Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Status
Not open for further replies.
2015 atakuwa na less one year ya kukubalika kikatiba kugombea urais.

Mods peleka huu uzushi kwenye jukwaa husika.
 
asituchanganye aondoke tu kama vipi.zito zito zitoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Wandugu,
Sinauzoefu sana na mambo ya siasa, ila kwa mwenendo wa huyu kijana mwenzetu Zitto kabwe inanipa mashaka...Kwa kweli anaonekana kuwa msaliti wa chama chake cha Chadema kwa kujipendekeza kwa chama tawala. haiingii akilini kusema yeye awe na ukaribu zaidi na kuona yanayofanywa na chama tawala kwa sasa ni bora na yamefanyika mengi...Wapi yule Kabwe wakutetea haki za wanyonge?

TETESI: (chanzo mitaani na kwa wachambuzi tofauti) Amenunuliwa na Serikali ya Jei kei kwa kuahidiwa mustakabali mnono wa maisha, alichoombwa ni afanye mbinu ya kuhamia NCCR na agombee uraisi kwa mwaka 2015 ili kuzigawa kura za CHADEMA
Zitto ni kijana anaekubalika, akitangaza uraisi wengi watamfuata na kuzigawa kura za chama machachari kinachoisumbua kichwa CCM.

WanaJF hili limekaaje jamani?
aende tu anakihelehele sana istoshe amepatikana mtu makini zaid yake bungeni ambaye ni tundu lissu na kama anajidaia ukijana wake yupo mnyika CDM aliikuta ikamfunza siasa kama anadhani kuondoka kwake kutayumbisha chama amedanganywa atapotea kisiasa awe makini
 

Kabla ya Chadema kumtimua/kimsimamisha uanachama Zitto kutokana na kutoendana na malengo ya chama, ingefaa chama hicho kifanye tathmini ya kutosha katika namna ya kumtimua. Bila shaka uongozi wa juu wa Chadema inafahamu nguvu za Zitto zinatoka wapi -- ni kutoka kwa mafisadi ambao wako tayari (kutokana na fedha) kuvishawishi vyombo na mamlka nyingine za serikali kumlinda.

Halafu pia kwa bahati mbaya kuna suala la udini, ambalo Zitto kesha onyesha kwamba huenda atalitumia -- kwamba anatimuliwa kutokana na dini yake -- ingawa hii haiwezi kuwa na mashiko sana pamoja na kwamba yeye ataitumia sana.

Chadema waangalie historia ambayo inaweza kuwaongoza: waangalie jinsi CUF ilivyokuwa inahaha kumtimua mwenyekiti wao wa kwanza James Mapalala. Iangalie jinsi hao hao CUF walivyokwama kuwafukuza Wabunge wao wawili wa viti maalum katika Bunge la 2000-2005 ambapo pamoja na kwamba CUF iliwafukuza uanachama hivyo kupoteza haki yao ya kuwa wabunge, Msekwa, wakati huo Spika, alikataa akasema bado ni wabunge --eti utaratibu hauklufuatwa na upuuzi mwingine etc etc!

Halafu kuna ile lesson ya marehemu Chacha Wangwe, ambayo viongozi wa Chadema lazima waliangalie, hasa kutokana na wabaya wao katika chama tawala walivyokuwa wakijaribu kuwasukumia kwamba wao (viongozi wa Chadema) ndiyo walihusika katika kifo chake eti tu kwa sababu Wangwe alikuwa amepanga kujitoa chamani!

Inawezekana kwa Mapalala, CUF hawakuwa na taabu sana kumtimua, kwa sababu hakuwa Mbunge. Kwa Mbunge kama Zitto (na kama ilivyokuwa kwa wale wa viti maalum wa CUF) inaweza ikawa shughuli nzito kwa Chadema. Bunge (kwa kutumia uwingi wa wabunge wa CCM ndani yake) linaweza kukwamisha kufukuzwa kwa Zitto kwa kisingizio eti kakakat rufaa (bila shaka atakata rufaa mahakamani) etc etc.

Mimi naona kwanza Viongozi wa Chadema wangemsihi ajitoe mwenyewe ajiunge na CCM au chama kingine bila kuleta purukushani kubwa. Kupoteza Mbunge mmoja kwa Chadema si hasara kubwa, hasa Mbunge huyo anaonekana kuwa anakisaliti chama na sera zake.

Akikata basi waanze kumtenga polepole katika vikao vya juu vya chama, asiwe anaalikwa hadi yeye mwenyewe ajihisi kwamba hatakiwi. Nadhani hiyo ndiyo njia sahihi na pekee.

Nawasilisha.
Mkuu kwani kuna mpango wa kumtimua?
 
Zito Zuberi Kabwe anahaki ya kuhamia chama chochote kile. CHADEMA wanatumia sheria na kanuni kuongoza chama, akipotoka watamchukulia hatua muafaka. kila mtu anahaki ya kujipambanua na kuonyesha mtazamo wake akiwamo Zito. Chama makini kama CHADEMA lazima kijipambanue kwa kuongozwa kitasisi na kujenga mfumo imara wa kuingiza wanachama makini na kuwatoa wasaliti. CHadema lazima iondokane na utegemezi wa umaarufu wa watu, kitegemee sera na maono mbadala katika kutafasili mahitaji ya Watanzania na kuyatafutia majibu muafaka.
 
Wandugu,
Sinauzoefu sana na mambo ya siasa, ila kwa mwenendo wa huyu kijana mwenzetu Zitto kabwe inanipa mashaka...Kwa kweli anaonekana kuwa msaliti wa chama chake cha Chadema kwa kujipendekeza kwa chama tawala. haiingii akilini kusema yeye awe na ukaribu zaidi na kuona yanayofanywa na chama tawala kwa sasa ni bora na yamefanyika mengi...Wapi yule Kabwe wakutetea haki za wanyonge?

TETESI: (chanzo mitaani na kwa wachambuzi tofauti) Amenunuliwa na Serikali ya Jei kei kwa kuahidiwa mustakabali mnono wa maisha, alichoombwa ni afanye mbinu ya kuhamia NCCR na agombee uraisi kwa mwaka 2015 ili kuzigawa kura za CHADEMA
Zitto ni kijana anaekubalika, akitangaza uraisi wengi watamfuata na kuzigawa kura za chama machachari kinachoisumbua kichwa CCM.

WanaJF hili limekaaje jamani?

Nani anamkubali? labda kwao kigoma
 
Zitto Kabwe, sasa anatuhumiwa ....

Soma Mwanahalisi la Leo Jumatano tarehe 1/12/2010

Box_front.gif


Guilty until proven innocent? au
Innocent until proven Guilty?

Wengine mnaitikia vibwagizo tu as if ni kasuku.
Think!

Mabadiliko ya kweli Tanzania hayatakuja kwa majungu, dhana na hearsays!

 
Mimi bado siamini lolote linaongelewa dhidi ya CHADEMA na ZITO.
 
CCM hawakuwatimua akina sitta, mwakyembe na wengine nyie mnataka kumtimua zitto? demokrasia ndani ya chadema ni changa mno. mkimtimua zitto mtakuwa ndio mmejimaliza.
 
Mtanzania wa leo hadanganyiki, Zito naye alewe kuwa pamoja na uwezo wake binafsi, CHADEMA imesadia kumfikisha hapo alipo. Tupo wengi tusio kwenye siasa, lkn tunafautilia kwa karibu kila jambo la kisiasa na wanasiasa. Hivyo Chadema wawe makini wasimwenee Zito kwa kujitutumua kwakwe kuonyesha yupo, Lkn zito naye asijione kuwa ni zaidi ya chama kama anavyokili siku zote kuwa chama ni zaidi ya ya yeye. Otherwise asije fuata mkumbo wa kina tambwe, Kablou, Jidawi, Ngawaia, Mrema na wengine wengi walifikiri wanaweza hadaa Wa TZ na watabaki salama.
 
Well Zitto ukihama tutahama na wewe usikhofu tupo na wewe popote utakapoenda
 
Dawa ya yote ni Zitto kunyamaza kimya bila kulia nyau watu wanasema Silence it pays,CDm pia wangesolve hii issue yao katikaa vikao vyao vya ndani magazeti hayatasaidia zaidi yakuchanganya wananchi
 
Akihama itakuwa vizuri kwa kuwa, kuwa na mtu kama huyu kwenye chama ni tatizo kubwa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom