Zitto ajilipua, tusimtose

Zitto ajilipua, tusimtose

Mi ntaanza kumpinga magufuli akianza kula na wazungu kupitia mikataba feki. Lasivyo mi nabaki na magufuli
 
Hapana siku hizi wana kukokobeach. Hiyo akwilinalisation was just an accident with a Godly blessing
Aisee... haya majamaa yasiyojulikana sijui baba ubaya ameyaibulia wapi...
 
Me nawaza tu zito amepatwa nanin Leo hii juu ya serikal hii mpaka aombe collabor ya wapinzani...kuna kipindi wapinzani bungeni walikuwa wanatoka nje wooote kuishinikiza serikal anabaki ZZK ndani na akamwagiwa sifa kedekede na haohao chichiem bungen..nawaza tuu..kwakwel Mzito simuamin akibanwa kidogo anaachia,nawaza tu ..

Sent from my Retro using JamiiForums mobile app

Inawezekana alikuwa hajakomaa lakini sasa inaonekana amekomaa kupita kiasi, Wakati mwingine matatizo yanakomaza.
Uswahiba wa ZZK na JK ulikuwepo kwa sababu JK alikuwa rafiki wa kila mtu kwa sababu ya diplomasia yake. Jk alikuwa rafiki wa LISSU,MBOWE na SLAA mpaka Marehemu Rev Mtikila. Kifupi diplomasia ya JK ilirahisisha sana maisha yake ya Urais kiasi cha mpaka maadui wa CCM kuona wenzao ndani ya upinzani ni wasaliti lakini hii yote ni diplomasia ya JK katika vita.

Kifupi ZZK alishindwa vita kwa JK, LISSU alishindwa vita kwa JK, Mbowe alishindwa vita kwa JK, Slaa alishindwa vita kwa JK, Lowassa alishindwa vita kwa JK, Marehemu mzee Sita alishindwa vita kwa JK na wengine wengi walishindwa vita kwa JK.
Kwa sasa ni rahisi sana kushinda mapambano maana adui anapanic na hana diplomasia..
 
Zitto umemaizia kwa kusema KURA; lakini kumbuka awamu hii ni nguli wa udukuaji (vibaka) wa kura kuliko awamu yoyote ile.
 
Mi ntaanza kumpinga magufuli akianza kula na wazungu kupitia mikataba feki. Lasivyo mi nabaki na magufuli
Akila na familia yake na watu wake ni sawa tu!!! Hata Mobutu aliwaaminisha wakongo kuwa afadhali yeye awe tajiri katikati ya maskini wakongo badala ya wazungu!! Akajenga jumba lenye uwanjwa wa ndege zake nyumbani kwao!! Alikuwa kama huyu!! Niwaulize kodi tunakusanya sana nini sababu ya umaskini? Tusifikiri kwa masaburi mkoloni mweusi ni fisi mbaya kuliko fisi mnyama
 
Akili ya zitto ni ya kujua mwenyewe,hasira zake ni kuona kitlya mkumbo na mama Ana Mghwira kula shavu yeye bado,na akili yake alifikiri atakua waziri mdogo wa madini,katoswa,ajiunge kwa wale aliowasaliti
Hapa umejibu hoja yake au umeamua kumshambulia tu?
 
Zitto dili zake zote za wizi kupitia kamati na hk kumpeleka nje kila wakati zimebuma amrbaki kupanic. Jpm ni namba nyingine ina msimamo na haiteleshi na majizi ya chadema na akina zitto
 
Nimewahi kusema uongozi huu ndio dhaifu kabisa kwa ushindani wa kisiasa. Na hili limedhihirika kwenye chaguzi mbalimbali za marudi zilizopita. Ni suala la muda tu wananchi waamke. Hapa Zitto kapiga mlemle
Baada ya 10 years mtasema ulikuwa uongozi strong kuwahi kutokea Tanzania...mark my words
 
Baada ya 10 years mtasema ulikuwa uongozi strong kuwahi kutokea Tanzania...mark my words

Kwa bahati mbaya huwa sina maoni ya kufuata mkumbo. Leo hii kuna watu wanamsifu JK hapa, huwa nawaambiwa waziwazi hata JK hakuwa mzuri kwa wapinzani labda kama kipimo chake ni Magufuli. Kwangu mimi bado JK alikuwa rais mwenye msimamo wa wastani na aliyeheshimu demokrasia kwa kiasi chake. Magufuli ni rais mwenye maamuzi bila kujali madhara yake, kwa tabia yake hii akipatia anapatia kwelikweli, na akikosea anafunika hata lile alilopatia. Pia hajali demokrasia kwani sio mtu anayeweza siasa za mijadala bali amri.
 
Zito rudi kwa yule mganga wako wa kikongoman umuombe msamaha na umlipe pesa yake,kwasababu kwa sasa hueleweki,umechanganyikiwa,mvuto kila siku unapotea,
Ndo yule jamaa aliyekasirika hadi akaamua kuripua mitambo na kusababisha nyumba ikashika moto!
 
Kwa bahati mbaya huwa sina maoni ya kufuata mkumbo. Leo hii kuna watu wanamsifu JK hapa, huwa nawaambiwa waziwazi hata JK hakuwa mzuri kwa wapinzani labda kama kipimo chake ni Magufuli. Kwangu mimi bado JK alikuwa rais mwenye msimamo wa wastani na aliyeheshimu demokrasia kwa kiasi chake. Magufuli ni rais mwenye maamuzi bila kujali madhara yake, kwa tabia yake hii akipatia anapatia kwelikweli, na akikosea anafunika hata lile alilopatia. Pia hajali demokrasia kwani sio mtu anayeweza siasa za mijadala bali amri.
During the JK era, the country was rotten to the core. Corruption has killed us. And we needed to exorcise the ghost of corruption. Tukahitaji mtu ambaye anaweza fanya major reforms in our entire system, akaja Magu. Na tunatakiwa tufahamu kila mtu ana mapungufu yake mengi tu cha muhimu ni kuvumiliana. Bado tuna changamoto nyingi sana kama nchi.

Tukirudi kwenye demokrasia, what many people think of democracy ni tofauti. Others think democracy as periodic voting la hasha. Democracy ina mambo mengi ndani yake. Labda yeye for now anaona in order to make things move in a full throttle, with steadiness that he want, that there are needs to limit freedom of political associations in the country. So tumpe muda, ngoja his first term iishe tuone.
 
Kweli kabisa, dikteta keshashindwa kutawala, kampeni ya viwanda ameshaisahau, bombardier kashindwa kununua sasa ameamua kuteka raia, kuagiza wanamgambo wa ccm(green guards) waue raia na kufunga wabunge wa upinzani...dikteta is a one term president...akikaa sana!
 
Huyu jamaa aangalie. Hawa watu wasiojulikana wanaweza wakam pyu pyu pyu akawa Akwilinalized.
Acha woga,sio kila mtu ni kunguru kama wewe,Mh Zitto ameshajitolea muhanga kuwakomboa watanzania,,,kwani unafikiri yeye hajui kama kuna watu wasiojulikana!!? wewe kama nani kuwambia watanzania Zitto aangalie!! msitishe watu, watu wamechokaaa,hali mbaya mitaani
 
Huyu jamaa aangalie. Hawa watu wasiojulikana wanaweza wakam pyu pyu pyu akawa Akwilinalized.

Hamna kitu. Kama ni hivyo, wangeshammaliza. Angalia anavyoruhusiwa kukagua shule na miradi mingine. Tizama anavyokosoa. Lakini hawi treated kama Tundu Lissu au John Heche au Sugu au Lema au Msigwa. Sidhani kama serikali ya sasa hivi itamruhusu Tundu Lissu kukagua miradi na kutembelea shule kama afanyavyo Zitto. Zitto alifanya hata mkutano wa kujadili makinikia etc. Bado kuna kila dalili kuwa anapata preferential treatment ukilinganisha na wanasiasa wengine wa upinzani. Ni kama vile anatumika ku-neutralize mambo kwa kutengeneza mazingira ya watawala kusema mbona Zitto anakosoa na hapati matatizo? Kwamba wanasiasa wengine wa upinzani wanapata shida kwa kuwa lugha yao mbaya. Lakini lengo kuu likiwa ni kudhoofisha upinzani na Zitto akiwa mshirika kwenye mradi huo.
 
Back
Top Bottom