Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Status
Not open for further replies.
Nilimsikiliza Lissu akizungumzia swala hilo,hakuzungumza kuhusu kumfukuza yeyote Chamani ila alizungumzia kutaka maelezo ya utoro Bungeni toka kwa wabunge hao waliokosekana siku ile akiwemo Zitto. Hata hivyo alimtaja Zitoo kwa nafasi yake kama kiongozi msaidizi wa kambi ya upinzani Bungeni.
Dalili nikuwa kama maelezo yake hayataridhisha anaweza kupoteza wadhifa huo wa msaidizi wa kiongozi wa upinzani.
 
Lets say for argument sake the boy is innocent...... Brothers and Sisters dont you think this is harsh.... I Suggest with this kind of information we better come with full proof rather than accusing someone who might or might not be innocent
 
Sura halisi ya Zitto imeshajitokeza kama ilivyo kwa James Mbatia, hawezi kuungwa mkono na mwanamageuzi yoyote wa ukweli, huyu ni msaliti,mbinafsi na anayependa kujipendekeza kwa JK. Kama akienda NCCR ni sawa na ndipo anapostahili kwani kisha tuma watangulizi wake huko. ZITTO NI ZIGO LA MAVI CHADEMA HALIBEBEKI.
 

Kabla ya Chadema kumtimua/kimsimamisha uanachama Zitto kutokana na kutoendana na malengo ya chama, ingefaa chama hicho kifanye tathmini ya kutosha katika namna ya kumtimua. Bila shaka uongozi wa juu wa Chadema inafahamu nguvu za Zitto zinatoka wapi -- ni kutoka kwa mafisadi ambao wako tayari (kutokana na fedha) kuvishawishi vyombo na mamlka nyingine za serikali kumlinda.

Halafu pia kwa bahati mbaya kuna suala la udini, ambalo Zitto kesha onyesha kwamba huenda atalitumia -- kwamba anatimuliwa kutokana na dini yake -- ingawa hii haiwezi kuwa na mashiko sana pamoja na kwamba yeye ataitumia sana.

Chadema waangalie historia ambayo inaweza kuwaongoza: waangalie jinsi CUF ilivyokuwa inahaha kumtimua mwenyekiti wao wa kwanza James Mapalala. Iangalie jinsi hao hao CUF walivyokwama kuwafukuza Wabunge wao wawili wa viti maalum katika Bunge la 2000-2005 ambapo pamoja na kwamba CUF iliwafukuza uanachama hivyo kupoteza haki yao ya kuwa wabunge, Msekwa, wakati huo Spika, alikataa akasema bado ni wabunge --eti utaratibu hauklufuatwa na upuuzi mwingine etc etc!

Halafu kuna ile lesson ya marehemu Chacha Wangwe, ambayo viongozi wa Chadema lazima waliangalie, hasa kutokana na wabaya wao katika chama tawala walivyokuwa wakijaribu kuwasukumia kwamba wao (viongozi wa Chadema) ndiyo walihusika katika kifo chake eti tu kwa sababu Wangwe alikuwa amepanga kujitoa chamani!

Inawezekana kwa Mapalala, CUF hawakuwa na taabu sana kumtimua, kwa sababu hakuwa Mbunge. Kwa Mbunge kama Zitto (na kama ilivyokuwa kwa wale wa viti maalum wa CUF) inaweza ikawa shughuli nzito kwa Chadema. Bunge (kwa kutumia uwingi wa wabunge wa CCM ndani yake) linaweza kukwamisha kufukuzwa kwa Zitto kwa kisingizio eti kakakat rufaa (bila shaka atakata rufaa mahakamani) etc etc.

Mimi naona kwanza Viongozi wa Chadema wangemsihi ajitoe mwenyewe ajiunge na CCM au chama kingine bila kuleta purukushani kubwa. Kupoteza Mbunge mmoja kwa Chadema si hasara kubwa, hasa Mbunge huyo anaonekana kuwa anakisaliti chama na sera zake.

Akikata basi waanze kumtenga polepole katika vikao vya juu vya chama, asiwe anaalikwa hadi yeye mwenyewe ajihisi kwamba hatakiwi. Nadhani hiyo ndiyo njia sahihi na pekee.

Nawasilisha.


Nakubaliana nawe. Atengwe kidogo kidogo hadi yeye mwenyewe ajhisi hatakiwi aondoke -- kama vile CUF walivyofanya kwa Lwakatare. Aliondoka mwenyewe.

Ikumbukwe kwamba hakuna kitu kibaya kwa kiongozi yoyote kama kutengwa ne wenzio!
 
Mimi nakubaliana na wale wanaosema aitwe na ajieleze yote kutokana na ushahidi utakaotolewa dhidi yake. Kila hatua ifanywe kufuata katiba ya chama -- maana 'watu wake' wanaompa jeuri wana fedha ya kwenda mahakamani. Na huyu Zitto anaonekana atakwenda tu mahakamani hata kupata injuction ya kuzuia kufukuzwa ikibidi majaji kuhongwa watahongwa tu.

Kwa ujumla CDM wawe very careful kuhusu Zitto -- amekuwa snake katika chama na anaonekana kuwa na malengo mabaya kwa kambi ya upinzani. Hii yote inatokana na ukweli kwamba CDM imefanya vizuri katika uchaguzi mwaka huu na CCM haikufurahishwa -- na badala ya kufanya siasa za kistaarabu, zinaanza siasa chafu kama vile walivyofanya kwa NCCR baada ya 1995.
 
Mimi hili jambo bado sijapata kina haswa kwani sikuweza kumsikiliza Tindu au kusoma magazeti. ila kwa haraka tuu yaonekana Zito ana mkakati wa kupambana na uongozi waCDM ili kujipatia umaarufu kwa mafisadi na yeye binafsi kunufaikaa.

kwa CDM, tatizo la Zito linatibika ni kuacha jazba kulishughulikia na kutoa nafasi ya vikao rasmi kulijadili pia umma upewe nafasi ya kumtambua Zito kama msaliti wa demokrasia nchin.

Kwa sasa siungi mkono tamko la kumfukuza uanachama bali aonywe na vikao rasmi kwa busara zaidi. natumai wazee wa CDM wapo na ni watu makini wana uwezo mkubwa kulishughulikia jambo hili kistaarabu na kuijenga CDM zaidi.
 
Mkuu una mawzo ya kujenga! kwanini usiingie kwenye siasa ugombee uongozi utoe mawazo yako hayo? ndipo utakapotambua kuwa vitumbua sio andazi!
 
bora wamvue uongozi wa unaibu bungeni na unaibu katibu mkuu chamani huyu jamaa mtu aliyempa kiburi hiki chjote ni mbowe mwenyewe wakati akiwa katika harakati za kuwavuta vijana kujiunga na cdm sasa kumwambia acha ni vigumu
 
Yeye ni maarufu tayari ila umaarufu wake ndo tishio kwa vigogo wa chama ndio maana inaelekea hata wamewahonga baadhi ya wanajf ili kumshugulikia zitto.ninasema mmehongwa kwa sababu mfano mimi nilivyo bize sijui kama naweza pata muda wa kuanza kuhangaikia imposibles
 
Mimi wasiwasi wangu ni kuwa hawa wanaomtumia Zitto kuisambaratisha Chadema wakikifikia asilimia kubwa ya lengo watamkolimba kisha wawasingizie viongozi wa Chadema kuwa ndiyo wauaji kama walivyofanya kwa marehemu Chacha Wangwe.Hawa waajiri wake wa siri mikono yao imejaa damu.


...na kwa bahati mbaya kabisa, yeye mwenyewe hajaliona hili.

 
Kuna thread moja ililetwa hapa ilikuwa inamzunguzia kwa kiini dhamira za Godfather Edwin Mtei na Chadema lakini kwa bahati mbaya mods waliifutilia mbali. Kwa kifupi mwandishi ameandika kwa kirefu mikakati ya Chadema na kuwagusia waandishi wa habari wawili ambao wapo kwenye mkakati huo pengine kwa kutumiwa bila kujua au kwa malengo maalum na majina yao yalitwajwa kuwa ni Jenerali Ulimwengu na Saed Kubenea. Kwa mikakati yake sishangai kuona Zitto anaandamwa na nani anajua who next? Arfi? Slaa? or Tundu Lissu? Tuombe uhai tuone. Na nitashukuru kama kuna mtu aliwahi kucopy yale maelezo maana mie ninayo in hard copy.


Si uiscan na kutuwekea hapa!!! Halafu hiyo info unajuaje credibility yake maana mtu yeyote anaweza kuja na story kama hiyo. Au kwa vile Mod aliifuta basi unafikiri ni genuine info siyo??
 
Some chadema fans never cease to amaze me!!

kwa akili yako ndogo mleta maada humu, hakuna mwenye uwezo wa kumtimua Zitto ndani ya chadema huyo hayupo!!!! hata wakae kikao na Mtei deliberately wamtimue hakuna!!!! unapoandika maada kama hizi uwe mwangalifu sana

Halafu kumbuka childish ideas kwenye siasa ni kujitukana, hujasema zito amekosea kitu gani na kwa nini afukuzwe! kama ni kutoenda bungeni walikuwa wengi tu hawakwenda bungeni!!! hupo hapo??

Akina Mbowe na Slaa hawatamweza Zitto walishamkosea na kijana kafyatuka sasa! mtatumia wee magazeti ya tz daima na mwanahalisi hamtaweza!!! ukishukutana na mtu anajiita mwanaume anashindwa ku-mface Zito na kwenda gazetini, wakati mko chama kimoja na wote mna vyeo ni weakness!!!

chadema naona mmepania sana kujiimarisha kwa style ya kutafuta mchawi nani, kupigana na Cuf, to me I am curious, this makes you guys aidha vilaza wa siasa, au hamjui mnaongea nini, yaani mnachefua, unajiona ukija tu JF unaweza andika lolote, wenye akili wanawaangalia

Lissu hajasema swala la kufukuzwa ila vikasuku vimerukia na kujipa moyo, na mwingine anaanzisha maada iko digrresive!!! what a shame!!
 
The Zitto Kabwe problem is something that CHadema will have to deal with but I think Zitto will eventually make a more nuisance of himself sooner that later and perhaps jump ship. At this rate I don't see Zitto going far with Chadema. Someni ukurasa wa 4 wa MwanaHalisi ya leo kuna makala nzuri kuhusu Zitto Kabwe. Kuna kitu kimoja dhahiri Kabwe anafikiri ni maarufu kuliko Chama kama alivyo Mrema. Tofauti yake na Mrema ni kwamba Mrema angalau alishakuwa waziri. Kabwe Zitto atatimkia huenda NCCR lakini ataishia kuwa Kiongozi wa chama tu. Binafsi kitendo chake cha juzi kimemshusha sana machoni mwa wapenzi wake ikiwemo na mimi. Where the notion of collective responsibility? With leaders like Zitto who needs fifth columnists in Chadema?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom