Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Status
Not open for further replies.
Naomba uongozi wa juu wa CDM ufanye utafiti wa hali ya juu kuhusu jambo hili. Baada ya kuridhika wampe nafasi ya kujieleza/kujitetea. Halafu wamtenge kama kweli anatumika kukiua chama.
 
Nadhani ni mapema sana kuanza kuzungumzia CHADEMA kumtimua/kumsimamisha uanachama Zitto. Hiyo itakuwa ni extreme decision na hata mimi nisingependa kuona jambo hilo linatokea. Kinachotakiwa kufanywa hapa ni uongozi wa CHADEMA kumuandikia Zitto barua kumtaka atoe maelezo kuhusu mwenendo wake. Napendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:

(i) Kama Zitto ataonesha uungwana na kukiri makosa yake, basi chama kimpe STERN WARNING kwa kutoa siri za vikao vya chama, kupingana na maamuzi rasmi ya chama na kutoa matamshi hovyo kwa media. Baada ya warning aachiwe aendelee na nafasi zake zote za uongozi wa chama.

(ii) Kama akileta dherewu kwa viongozi wa chama na kukataa kukubali makosa yake, asifukuzwe uanachama. Avuliwe uongozi kama naibu katibu mkuu wa CHADEMA na aendelee kuwa mwanachama na mbunge.

(iii) Iwapo ataonesha dherewu kubwa, kejeli, matusi, kashfa na uhaini waziwazi kwa chama, basi hapo as a last resort ndiyo anaweza kufukuzwa uanachama wa CHADEMA ili kulinda umoja na mshikamano wa chama.

Chonde chonde, tusifanye maamuzi kwa jazba. Pamoja na matatizo yake, Zitto bado ana mchango mkubwa wa kutoa. Ila his actions should not go unpunished. Ni lazima chama kimchukulie hatua kali ili kuwekana sawa. Napendekeza achukuliwe hatua namba (i) iwapo atakuwa muungwana na kukiri makosa yake.
 
Sidhani kama CHADEMA watamfukuza zitto chamani kwa sababu kufanya hivyo kutakidhoofisha na kukiyumbisha chama kutokana na ushawishi alionao zito. Kumbuka kuwa kumekuwa na upepo unaodai u-kaskazini katika chadema. Kitendo cha kumfukuza uanachama zito kwa sababu yoyote ile (Unless it is a very obvious reason) kitakuwa ni sawa na kugongea muhuri wa kuthibitisha hii dhana na propaganda inayoenezwa; kitu ambacho kitatumiwa na wabaya wa chadema kukidhoofisha chama.

Kwa mtizamo wangu nadhani endapo itaonekana kwamba mwenendo wa zito utahitilafiano na maagizo ya chama kiasi cha kuathiri chama, Chadema itatakiwa kumwita na kumuonya na kama atakua hasikii basi wanaweza kumvua uongozi lakini sii uanaachama.
Cha kuangalia ni kwa uongozi wa CHama kutomruhusu zito kutumia umaarufu wake ku-blackmail chama kifanye kama atakavyo kwa sababu kufanya hivyo ni kukipoteza chama. Endapo itatokea kuwa Zito amevuliwa uongozi ndani ya chadema kutokana na utovu na nidhamu, sidhani kama ataendelea kuwa loya kwa Chama kwa sababu kwa kumuangalia sioni kama ni mtu humble, nadhani atakihama chama yeye mwenyewe.

Kwa hiyo kama god forbid in the future itabidi kuchukua hatua kama hiyo lazima kuwepo na 'Plan B' ya kuziba Damage itakayosababishwa na kuondoka kwake.
 
Japo sikubaliani na kila anachofanya Mh. Zitto naona sasa tunavuka mpaka. Mnataka afe au ajinyonge ndio mfurahi? Kila kukicha Zitto kwani yeye malaika? Mimi naipenda CHADEMA na nakubali Zitto amefanya makosa mara kadhaa lakini the way watu wanamshambulia kwa sasa inatia kinyaa. Tufike mahali tyumwache yeye mwenyewe kama akihama/akifukuzwa/asamehewa au akiamua kuachana nasiasa iwe ni kwa uamuzi wake mwenyewe maana sasa inaonekana sasa hao chadema na Zitto si ajabu wameshayamaliza sasa nyie mmebaki kumshambulia tu kijana wa watu.
:embarrassed:
 
My advice would be apokonywe uNaibu Katibu Mkuu. Abaki ordinary member of the party. Atajifukuza mwenyewe. Ila utoto unamsumbua.
Utoto umetokana na inferiority complex. Umetoka ktk umaskin sasa leo akikaa na majina makuu ya ufisadi anafurahia joto. That blinds his little judgement mwishowe amesahau alikotoka na mchango wa chama kumfikisha alipo.
Look at his record & foresee his future. Alikuwa machachari wakusumbua serikali. Mara hii machachari wakuvuruga chama. Can u see this?
 
Zitto ni kirusi hatari sana hafai kuendelea kuwa kiongozi au mwanachama wa CDM.. Hatupiliwe mbali huko tumechoka kusikia ujinga wake.
 
Wandugu,
Sinauzoefu sana na mambo ya siasa, ila kwa mwenendo wa huyu kijana mwenzetu Zitto kabwe inanipa mashaka...Kwa kweli anaonekana kuwa msaliti wa chama chake cha Chadema kwa kujipendekeza kwa chama tawala. haiingii akilini kusema yeye awe na ukaribu zaidi na kuona yanayofanywa na chama tawala kwa sasa ni bora na yamefanyika mengi...Wapi yule Kabwe wakutetea haki za wanyonge?

TETESI: (chanzo mitaani na kwa wachambuzi tofauti) Amenunuliwa na Serikali ya Jei kei kwa kuahidiwa mustakabali mnono wa maisha, alichoombwa ni afanye mbinu ya kuhamia NCCR na agombee uraisi kwa mwaka 2015 ili kuzigawa kura za CHADEMA
Zitto ni kijana anaekubalika, akitangaza uraisi wengi watamfuata na kuzigawa kura za chama machachari kinachoisumbua kichwa CCM.

WanaJF hili limekaaje jamani?


Kugombea uraisi hamna kigezo cha umri? Atakuwa amefikia umri unaoruhusiwa?
 
Naungana na waliotangulia, mambo mazito kama hayo hayahitaji haraka wala hasira. Aitwe kwenye vikao vya chama na aelezwe akikaidi avuliwe nyadhifa zake na abaki tu kama mwanachama
 
Zitto ni kiongozi mzuri na kamwe asichoke kujifunza pamoja na kuwa na elimu nzuri, maamuzi ya wengi yana maana kubwa katika kukuonesha wewe ni nani na unataka nini. Kupingana bila kupigana ndiyo siasa sahihi, politics of limited objectives.

Naunga mkono hatua ya chadema kutaka maeleo kutoka kwa wabunge wake ambao hawakuhudhuria kikao cha bunge, utawala unahitaji kitu kama hiki na kamwe huwezi kuongoza taasisi kama bata au kambale, ni lazima taratibu ziwepo na ziheshimiwe hata kama unadhani zina mapungufu ama huzipendi
 
Nadhani ni mapema sana kuanza kuzungumzia CHADEMA kumtimua/kumsimamisha uanachama Zitto. Hiyo itakuwa ni extreme decision na hata mimi nisingependa kuona jambo hilo linatokea. Kinachotakiwa kufanywa hapa ni uongozi wa CHADEMA kumuandikia Zitto barua kumtaka atoe maelezo kuhusu mwenendo wake. Napendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:

(i) Kama Zitto ataonesha uungwana na kukiri makosa yake, basi chama kimpe STERN WARNING kwa kutoa siri za vikao vya chama, kupingana na maamuzi rasmi ya chama na kutoa matamshi hovyo kwa media. Baada ya warning aachiwe aendelee na nafasi zake zote za uongozi wa chama.

(ii) Kama akileta dherewu kwa viongozi wa chama na kukataa kukubali makosa yake, asifukuzwe uanachama. Avuliwe uongozi kama naibu katibu mkuu wa CHADEMA na aendelee kuwa mwanachama na mbunge.

Hapa pa kumvua uongozi pana ugumu, Sidhani kama atakubali kuvuliwa uongozi na kuendelea kukaa katika chama bila kuleta madhara yoyote katika chama. Nionavyo aweza kuendelea kubaki chamani ili asipoteze ubunge wake lakini akawa mwiba wa kukibomoa chama ili ajipatie umaarufu. Nionavyo mimi huyu dogo anapenda sana umaarufu kiasi kwamba yuko tayari kufanya controvesy yoyote ili aachive goals zake.

Hata hivyo, Ni lazima kuwe na PLAN B katika maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na Chadema
 
Who said anatimuliwa..... aint we getting ahead of ourselves.... or rather putting a cart infront of a horse
 
Watanzania wa leo wako makini, wanaweza kuzichambua mbichi na mbivu na Mungu anawadhihirishia hayo kama ambavyo inajionyesha kwa Zitto. Shukuruni Mungu haya ya Zitto ni baada ya uchaguzi na yatapatiwa ufumbuzi hopefully bila kuathiri mstakabali wa chama kwa kiasi fulani! Zitto anaweza kumfuata EL na kubakia na vyeo vya kuteuliwa maana hata wananchi wake hawafurahii anayoyafanya kwa sasa. Mimi namuomba ajiunge na CCM tunamkaribisha tuzidi kuendeleza mambo yetu ya Buzwagi!
 
Dawa ya yote ni Zitto kunyamaza kimya bila kulia nyau watu wanasema Silence it pays,CDm pia wangesolve hii issue yao katikaa vikao vyao vya ndani magazeti hayatasaidia zaidi yakuchanganya wananchi

je zitto ataweza kukaakimya hasiende magazetini?
 
Mimi bado siamini lolote linaongelewa dhidi ya CHADEMA na ZITO.
True now more than never, we need to be carefull there is a lot of kupakana matope...... going on... For whose benefit I dont know, but for sure its not for Tanzanians, Lots of unansweared questions....
 
Mimi wasiwasi wangu ni kuwa hawa wanaomtumia Zitto kuisambaratisha Chadema wakikifikia asilimia kubwa ya lengo watamkolimba kisha wawasingizie viongozi wa Chadema kuwa ndiyo wauaji kama walivyofanya kwa marehemu Chacha Wangwe.Hawa waajiri wake wa siri mikono yao imejaa damu.
 
Tatizo kubwa ninaloliona la CDM kuhusu Zitto ni moja tu -- kwamba nguvu zake ziko nje ya CDM, siyo ndani. Sasa hao wa nje wata-react vipi?a, na hapa ninamaananisha katika uongozi wa juu wa chama. Inawaezekana kwa wafuasi wa CDM wa kawaida wanamuona Zitto ni shujaa -- lakini hawa hawana nguvu za kimaamuzi -- na Zitto analielewa hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom