Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Dec 1, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Zitto Kabwe, sasa anatuhumiwa kuyumbisha Chama chake kwa kukiingiza katika mahusiano ya mashaka.
  Naibu katibu mkuu huyo wa CHADEMA anafanya mawasiliano nje ya Chama chake ambayo wachunguzi wameeleza yanaweza kukigawa Chama na kukiangamiza.

  1.Anamahusiano ya karibu na watuhumiwa wa ufisadi.
  Taarifa zilizopatikana jijini Dar es salaam zinasema licha ya Zitto kuwa karibu sana na watuhumiwa wa ufisadi pia ANAJIPENDEKEZA kwa Rais (anayemtambua) jAKAYA kIKWETE.

  Waziri mmoja mwandamizi katika Serikali ya Kikwete ameliambia Mwanahalisi kuwa "KUJIKOMBA KWA ZITTO KWA RAIS KUMELENGA KUGOMBANISHA BAADHI YA MAWAZIRI NA RAIS NA MAWAZIRI KWA MAWAZIRI"

  "Huyu Bwana mdogo anachukua habari maneno huku anapeleka kule....Mara ameomba uwaziri. Mara hivi....Mara vile, ili mradi ni shida. Kuna siku Rais alisikika akisema Kwanini huyu bwana mdogo asiimarishe Chama Chake kuliko haya anayoyafanya?" Ameeleza waziri huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

  2. Mbali na kuwa na mawasiliano na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, Zitto amedaiwa kuwa na Tabia ya kuwasiliana na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari na kujiandikia habari huku wao wakitakiwa WAZIPATE KAMA ZILIVYO
  Kwa mfano, katika mawasiliano yake na mmoja wa wahaririwa gazeti moja lonalotoka kila siku nchini (jina tunalo) Zitto ANAELEZA:
  ........"Hii ripoti inapaswa kusomwa siku ya Jumatano. Nimekutumia wewe pekee. So I expect a build up siku ya Jumatano bila ya kutoa details na stori ya Alhamis iandaliwe vizuri na kwa muda mrefu labda ikiwemo na Q and A (maswali na majibu) na mimi katikati katika kutoa elaboration. Yaani tufanye splash mbele with issues and graphs"
  Akiandika kwa kuagiza kama mhariri wa gazeti, Zitto anasema, "Jumatano yaweza kuwa na stori" huku akipendekeza kichwa cha habari kuwa " ZITTO ANA SIRI NZITO.........."
  Anasema, Nadhani ukishafanyia editing nimpe .......(anataja jina)..kwa stori building maana yeye ataikosa.......... Pia tumpe na .......(anataja tena jina). Hao tu"

  Zitto naeleza kwa njia ya barua pepe " Nataka pia IPP media wakose kabisa na wasikie ukumbini tu ili waendelee na maspin yao ya kina Kilango.
  Mawasiliano kama hayo aliwahi kuyafanya na mhariri wa gazeti la kila siku siku mbili kabla ya Rais Kikwete kuhutubia Bunge.
  Katika mawasiliano yake na Mhariri hiyo Zitto anasema..............."Nimekutumia hii nyaraka, naomba uifanyie kazi. Lakini kesho unaweza kuwa na stori: Muundo wa Baraza la mawaziri. Kikwete kushirikisha wapinzani. Tamko la chadema latibua."

  Katika hatua nyingine Zitto anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya karibu na ya kikazi na Maria Kejo, mtumishi wa serikali anayetuhumiwa na Chadema katika kashfa kadhaa nchini.

  Soma Mwanahalisi la Leo Jumatano tarehe 1/12/2010
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  I think Mwanahalisi should cool a bit and leave Zitto for now... Give a boy a second Chance... We all deserve that
   
 3. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mhhh haya sasa.....
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Zitto Kabwe = Augustine Lyatonga Mrema

  A lot of non sense from them!!
   
 5. i

  igoji Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni kijana na nilikua navutiwa sana na wanasiasa vijana kama Zitto, Mdee, etc. ambao kwa michango yao bungeni imenifanya nijivunie kwamba vijana tunaweza kubadili nchi hii. Sasa haya mambo anayofanya Zito yananivunja moyo kabisa, "Simpendi na wala sitaki kumsikiliza tena".:Cry::Cry:. Mdee na Mnyika ndio mliobakia moyoni kwangu, nanyi mkiharibu basi naacha kufuatilia Siasa.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hakika ANGUKO LA ZITTO limekaribia sasa
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Binafsi nimekuwa shabiki wa mheshimiwa zitto zuberi kabwe, mkigoma huyu alinishawishi sana niamini ktk mrengo wa siasa zake ila nilipomuona anamsogelea muungwana kwa mapambio kama john cheyo basi nikahisi hapa hatuna mtu mwenye courage ya kisiasa bali mpenda ummarufu kwa gharama yoyote ile in the name of democrasy. Nasema sasa nimeliamini hili baada ya hamad rashid wa cuf pale moven pick alipojipambanua eti yeye ni mwanasiasa mzoefu mbele ya mbowe!!! Hamad rashid anataka tuamini kuwa zitto ameshinda ubunge kwa kura za waislamu tu!!!! Maana amesema siku ile kuwa"mh.zitto anakiri kuwa aliambiwa na wananchi kule kigoma kuwa hatukuchagui kwa sababu ni muislam! Hivi ni kweli? Na je mgombea wa ccm ni mkristo? Cuf ni mkristo? Na mbona akachaguliwa yeye?!! Nilitegemea sana kuwa angelijitokeza na kumkanusha hamad rashid juu ya tuhuma alizowatwika wakristo wa kigoma. Hajafanya hilo na yeye anaimba wimbo huo kama mheshimiwa rais kuwa wakristo wamemuumiza!! Hamad rashid amedokeza pale moven pick kuwa kuna mheshimiwa mmoja ilimbidi asiweke hadharani uislamu wake ili achaguliwe!!!! Nasikitika hakuwapa hadira yake jina la mh.huyo kama alimvyomfanyia zito???

  Nimejifunza kuwa wanasiasa wanadhani mchezo wa dini ni wa kawaida tu midomoni mwao, wanasahau kilichom cost alhaj mwinyi 93-95 mpaka akajikuta muungano unatishiwa na hoja ya serikali 3 ikapata tija, cuf wanaamini waislamu wanaonewa ktk duru zote nchini na hawataki kuamini kuwa usawa na haki hapa nchini na mara zote hawajajitokeza ktk utetezi wa maslahi ya wakristo!!!!

  Ccm na cdm wanapaswa wacheck na ku balance uwiano wao ktk siasa za nchi.

  Kizazi hiki cha teknohama kina madhara sana kwa vyama hivi viwili aidha + au -
   
 8. Sailor Boy

  Sailor Boy Senior Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :embarrassedzito mbona unataka kui let down CHADEMA? UNATAKA WANA CCEM WAPATE CHA KUSEMA KWAMBA CHADEMA NI MCHANGA 2? BE SERIAZ KA VP NENDA UKO CCM UONE KA UTAWIKA TENA.:embarrassed::whoo:
   
 9. M

  Maka Kassimoto Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zito simwelewi kiasi fulani. Mitazamo na misimamo yake ni shakashaka hivi.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Yangu macho tu!
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna thread moja ililetwa hapa ilikuwa inamzunguzia kwa kiini dhamira za Godfather Edwin Mtei na Chadema lakini kwa bahati mbaya mods waliifutilia mbali. Kwa kifupi mwandishi ameandika kwa kirefu mikakati ya Chadema na kuwagusia waandishi wa habari wawili ambao wapo kwenye mkakati huo pengine kwa kutumiwa bila kujua au kwa malengo maalum na majina yao yalitwajwa kuwa ni Jenerali Ulimwengu na Saed Kubenea. Kwa mikakati yake sishangai kuona Zitto anaandamwa na nani anajua who next? Arfi? Slaa? or Tundu Lissu? Tuombe uhai tuone. Na nitashukuru kama kuna mtu aliwahi kucopy yale maelezo maana mie ninayo in hard copy.
   
 12. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Vituko vya mh. huyu vimezidi. Atakiwa kutubu anayo ajenda gani na ni wakina nani anawatumikia. akikataa kufanya hayo chadema ichukue hatua za haraka kumuhengua vinginevyo uenda akakisambaratisha chama hicho,
   
 13. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Binafsi nimekuwa shabiki wa mheshimiwa zitto zuberi kabwe, mkigoma huyu alinishawishi sana niamini ktk mrengo wa siasa zake ila nilipomuona anamsogelea muungwana kwa mapambio kama john cheyo basi nikahisi hapa hatuna mtu mwenye courage ya kisiasa bali mpenda ummarufu kwa gharama yoyote ile in the name of democrasy. Nasema sasa nimeliamini hili baada ya hamad rashid wa cuf pale moven pick alipojipambanua eti yeye ni mwanasiasa mzoefu mbele ya mbowe!!! Hamad rashid anataka tuamini kuwa zitto ameshinda ubunge kwa kura za waislamu tu!!!! Maana amesema siku ile kuwa"mh.zitto anakiri kuwa aliambiwa na wananchi kule kigoma kuwa hatukuchagui kwa sababu ni muislam! Hivi ni kweli? Na je mgombea wa ccm ni mkristo? Cuf ni mkristo? Na mbona akachaguliwa yeye?!! Nilitegemea sana kuwa angelijitokeza na kumkanusha hamad rashid juu ya tuhuma alizowatwika wakristo wa kigoma. Hajafanya hilo na yeye anaimba wimbo huo kama mheshimiwa rais kuwa wakristo wamemuumiza!! Hamad rashid amedokeza pale moven pick kuwa kuna mheshimiwa mmoja ilimbidi asiweke hadharani uislamu wake ili achaguliwe!!!! Nasikitika hakuwapa hadira yake jina la mh.huyo kama alimvyomfanyia zito???

  Nimejifunza kuwa wanasiasa wanadhani mchezo wa dini ni wa kawaida tu midomoni mwao, wanasahau kilichom cost alhaj mwinyi 93-95 mpaka akajikuta muungano unatishiwa na hoja ya serikali 3 ikapata tija, cuf wanaamini waislamu wanaonewa ktk duru zote nchini na hawataki kuamini kuwa usawa na haki hapa nchini na mara zote hawajajitokeza ktk utetezi wa maslahi ya wakristo!!!!

  Ccm na cdm wanapaswa wacheck na ku balance uwiano wao ktk siasa za nchi.

  Kizazi hiki cha teknohama kina madhara sana kwa vyama hivi viwili aidha + au -
   
 14. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #14
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa wengi ambao hammjui huyu mbunge kijana mtakuwa mnashangaa sana why anakegeuka kegeuka kila mara ila kwa mliokuwepo chuo wakati akisoma na hasa 2001/2002, hamuwezi shangaa sana leo kubadilika badilika kwa kijana huyu, ni mtu anayependa sana sifa binafsi na wala si kwa ajili ya group zima, anapenda kuonekana yeye kama yeye na wala siyo wengine, asipokuwa makini naye pia ataanguka kama mzee wetu mrema na kijana wetu mbatia, bora hata mrema umri umekwenda na si kama anguko la mbatia, so asipokuwa makini hakika 2015 harudi sehemu yeyote ile, kazi kwake, kwani kwetu sisi ni kurekebisha pale palipo na mapungufu yanayooneka
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Atahamia sisiemu tu, ameshashtukia mambo ya CHADEMA (kuwekwa chambo/chachu) ya kisiasa
   
 16. markach

  markach Senior Member

  #16
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zitto inakubidi utulie. Sisi vijana wapenda mageuzi hatufurahi tukiona nyie viongozi wa chama mkianza kukwaruzana, Au labda ndio demokrasia? Please Zitto, ni mapema mno na safari tulio nayo bado ni ndefu, kuwa mvumilivu
   
 17. k

  kibebii Member

  #17
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  politics! politics nononono !
  SIASA NONONO NIMEKOSEA
  SIHASA!
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sina imani na Zitto ata Kidogo
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...another Spin machine against Zitto Kabwe at full Speed!
  Hii dhambi itaendelea kutafuna mmoja baada ya mwingine.

  "Education commences at the mother's knee, and every word spoken within the hearsay of little children tends toward the formation of character"


  THINK!!!!
   
 20. H

  Hamuyu Senior Member

  #20
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Zitto = embe iliyoiva ndani yake wamo pia funza
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...