Kilichokiua chadema ni ukanda udini na ukabila full stop.
ACHA KUPOTEZA MUDA WAKO KUPAMBANA NA CHADEMA,NENDA DODOMA UKACHUKUE UFUNDI WA KUZUIA GESI ISITOKE MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya
Chemba, mkoani Dodoma Francis
Mtinga amelazimika kuwapa wazee
wa kimila kondoo wawili kwa ajili ya
tambiko la kuwaondoa nyoka
wanaodaiwa kuzuia miradi ya
maendeleo.
Akizungumza kwa simu jana, Mtinga
alisema uamuzi wa kuwatoa kondoo
hao ulifikiwa baada ya kubaini kuwa
makandarasi wanaofanya kazi
wilayani humo wamepunguza kasi
kutokana na kuhofia nyoka
wanaoaminika kuwa wa kishirikina.
Alisema makandarasi wanaochimba
mashimo kwa kusimika nguzo za
umeme wamekuwa wakikumbana na
nyoka, huku wale wanaofukia
mabomba ya maji wakijikuta katika
wakati mgumu baada ya mabomba
hayo kupasuka kila wanapoyafukia
ardhini.
Mtinga alibainisha kuwa wazee
wanaolalamikiwa kusababisha vioja
hivyo wanadai kwamba baadhi ya
miradi inayotekelezwa na Serikali
inapita katika maeneo yao ya
kutambikia, hivyo walitoa sharti
kuwa ili miradi iendelee lazima
wapewe kondoo.
Wao walikuwa wanataka
tuwatambue, nimeongea nao,
nimewatambua. Nimewapa kondoo
wamechinja tena walikula bila
chumvi. Huwezi kupuuza haya
mambo, maana vibarua wamegoma
kufanya kazi wanaogopa nyoka, sasa
kazi inaanza kusuasua, alisema
Mtinga na kuongeza:
Ni muda mrefu mabomba yalikuwa
yanapasuka, watu walikuwa
wanalalamika kuwa waliondolewa
kupisha ujenzi wa mabomba hayo
bila kupewa fidia na wakasema
watahakikisha yanaendelea
kupasuka. Sasa tumewapa
walichokuwa wanataka tuone
sayansi yao itaishia wapi.
Pia alibainisha kuwa ingawa Serikali
haiamini katika uchawi, historia
inaonyesha kuwa wazee hao
waliwahi kukwamisha mambo
kadhaa ya kimaendeleo baada ya
kukataliwa kupewa kitu
walichokuwa wanakitaka na
kwamba mpaka sasa mambo hayo
hayajapatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wao wananchi
wanaoishi katika maeneo ambako
mradi wa mabomba ya maji umepita,
wamekuwa wakiilalamikia Serikali
kuwa haikuwalipa fidia, hivyo
kuahidi kufanya kila njia
kukwamisha mradi huo.
Akizungumza wakati wa kutia saini
mikataba ya ujenzi wa mifumo wa
usambazaji maji katika vijiji vitano
vya wilaya hiyo juzi, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Chemba,
Mweshimiwa Rajab alikaririwa na
televisheni moja akiwataka
makandarasi kwenda haraka
kuwaona wazee hao ili kunusuru
miradi hiyo isikwamishwe.
Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya
ya Chemba, Robert Mganga
akizungumza kupitia televisheni hiyo
juzi, alisema imani za kishirikina
zinakwamisha utekelezaji wa miradi
ya maendeleo katika wilaya hiyo...
Kila wanapochimba shimo badala ya
kufukua mchanga wanafukua
nyoka, alisema.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Dk
Lutengano Mwakahesya alisema jana
kuwa ofisi yake haiamini katika
ushirikina na kwamba mkandarasi
yeyote atakayeshindwa kufanya kazi
kwa kisingizio cha ushirikina
atawajibishwa.
Sisi tunachojua wakati wa kazi
wanaweza kukutana na mwamba au
jiwe gumu. Rea hawaamini hizo
imani, wananchi wanataka umeme
na siyo kitu kingine, kama mhandisi
akishindwa kutekeleza mradi
tutamtoza faini, alisema.