Zitto akaribishwa NCCR-Mageuzi Urais 2015

Zitto akaribishwa NCCR-Mageuzi Urais 2015

Safi sana Kisandu!Nimeona leo mtaani jinsi watanzania walivyopekea kauli yako positively. Wanadai kule Zitto aliko kila akitaka kugombea chochote anapigwa nyundo ya kichwa. Kama NCCR inampokea na kumpeleka kwa wapigakura waamue, hiyo ndio demokrasia halisi. Mhe. Zitto, njoo NCCR upate haki yako ya kugombea. Hata mimi Kura yangu unayo.
 
Kisandu ananipa mashaka juu utimilifu wa fikra zake,maana akiwa angali CDM huko Tanga aliwahi kusema atajitoa CDM na kisha atagombea urais kupitia chama chochote,kweli chama amepata hicho chochote na ameangukia NCCR,leo anaibuka na hoja ya kumuomba ZZK aende NCCR akatimize ndoto yake ya kugombea urais.hapa ndipo napata mashaka na uelewa wa Kisandu,nadhani kama lengo lake ni kuvuruga watanzania kwa kuisaidia CCM kupitia divide and Rule ili hali watu wagawike basi anajidanganya na wapambe wake.nawashauri wote wanaodhani CDM hakuna demokrasia wakamuunge mkono Kisandu au mkakijenge CHAUMA kisha tupambane kwenye field war ya kisiasa.sio kupiga domo tu

1:Sababu kubwa iliyomuondoa CHADEMA kwa madai yake ni kwamba vijana wanaotoka CCM na vyama vingine wanatumika kwenye M4C kuliko vijana walioko ndani ya CHADEMA.Sasa yeye alipohamia NCCR-Mageuzi ndani ya Masaa 72 tu alipewa cheo cha kitaifa tena aliundiwa cheo ambacho hakikuwepo.Je hoja yake iko wapi?Je,NCCR-Mageuzi kulikua hakuna vijana wenye uwezo zaidi?Unafiki huu

2:Alisema amejengewa Bifu kwa kutangaza kugombea Urais na kwamba atagombea urais akiwa chama chochote.Masaa 144 baada ya kujiunga NCCR-Mageuzi ametangaza kumtaka mgombea Mwingine wa urais.Misimao yake iko wapi?

Haya ndiyo matatizo ya watu kuingia katika siasa bila kujua wanasiammia nini na kukosa dira.Kazi ya kudhoofisha CHADEMA inaendelea kuwawia vigumu na in the process ni lazima watu waaibike.

Itikadi ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA ni tofauti kabisa,sasa kijana aliyepewa kazi ya Uenezi anaporopoka hivi bila kuzingatia itikadi ni kuidhalilisha demokrasia na kuwa kituko katika siasa
 
Chama cha NCCR-Mageuzi kimefungua milango kwa mbunge wa kigoma kaskazini (Chadema) Mh Zitto, kujiunga na chama hicho ili kutimiza ndoto yake ya kugombea urais mwaka 2015. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na katibu wa mahusiano na uenezi wa kitengo cha vijana wa NCCR-Mageuzi, Deugratius Kisandu.Source Mtanzania jpili.
wasiliana na Zito,atuambie yeye nwenyewe,sisi wana chadema tunamfahamu Zito,yeye sio mtu wa kusemewa wala sio wa polepole,hayo ni maneno yako ya kimagamba.sisi hatutokuamini huo ni uzushi na mtazusha sana,mmeanza kwa Slaa,mkajaribu kwa Lissu,sasa mmeamia kwa Zito,mkitoka hapo mtaenda kwa Mboe.lakini ampati kitu,sisi kazi yetu ni moja kuiondoa ccm madarakani tu,
 
Why don't you give Zitto Kabwe a break so that he can reconcile himself with his fellow party leaders and members to strengthen CHADEMA, the biggest opposition party in the country and potentially the source of the next government in waiting ? Je ZZK ana kiu kikali cha kugombea uraisi kiasi hicho! Inasaidia nini kugombea uraisi katika chama dhaifu kisicho na effect yoyote katika mstakabali wa Taifa ? Kwa nyadhifa na majukumu aliyo nayo kitaifa, kichama, bungeni, jimboni kwake na kwingineko, inamsaidia nini ZZK leo hii kugombea uraisi for the sake of it ? Nimeanza kufikiria kuwa vyombo vya habari vinamtumia ZZK kujinadi kibiashara. Lakini vikijua au bila kujua, vyombo hivi na waandishi vinamuathiri sana ZZK kwa kumchonganisha na viongozi na wanachama wenzake. Hili siyo jambo zuri kwa CHADEMA na upinzani kwa ujumla.

Nakuunga mkono kiongozi ujue tanzania kunasiasa uchwara nyingi nadhani hata huyu anayemkaribisha zitto NCCR si alikuwa CDM na nadhani lengo lake ilikuwa luivuruga CDM sasa japo ametoka bado anaendelea na kazi yake ya kuivuruga CDM. Swala la zitto au slaa kugombea uraisi nadhani hilo halina mjadala ukiwasikiliza viongozi wa CDM kwa makini hakuna aliyesema fulani ndiye atakayegombea na fulani haruusiwi nadhani kutakuwa na utaratibu maalumu wa kumpata atakaye peperusha bendera ya CDM ambapo wanachama wa CDM ndio watakaohamua kwa njia ya kura. Pia hata kama zitto hatogombea 2015 bado CDM inaweza kumsimamisha 2020 na hilo si tatizo kwa kuwa kijana atakuwa ameiva vya kutosha katika siasa za tanzania na nadhani CDM si kama vyama vingine masalani CUF ambapo tangu vyama vingi vianze 1995 Lipumba peke ndiye amekuwa akigombea
 
Huyo hafai kuwa kiongozi wa tawi achilia mbali urais hana nidhamu kwa wakubwa, ana uchu wa madaraka, hana subira, anafikiri ana akili kuliko mtu yoyote, nk. Huyo hafai kwa sasa na akijaribu atakuwa amejimaliza. Hapo alipofika ni pazuri, angetulia asome hekima za uongozi vizuri, apate support na baraka za wazee ipite kama miaka kumi ndio aanzishe move hiyo angefanikiwa lakini sio leo
 
Jamani huyu mtu naöna ni mwehu ,hivi si huyu huyu kisandu alikuwa anautaka urais na ndo kilichomwöndoa Chadema kwamba hapewi fursa ya kugombea urais? Fursa si hiyo ameshapata agombee huko NCCR halina lolote hilo njaa tu inamsumbua atakufa huyo tamaa mbaya
 
Safi sana Kisandu!Nimeona leo mtaani jinsi watanzania walivyopekea kauli yako positively. Wanadai kule Zitto aliko kila akitaka kugombea chochote anapigwa nyundo ya kichwa. Kama NCCR inampokea na kumpeleka kwa wapigakura waamue, hiyo ndio demokrasia halisi. Mhe. Zitto, njoo NCCR upate haki yako ya kugombea. Hata mimi Kura yangu unayo.
zito sio mtu wa kusemewa kama unavyofikiri,mawazo yako bado ni ya umagamba,kama anaweza kuwasema magamba ambao wao wana kila kitu,polisi,usalama wa taifa,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa, mawaziri,na serikali ataogopa nini kusema hayo unayoyasema kwa chadema ambao hawana lolote.nyinyi hata mfanye nini amuwezi kukigawa chadema,chadema ni chama makini,mwenyezi mungu amekipanda ili kuwaokoa watanzania kutoka mikononi mwa mafisadi,mwenyezi Mungu awezi kutuacha tuonewe milele, kama alivyompa nguvu Nyerer kututoa mikononi mwa wakoloni ndivyo ilivyo kwa chadema,hivyo mnajisumbua bure
 
Huyu Kisandu yeye ameshajimaliza kisiasa, sasa anajitahidi kumuharibia na Mh.Zitto. Mbona alipokuwa CDM aling'ang'ania kugombea yeye mwenyewe (Kisandu), sasa inakuwaje anamrushia ZK?
 
Huyo hafai kuwa kiongozi wa tawi achilia mbali urais hana nidhamu kwa wakubwa, ana uchu wa madaraka, hana subira, anafikiri ana akili kuliko mtu yoyote, nk. Huyo hafai kwa sasa na akijaribu atakuwa amejimaliza. Hapo alipofika ni pazuri, angetulia asome hekima za uongozi vizuri, apate support na baraka za wazee ipite kama miaka kumi ndio aanzishe move hiyo angefanikiwa lakini sio leo
Salimkabora wala usipati tabu ya kuwajibu,hayo yaliyosemwa hapo sio mawazo ya Zito,hayo ni maneno na mawazo ya wakina magamba,kutaka kuvuruga chadema,Zito sio mtu wa kusemewa
 
tusubiri maana ni inaweza ikawa ilikuwa move mmoja tuvute subira
 
Back
Top Bottom