyo ndo mtazania wa Kweli engine wachumia tumbo!
 
Kwa hiyo kama mtu hana ziada anakuwa hana kitu kabisa!!!???
Amesema malipo ya ziada hatachukua...atachukua stahili yake...na hapo hapo akasema ziada atapeleka Ocean Road na huko Kigoma kujenga bweni. Siyo habari ya kusema hana ziada...amesema ziada ataitoa msaada, na wakati huo huo akiwa amesema hataichukua. Soma uelewe.
 
Zitto, anasema atachukua zile anazostahili kwa mujibu wa sheria , sasa yeye ambazo hastahili ni ngapi? Vipi kuhusu posho ya kukaa ambayoalisema aliacha kuchukua , mbona aliendelea kuchukua ?

Usijionyeshe jinsi usivyojua mambo.

Zitto aliiacha kuchukua posho za makalio toka mwaka 2011.

Usiongee bitu usivyovijua,ni kujionyesha utupu.
 
Matusi/maneno ya kashfa na kejeli hayakujengi mwana JF; badala yake yanakufanya uonekane kuwa u-mvivu wa kufikiri. Badilika!

Ni kweli kabisa, JF sasa wanataka waifanye kama kijiwe cha kahawa ambako machizi wanabishana tu.Mtu ata ajiulizi wala hafikirii.
 
11009204_870091173083905_1311677072794020071_n.jpg
 
Amesema malipo ya ziada hatachukua...atachukua stahili yake...na hapo hapo akasema ziada atapeleka Ocean Road na huko Kigoma kujenga bweni. Siyo habari ya kusema hana ziada...amesema ziada ataitoa msaada, na wakati huo huo akiwa amesema hataichukua. Soma uelewe.

Ziada inatokana na matumizi yake sio uelewa wako au wangu anaweza pewa shilingi mia tu akatumia sabini thelathini ikabaki na hiyo akaiita ziada akatoka huko alikotaja . . . .. .ziada ya mtu anaijua mwenyewe. . . .
 
Muulize HUYO ZZK katumia pesa ngapi za Mbowe alipokuwa pale UDSM na kugombea ubunge Kigoma kaskazini na katumia vifaa vingapi vya chadema kama helcopter na vinginevyo. Halafu google upate taarifa za Mbowe kafanya nini HAI bila kufilisi shirika lolote la UMMA kama nalivyofanya yeye kuishinikiza NNSF kuingia mkataba na kampuni yake

Wew kilaza kweli tu Google ili iweje , wew unaishi hai .. au unashinda tu huku kwenye keyboard , hizo ambulance na gari ya taka ya lala salama ndio unaona amaefanya kitu , aisee wew subiri October ndio utajua mbowe kafanya nin
 
By Zitto,

.............
Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.
......................
Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.


Alichokisema Zitto kinaingia akilini maana hizo pesa hata kama hatazichukuwa ofisi ya bunge haitazirudisha hazina.

Tatizo ni wewe muleta habari. Wewe umeshindwa kuonyesha busara kwa kuandika madudu. Kuiga siyo jambo la aibu na hata siyo kupenda sifa. Zitto siyo muanzilishi wa misaada hapa Duniani. Ngereja alipata mgawo wa wizi wa escrow na kwa aibu amelazimika kuzitoa misaada ili aonekane mtu wa niya njema angalau kwa mwaka huu tu!

Ktk historia wezi wote wa dunia ya ulaya, walikuwa wakitoa indulgence (induljensia) ili kuwa kama kujisafisha makosa. Sasa wewe kwa nini usifie mtu kwa kuwadhalilisha wengine?
 
Ziada inatokana na matumizi yake sio uelewa wako au wangu anaweza pewa shilingi mia tu akatumia sabini thelathini ikabaki na hiyo akaiita ziada akatoka huko alikotaja . . . .. .ziada ya mtu anaijua mwenyewe. . . .

Soma uelewe, acha kujitoa ufahamu Zitto hazungumzii ziada ya matumizi yake. Anazungumzia ziada kwenye mafao. Amesema ziada ya kile anachostahili, siyo ziada ya matumizi yake. Fuatilia suala hili kwa kumaanisha utaelewa. Kabla ya kufanya hivyo, usinijibu. Kama ungekuwa unafuatilia masuala haya japo kwa kusikia tu mtaani, usingeshindwa kulielewa hili. napoteza muda kujadiliana na mtu aliyeamua kujifanya kipofu huku macho anayo.
 
"Fedha yote ya
ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka
kusaidia......" ZZK ss itakuwaj apokee hela nje ya sheria? Na imeshapitishwa kwamba wapewe hyo posho ina maanisha ni kwa sheria, ss hilo fungu la msaada ambalo c kwa mujib wa sheria atalitoa wapi? Ikumbukwe mvunja sheria ni mwalifu
 
Aseme anazostahili kwa mujibu wa sheria ni ngapi? Mbona yeye analipwa wakati alifukuzwa kwenye chama chake na kuukosa Ubunge ? Mbona mpaka leo akina Danny Makanga na Erasto Tumbo , tangu walipofukuzwa UDP hawajawahi kulipwa mafao yao ? yeye analipwakwa utaratibu upi?

Amesema hivyo kwa kuwa anajua hatolaipwa.
 
Soma uelewe, acha kujitoa ufahamu Zitto hazungumzii ziada ya matumizi yake. Anazungumzia ziada kwenye mafao. Amesema ziada ya kile anachostahili, siyo ziada ya matumizi yake. Fuatilia suala hili kwa kumaanisha utaelewa. Kabla ya kufanya hivyo, usinijibu. Kama ungekuwa unafuatilia masuala haya japo kwa kusikia tu mtaani, usingeshindwa kulielewa hili. napoteza muda kujadiliana na mtu aliyeamua kujifanya kipofu huku macho anayo.


"Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili" sio "fedha yote zaidi ya ninachostahili". . . . . . kumaanisha ndio kufanyaje na umapimaje huko kumaanisha!!!???? Kumbe we unasikia mtaani tu ndio unaelewa. . . . ..kama unapoteza muda then huna busara kabisa . . . .. . . .tumia muda wako vizuri
 
Back
Top Bottom