Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Status
Not open for further replies.
Since ameshachaguliwa basi tumwache afanye kazi...... This critising wont help anyone..... Lets reserve our judgement and see what he can do you know once bitten twice shy.... probably kajifunza
 
Gazeti linalomilikiwa na CHADEMA kila asubuhi linamnanga Zitto kulikoni? au ndio "Akufukuzae hakwambii toka"?
 
Huyo kijana nimtu anayetaka umaarufu sana na hapo mjue anachokifanya ni kutafuta umaarufu ila hajaasi chama bado ni mtu muadilifu sana na humwaambii kitu kuhusu chadema hapo anawakebehi ccm tuu ngoja bunge lianze wachaneni na magazeti ZITTO bado ni mtu safi sana na chama kinamtumbua chadema wanaona mbali sana ingekuwa yupo nje ndani ungeshasikia tamko la pipoos power chap chap wacheni kuamini mwanahalisi
 
Sina imani na Zitto ata Kidogo

Zitto kama ni mpenda mageuzi na anaitakia nchi yetu mema angeachia gazi both bungeni na kwenye chama, tusonge mbele. Chadema wameshakuona wewe Zitto kama sell-out kwa hiyo kwenye vikao itakuwa ngumu sana kuzungumzia mikakati ya siri na wewe ukiwepo. Kunusuru chama ni vizuri Zitto ukabaki kama mwanachama wa kawaida. Huwezi kutoa siri za kikao TBC and yet uwe kwenye inner circle. Ulifanya makusudi maana ulisema unangojea hukumu yako.
 
kwa wengi ambao hammjui huyu mbunge kijana mtakuwa mnashangaa sana why anakegeuka kegeuka kila mara ila kwa mliokuwepo chuo wakati akisoma na hasa 2001/2002, hamuwezi shangaa sana leo kubadilika badilika kwa kijana huyu, ni mtu anayependa sana sifa binafsi na wala si kwa ajili ya group zima, anapenda kuonekana yeye kama yeye na wala siyo wengine, asipokuwa makini naye pia ataanguka kama mzee wetu mrema na kijana wetu mbatia, bora hata mrema umri umekwenda na si kama anguko la mbatia, so asipokuwa makini hakika 2015 harudi sehemu yeyote ile, kazi kwake, kwani kwetu sisi ni kurekebisha pale palipo na mapungufu yanayooneka

Tahadhari ilishatolewa kuwa huyu bw. mdogo ni nduwila kuwili na mganga njaa ile mbaya . Anaombagaombaga kama wale wanamuziki wetu toka pande zile za jirani na Kigoma . Hana tofauti kabisa japo kasoma soma. Ni mtu hatari zaidi maana ni mbea na spinner. Ahamie tu huko kwa mafisadi aachanae na wapambanaji. Hebu fikiria eti anadhani Kikwete atampa UWAZIRI .... insanity of its kind .
 
huyu tulimwambia atulie humu jamvini lakininaona bado ................
 
Waswahili wamesema zamani "Akufukuzae hakwambii toka".

Gazeti linalomilikiwa na CHADEMA kila asubuhi linamnanga Zitto kulikoni?

You know there is more than what meets the eye......
Kama ni kweli Zitto kafanya hayo kwanini Gazeti lisiandike? kama ni kweli lakini?
Kama anasingiziwa ni kwanini? Na kwanini Chama kisifuatilie hayo?
Am sure ndani ya Chama wanajua ukweli upo wapi? Na sidhani kama Chama kinaweza kufungia macho uonevu kama kweli wanamuonea
My Advice these things should be sorted... and nobody needs to know.
 
Ukiona hivo ujue umaarufu wa zitto ni tishio kwa vigogo wa cdm hasa akina mtei mbowe families,sas lazima wamchafue.Kumbuka:Aliyekwezwa na Mungu hakuna wa kumshusha
 
Atahamia sisiemu tu, ameshashtukia mambo ya CHADEMA (kuwekwa chambo/chachu) ya kisiasa

Yaani weeee acha tu huyu kijana namfahamu toka Tosamaganga alivyoongoza mapinduzi na kumn'goa kiongozi wa wanafunzi aliyekuwa madarakani, Pia jinsi alivyokuwa akitembea na secretary wa H/Master pale Tosa alivyokuja chuo mimi tayari nilimshamstukia for his erratic behaviour na nilikuwa sisiti kutamka wazi kuhusiana na tabia ya huyu Kijana h na alipoungana na yule mwenzake Rugemalira situation ikawa very worse.....ZITTO TAFADHALI ONDOKA CHADEMA ..KWANI KUCHEZA NA CHADEMA NI SAWA NA KUCHEZA NA NGUVU ZA UMMA..ONDOKA HARAKA. SI ULISEMA UNATAKA KUWA LECTURER NA SASA KWAMBA SIASA BASI? NENDA KAFUNDISHE MZUMBE.
 
siku ile weberoya alipoleta ile thread humu nilimuonya huyu kijana kwa sauti kubwa na weninge wengi walifanya hivyo
lakini inaonekana habadiliki

hana ADABU
 
Atahamia sisiemu tu, ameshashtukia mambo ya CHADEMA (kuwekwa chambo/chachu) ya kisiasa
Ana mpango wa kugombea urais 2015 hivyo si rajisi sana kwenda ccm na si rahisi pia kuendelea ndani ya cdm. Nadhani sasa hivi annangali wapi anaweza kukubalika kwa urahisi ili atorokee huko. NCCR linaweza kuwa chaguo litakalomfaa.
 
You know there is more than what meets the eye......
Kama ni kweli Zitto kafanya hayo kwanini Gazeti lisiandike? kama ni kweli lakini?
Kama anasingiziwa ni kwanini? Na kwanini Chama kisifuatilie hayo?
Am sure ndani ya Chama wanajua ukweli upo wapi? Na sidhani kama Chama kinaweza kufungia macho uonevu kama kweli wanamuonea
My Advice these things should be sorted... and nobody needs to know.

Haya bwana.

Mimi ninachokiona kutokana na yote haya ni 'mvurugano' ndani ya chama. Ikiwa ni kweli Zitto hufanya yale yanayosemwa basi mgongano upo na ikiwa anazuliwa vile vile inaonyesha mgongano upo.

CHADEMA tokea baada ya uchaguzi imekosa dira, kauli zenye kupingana baina ya viongozi zimekuwa nyingi kuliko kauli zenye muelekeo mmoja.
 
Kama haya yanayosemwa kila siku kumhusu Zito ni ya kweli Chadema inabidi wakae chini wachukue hatua. Ni bora wakamoffload Zito sasa hivi ili wawe na nafasi ya kujipanga mapema kuliko aje ajitoe mwenyewe karibu na 2015 ambayo itakuwa na negative impact kwa chama pasipokuwa na nafasi ya kujiweka sawa.
 
Kosa alilofanya Zitto ni kuingia kwenye Kamati ya Madini! hilo ndilo linalotafuna profile yake!
Huwezi ingizwa kwenye kamati ya wanasheria vichwa kama bomani ukiwa kijana vile tena kwenda kwenye mzinga wa asali uliokimbiwa na nyuki halafu utoke bila kuvimbiwa asali! labda usiwe mpenda asali! otherwise you will fall in the trap!
Zitto aliangukia mtegoni! wakulaumiwa ni viongozi wa CHADEMA kumruhusu kuingia kwenye kamati!
 

Kabla ya Chadema kumtimua/kimsimamisha uanachama Zitto kutokana na kutoendana na malengo ya chama, ingefaa chama hicho kifanye tathmini ya kutosha katika namna ya kumtimua. Bila shaka uongozi wa juu wa Chadema inafahamu nguvu za Zitto zinatoka wapi -- ni kutoka kwa mafisadi ambao wako tayari (kutokana na fedha) kuvishawishi vyombo na mamlka nyingine za serikali kumlinda.

Halafu pia kwa bahati mbaya kuna suala la udini, ambalo Zitto kesha onyesha kwamba huenda atalitumia -- kwamba anatimuliwa kutokana na dini yake -- ingawa hii haiwezi kuwa na mashiko sana pamoja na kwamba yeye ataitumia sana.

Chadema waangalie historia ambayo inaweza kuwaongoza: waangalie jinsi CUF ilivyokuwa inahaha kumtimua mwenyekiti wao wa kwanza James Mapalala. Iangalie jinsi hao hao CUF walivyokwama kuwafukuza Wabunge wao wawili wa viti maalum katika Bunge la 2000-2005 ambapo pamoja na kwamba CUF iliwafukuza uanachama hivyo kupoteza haki yao ya kuwa wabunge, Msekwa, wakati huo Spika, alikataa akasema bado ni wabunge --eti utaratibu hauklufuatwa na upuuzi mwingine etc etc!

Halafu kuna ile lesson ya marehemu Chacha Wangwe, ambayo viongozi wa Chadema lazima waliangalie, hasa kutokana na wabaya wao katika chama tawala walivyokuwa wakijaribu kuwasukumia kwamba wao (viongozi wa Chadema) ndiyo walihusika katika kifo chake eti tu kwa sababu Wangwe alikuwa amepanga kujitoa chamani!

Inawezekana kwa Mapalala, CUF hawakuwa na taabu sana kumtimua, kwa sababu hakuwa Mbunge. Kwa Mbunge kama Zitto (na kama ilivyokuwa kwa wale wa viti maalum wa CUF) inaweza ikawa shughuli nzito kwa Chadema. Bunge (kwa kutumia uwingi wa wabunge wa CCM ndani yake) linaweza kukwamisha kufukuzwa kwa Zitto kwa kisingizio eti kakakat rufaa (bila shaka atakata rufaa mahakamani) etc etc.

Mimi naona kwanza Viongozi wa Chadema wangemsihi ajitoe mwenyewe ajiunge na CCM au chama kingine bila kuleta purukushani kubwa. Kupoteza Mbunge mmoja kwa Chadema si hasara kubwa, hasa Mbunge huyo anaonekana kuwa anakisaliti chama na sera zake.

Akikata basi waanze kumtenga polepole katika vikao vya juu vya chama, asiwe anaalikwa hadi yeye mwenyewe ajihisi kwamba hatakiwi. Nadhani hiyo ndiyo njia sahihi na pekee.

Nawasilisha.
 
Wandugu,
Sinauzoefu sana na mambo ya siasa, ila kwa mwenendo wa huyu kijana mwenzetu Zitto kabwe inanipa mashaka...Kwa kweli anaonekana kuwa msaliti wa chama chake cha Chadema kwa kujipendekeza kwa chama tawala. haiingii akilini kusema yeye awe na ukaribu zaidi na kuona yanayofanywa na chama tawala kwa sasa ni bora na yamefanyika mengi...Wapi yule Kabwe wakutetea haki za wanyonge?

TETESI: (chanzo mitaani na kwa wachambuzi tofauti) Amenunuliwa na Serikali ya Jei kei kwa kuahidiwa mustakabali mnono wa maisha, alichoombwa ni afanye mbinu ya kuhamia NCCR na agombee uraisi kwa mwaka 2015 ili kuzigawa kura za CHADEMA
Zitto ni kijana anaekubalika, akitangaza uraisi wengi watamfuata na kuzigawa kura za chama machachari kinachoisumbua kichwa CCM.

WanaJF hili limekaaje jamani?
 
Mwaka 2015 umri wa Zitto utakuwa bado kuruhusiwa kugombea urais, huu ni uongo na upuuzi na uzushi.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom