Zitto aifyatua CCM, ASEMA IMESHINDWA KUONDOA UMASIKINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aifyatua CCM, ASEMA IMESHINDWA KUONDOA UMASIKINI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto ambaye amekitupia lawama Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kupunguza umaskini nchini

  Exuper Kachenje, Dodoma na Leon Bahati

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto ameishambulia CCM kwa kushindwa kuondoa umasikini nchini katika kipindi cha miaka minne iliyopita, licha ya serikali yake kuidhinishiwa bajeti inayoomba kila mwaka.Akichangia hoja ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/11 bungeni jana, alisema haijalenga (bajeti hiyo) katika shughuli za maendeleo, badala yake imejikita zaidi katika kuwashibisha watu wenye uwezo na kuzidi kuangamiza walalahoi.

  "Hii ni bajeti mbaya. Ni kwa ajili ya tumbo. Ina faida zaidi kwa wenye uwezo," alisema Zitto.


  Alisema kutokana na ubaya wa bajeti hiyo, watakaoumia zaidi ni walalahoi wanaofikia 13 milioni nchini ambao wanaishi kwa dola moja ya Marekani (Sh 1,400) kwa siku.


  "Ni bajeti ambayo ina faida zaidi kwa wenye uwezo," alisema Zitto akichambua kuwa imeshindwa kujitosheleza kutokana na mapato ya ndani.


  Ili kuendesha nchi kwa bajeti hiyo, Zitto alisema: "Itabidi serikali ikope kwa wahisani kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi, kulipa posho na kununua mafuta kwa ajili ya magari".


  Akionekana kuwa makini na aliyepangilia hoja zake zilizotiwa na nguvu ya takwimu, Zitto alikigeukia CCM na kusema chama hicho kinapaswa kubeba lawama zote kwa sababu kimeshindwa kutekeleza ahadi zake kulingana na Ilani yake ya mwaka 2005.


  Kuhusu Chuo Kikuu Dodoma Zitto alidai; "Hilo halipo katika ahadi za CCM, kama yupo mbunge wa CCM asimame aje aonyeshe ni wapi Ilani ya CCM ilipotoa ahadi itajenga Udom, hakuna, hakuna, ‘nachallenge'; kama yupo anayeweza kuonysha aje. Ujenzi wa Udom ni wazo na ahadi ya Chadema ya mwaka 1992".

  Maneno hayo yaliyomwinua Mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongella (CCM) na kuombna mwongozo wa Spika.

  "Mwongozo wa Spika. Hivi ni utaratibu mzuri kuwaambia Watanzania kupitia Bunge kwamba, CCM ilidanganya", alihoji Mongella baada ya kumyamazisha Zitto kwa kuomba mwongozo wa Spika.


  Hoja ya Mongella iliungwa mkono na Naibu Spika, Anna Makinda aliyeongoza kikao hicho jana asubuhi.


  "Upo sahihi Mheshimiwa Mongella, lakinin lazima tukubali kuwa katika wakati huu, ndio wakati hayo yatatokea tu", alisema Makinda.


  Akichangia hotuba hiyo, Zitto alitumia maneno makali akisema bajeti hiyo ni sawa na barua ndefu ya CCM kutaka kujinyonga kwa kuwa ni ya kuchumia tumbo.


  " Toka serikali iingie madarakani kwa miaka minne iliyopita Bunge limeidhinisha zaidi ya Sh26trilioni kama bajeti, kutoka 2006/2007 mpaka mwaka 2009/2010. Leo na mpaka Jumatatu tunajadili, na kwa wingi wa wabunge wa CCM kwa vyovyote vile watapewa cheki nyingine ya Sh11trilioni pia.


  "Kwa ujumla katika miaka mitano, tutakuwa tumewapa jumla ya Sh37trilioni kwa ajili ya kuleta maendeleo, laikini katika miaka minne iliyopita jumla ya Watanzania 1.6 milioni wamekuwa maskini", alisema Zitto.


  Aliongeza kuwa hadi wakati huu idadi ya watu maskini nchini imefikia 13milioni ambao wanaoishi chini ya dila moja kwa siku, lakini bajeti hiyo ikikaa kimya bila kueleza jinsi itakavyowaondoa katika kadhia hiyo.


  Alisema bajeti hiyo inatoa faida zaidi kwa watu wenye uwezo ikiwaacha maskini bila ufumbuzi na kwamba, matumizi ya ndani yana pengo la Sh1.8 trilioni, hivyo katika kila Sh100 inayotumiwa, serikali inakopa kiasi cha Sh23.

  Akichangia bajeti hiyo, DkMongella aliwatuhumu wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya kuwa kikwazo cha maendeleo kwa kukosa ubunifu.

  Alifafanua: "Kupitia Mkukuta (Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania) unaonyesha kwamba utapunguza umasikini nchini kwa kati ya asilimia nane hadi kumi."

  Akichangia hotuba hiyo Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga aligusia zaidi sekta ya miundombinu hasa bandari na reli akisema kuwa ipo haja kwa serikali kuchukua hatua za haraka kuliponyesha Shirika la Reli nchini (TRL), alilosema ni sawa na mgonjwa aliyelazwa katika chumba cha wangongwa mahututi.

  "Bandari zikitumika vizuri zitainua uchumi, tatizo miundombinu yetu, reli, TRL ni gonjwa, lipo ICU, ipo haja ya kuliponyesha haraka. Shirika halina injini, mabehewa mabovu, bado halijaanza kazi licha ya kipande cha reli kilichoharibika Kilosa kutengenezwa. Halina fedha hata za kununulia mafuta. Serikali itenge fedha kulinusuru shirika hili". Alisema Kaboyonga.


  Wabunge wengine waliochangia mjadala wa hotuba hiyo ya bajeti hadi jana mchana ni pamoja na, Abdalah Mtutura, Juma Killimbah, Mgana Msindai na Chrisant Mzindakaya aliyesema takwimu za Benki ya Dunia (WB)za mwaka 2007 zinaonyesha kuwa asilimia 89 ya Watanzania ni maskini na kuongeza kuwa wengi wa Watanzania ni wavivu.


  Wengine ni Athuman Janguo na Herbert Mntangi, Khadija Saleh Ngozi ambao walionyesha wasiwasi kuhusu kampuni kubwa za madini kupewa misamaha ya kodi katika mafuta ya kuendeshea mitambo.


  Mjadala huo wa bajeti unaendelea leo na Jumatatu jioni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo atahitimisha kwa kujibu hoja za wabunge.


  Zitto aifyatua CCM, ASEMA IMESHINDWA KUONDOA UMASIKI
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mhh Hichi ni kichwa...kwa kweli....Tungekuwa na watu bungeni wenye udhubutu kama kijana huyu kama 15 hivi.Wanao ongea kwa takwimu na bila kuogopa...wakiwa na ushahidi ohh tungekuwa mbali..
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  It is true hawa jamaa wameshindwa kabisa..Zitto mwendo huo huo hakuna kuwaonea huruma.
   
 4. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera zito kwa ujasiri huo ulioonyesha....mimi naamini hukuwa unafanya kampeni kama Mongela alivyotaka kutuonyesha.

  Hivi Mongella atagombea tena ukerewe? jamani toka nipo mduchu mongela...nimeingia shule ya msingi mongela...sekondari mongela...chuo mongela...sasa nina watoto mongela..mmmh hebu wanasiasa wawekewe ukomo...kisha mrithisha mwanae siasa bado hajaridhika tu?!! aaaah apumzike bwana awaache vijana kina Zito wajenge taifa.....wana forum chukueni fomu za ubunge jamani tuongeze nguvu bungeni.

  Mix with yours
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  mongela si ndio mwizi mkubwa

  zito ni kifaa bana
  ccm ni genge la wezi na majizi makubwa
   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Safi kaka, kaza buti, tutafilka tuu.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi Getrude Mongela zile kondomu walizokwenda nazo Beijing alisha zitolea maelezo? Halafu kaiba fedha ktk bunge la afrika mbona hakushitakiwa?
   
 8. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Mongella nae si aliiba hela za PAP..lol. Campaign or not.. Zitto spits the truth..word is born.
   
 9. mpuuzi

  mpuuzi Member

  #9
  Jun 12, 2010
  Joined: May 29, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado mnaimani na Zitto....Subirini mwone!
   
 10. A

  Alpha JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  This is News?

  CCM has been in charge since independence. They've had more than 40 years to realize their vision for a better Tanzania for all and they have failed miserably. The truth of the matter is the last idea they had was Ujamaa which was a disaster. Since then it's been nothing but incompetence and corruption. Yet they keep getting elected over and over again.

  While i'm not a big fan of the opposition it's about time Tanzanians took that risk and gave them a chance. playing it safe with CCM has taken us nowhere.
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,524
  Likes Received: 1,693
  Trophy Points: 280


  Mchango wa Zitto Kabwe katika Bajeti ya Serikali 2010/2011


  Dodoma, 11/6/2010.


  Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Bajeti, hotuba ya mwisho ya bajeti kwa Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi katika kipindi chake cha miaka 5 toka wameingia madarakani. Toka Serikali hii imeingia madarakani kwa miaka 4 iliyopita Bunge limeidhinisha zaidi ya shilingi trilioni 26 kama bajeti, [2006/2007 Tshs 4tr, 2007/2008 Tshs 6tr, 2008/2009 Tshs 7tr na 2009/2010 Tshs 9tr] toka mwaka 2006/2007 mpaka mwaka 2009/2010. Leo na mpaka Jumatatu tunajadili na kwa wingi wa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi humu kwa vyotevyote vile watatoa hundi nyingine ya shilingi trilioni 11. Kwa hiyo jumla katika miaka 5 tutakuwa tumewapa [serikali] jumla ya shilingi trilioni 37 kwa ajili ya kuweza kuleta maendeleo katika Taifa letu.

  Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika kipindi cha miaka 4 iliyopita jumla ya Watanzania milioni 1.9 wamekuwa maskini zaidi na kuongeza idadi ya watu maskini mpaka kufikia watu milioni 13. Kwa hiyo tunapojadili bajeti hii tunazungumza bajeti ambayo tuna Watanzania zaidi ya milioni 13 ambao wanaishi chini ya Dola moja kwa siku na bajeti hii haijibu matarajio yao. Bajeti hii haielezi ni jinsi gani Watanzania hawa wataweza kushiriki katika uchumi na kukua na kuondoka katika wimbi la umaskini.

  Bajeti hii ni the longest suicide letter ambayo Chama cha Mapinduzi imejiandikia mbele ya wananchi. Kwa sababu ni bajeti ambayo inatoa faida zaidi kwa watu ambao tayari wana uwezo [rich people] na haielezi jinsi ya kuondoa changamoto kwa watu ambao ni maskini [impoverished people] zaidi ya milioni 13.

  Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa aliyetoka kuzungumza hivi sasa [mheshimiwa Mzindakaya] alizungumza kuhusiana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.
  Mwaka 2005 Chama cha Mapinduzi kiliwaahidi Watanzania kwamba watahakikisha kwenye ilani yao sekta ya kilimo inakua kwa asilimia 20 [!]. Kwa mujibu wa MKUKUTA wa kwanza ambao tunaumaliza sasa ilitakiwa sekta ya kilimo ikue kwa asilimia kati ya 8 mpaka 10 ili kuweza kuwaondoa nusu ya Watanzania kwenye umaskini [wa kutupwa].
  Kwa masikitiko makubwa kwa taarifa ya hali ya uchumi ambayo Waziri wa Fedha ameisoma jana sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 3.2 tu mwaka 2009 [ukiweka na wastani wa ukuaji wa idadi ya watu pamoja na madhara ya mfumuko wa bei ukuaji huu ni hasi (negative growth)].
  Katika kipindi cha miaka 5 toka Serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani sekta ya kilimo imekua kwa wastani wa asilimia 4 peke yake. Mmeshindwa hata kufikia nusu ya malengo yenu ya ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mmeshindwa hata kufikia nusu ya ahadi kwa mujibu wa MKUKUTA. Hii ni aibu kubwa sana na tumewapa jumla ya shilingi trilioni 26 kwa miaka 4 iliyopita na mmeshidwa kukuza kilimo angalau kufikia nusu ya mambo ambayo nyinyi mlikuwa mmeyatarajia.(Makofi)

  Faida kama za Dodoma University, nilikuwa naomba nitoe challenge. Kwa Mbunge yoyote wa Chama cha Mapinduzi asimame na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi aonyeshe ni wapi Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imesema itajenga Chuo Kikuu Dodoma?
  Yeyote miongoni mwenu asimame nam-challenge, hakuna. Mtu yeyote asimame na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi aseme Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi iliahidi University of Dodoma, hakuna. Kwa hiyo hamuwezi kufaidika na kutaka kujisifu kwa vitu ambavyo wala hamkuwaambia wananchi. UDOM wazo la ujenzi na kugeuza Dodoma kuwa University City ni wazo ambalo lilitolewa na CHADEMA toka mwaka 1992. Huo ndio ukweli.

  Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Fedha ametusomea bajeti ya mapato ya ndani kuongezeka kwa zaidi ya shilingi trilioni moja (Domestic Revenue). Tofauti kati ya Recurrent Budget [Bajeti ya kawaida] peke yake kwa mujibu wa takwimu ambazo amezisoma Waziri wa Fedha zinaonyesha kwamba asilimia 23 ya Recurrent Budget ita-financi-wa [itagharamiwa] kutokana na mikopo na misaada kutoka nje. Recurrent yaani Mishahara, Mafuta jumla ya shilingi trilioni 1.8 ni a black hole kwenye Recurrent Budget.
  Huko nyuma tulifikia wakati ambapo (Domestic Revenue) au fedha za ndani ziliweza kuendesha matumizi ya kawaida. Sasa hivi tunakwenda katika hali ambayo fedha za ndani hazitoshi kuendesha matumizi ya kawaida. Hii ni hali mbaya sana.

  Mheshimiwa Naibu Spika, yaani katika kila shilingi 100 tunaitumia katika matumizi ya kawaida shilingi 23 inabidi twende tukakope, tunakopa kulipa mishahara, tunakopa kulipa posho, tunakopa kununua mafuta ya magari yetu, hii ni nchi ya namna gani?

  Kama alivyosema Waziri Kivuli wa Fedha na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Fedha na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni [Hamad Rashid Mohammed] bajeti hii ni moja ya bajeti mbaya kuliko zote katika historia ya nchi yetu. Kwa sababu ni bajeti ya kuchumia tumbo, ni bajeti ya chote tunachokikusanya tunakila hatuendelei na bado tunabakia na gap ya kwenda kutafuta na kwenda kukopa na misaada kwa ajili ya kula na sio kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa sababu asilimia 65 ya bajeti ya maendeleo bado inategemea wafadhili na ukichukua recurrent na development budget asilimia 44 ya bajeti yetu na sio 33 kama Waziri alivyosema bajeti bado tunategemea wafadhili.
  [Bajeti ya matumizi ya kawaida ina nakisi ya Tshs 1.8tr ambayo itazibwa na misaada ya wafadhili na mikopo kutoka ndani na nje. Inasemekana mwaka huu Serikali itafanya Deficit Financing (PRINTING MONEY!!!) ya thamani ya takribani 350bn. Katika Bajeti ya Maendeleo kuna nakisi ya Tsh 2.4tr ambayo ni sawa na asilimia 65 ya Bajeti ya Maendeleo na itazibwa na misaada na mikopo kutoka ndani na nje ya nchi].

  Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima Serikali ikubali sio sifa kuwa na bajeti kubwa sana. Kwa sababu bajeti hii inapelekea kwa mfano kodi ambazo zitaongezeka kwa ajili ya kuziba kuongeza mwanya wa makusanyo shilingi bilioni 300 zinatoka Large Tax Payers Department. [ Kodi mpya zinazopendekezwa kukusanywa za jumla ya shilingi 1tr, 300bn zitatoka kwa walipa kodi wakubwa, 300bn kodi za biashara ya kimtaifa ie trade taxes na 110bn kutokana na PAYE. Shilingi 300bn nyingine zitatoka ‘non-tax revenue ambapo 153bn ni mrahaba wa Madini]. Kwa Shilingi biloni 300 zitakazotoka trade taxes na hali ya uchumi sio nzuri kiasi hicho [itabidi tutegemee importation]. Maana yake ni kwamba tunategemea watu wa import zaidi ili tuweze kukusanya zaidi. Ni hali ambayo sio nzuri ni hali ambayo inaweza kuleta matatizo zaidi katika uchumi wa Taifa letu. [kwa kodi kutoka walipaji wakubwa na PAYE makadirio yanaweza yasifikiwe maana zitategmea mazingira ya biashara na hasa ukizingatia kuwa Serikali itaenda kukopa katika mabenki na crowding out effect itakosesha private sector mikopo na hata kupunguza uzalishaji na kupunguza ajira].

  [mapendekezo ya kutatua changamoto hizi ni pamoja na kupunguza matumizi ya kawaida kwa kiasi kikubwa ikiwemo kupunguza sana posho zikiwemo posho kwa Wabunge na viongozi wa Serikali na matumizi makubwa ya mafuta ya magari (fuel bill). Pili, badala ya kukopa katika Benki za Biashara Serikali itoe Infrastructure Bond kwa ajili ya kupata fedha za kutengeneza mfumo wa usafirishaji umeme, kuimarisha gridi ya Taifa na kujenga Gridi mpya ya Kaskazini Magharibi. Tatu, Uzalishaji wa Umeme (power generation) ufanywe na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama ambavyo wameelekezwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Nne, Serikali iuze 25% ya hisa zake katika Kampuni ya simu ya Zain Tanzania kupitia IPO. Uuzwaji wa sehemu ya hisa za serikali katika Benki ya NBC bado haupo wazi kwani mapato ambayo serikali inasema itapata ni kidogo mno kulingana thamani ya Benki hiyo (serikali ina hisa 30% na wanasema watapata Tshs 30bn. Serikali ikiuza asilimia 20 ya hisa NBC kwa njia ya IPO itapata zaidi ya Tshs 100bn). Tano, EuroBond ilete mapato yatakayotumika kujenga Barabara na Reli peke yake ili kupata manufaa ya mkopo huu ambao utakuwa ghali sana].

  Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Fedha amezungumza kuhusu kuuzwa kwa hisa za NBC na Serikali kupata zaidi ya shilingi bilioni 30. Lakini nimeangalia kitabu namba moja Revenue Book hiyo source of revenue haimo. Kwa hiyo nilikuwa naomba Waziri wa Fedha aweze kutoa ufafanuzi ? [Kila shilingi inayotarajiwa kukusanywa na Serikali ni lazima ionyeshwe katika Kitabu Na 1 cha Mapato ya Serikali. Tshs 30bn zimetajwa katika Hotuba ya Bajeti lakini haimo katika kitabu hicho.....!!!!].

  Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu na la mwisho kwa sababu ya muda. Waziri wa Fedha jana alizungumza kurejesha misamaha ya kodi ya mafuta kwa Kampuni za Madini. Madhara ya uamuzi ambao umeufanya ambao ni kwamba tunarudi nyuma, ile goodwill ambayo tumeitengeneza kwenye Sheria Mpya ya Madini tunaiua. Naelewa kwamba Serikali inaogopa kushtakiwa kwa sababu watu wamesaini zile MDA[mineral development agreements]. Lakini kuna namna za kuhakikisha kwamba sekta ya madini inafungamanishwa na sekta nyingine za uchumi.
  Ukiruhusu Makampuni ya Madini yaagize mafuta kuzalisha umeme wao bila kulipa kodi maana yake ni kwamba hawatanunua umeme kutoka TANESCO. Sasa hivi kuna kazi ambayo imefanyika tayari Wizara ya Nishati na Madini. Migodi yote isipokuwa mmoja sasa unaweza kupata umeme kutoka TANESCO. Lakini kwa kuwaruhusu kuagiza mafuta ya kuzalisha umeme wao wenyewe tunaingia kwenye tatizo la fungamanisho kati ya sekta ya madini na sekta ya umeme. [Migodi hutumia takribani asilimia 13 ya gharama zake za uzalishaji katika Umeme]

  [Vile vile, Kwa kuwa msamaha huu hautahusisha wakandarasi wa ndani wanaofanya biashara na Kampuni za Madini (local contractors), hivyo hapatakuwa na vivutio kwa kampuni za madini kutumia wakandarasi wa ndani. Kampuni za madini zitaona ni rahisi zaidi (less costly) kufanya shughuli ya kuchimba wenyewe (owner mining). Hii inaua (kills) dhana ya fungamanisho kati ya sekta ya madini na sekta ya ujenzi (construction sector) ambayo ilikuwa ni dhumuni mojawapo la Sheria mpya ya madini ili kujibu changamoto ya fungamanisho dogo la sekta ya Madini na sekta nyingine za Uchumi (low integration of the mining sector to other sectors of the economy). Katika muundo wa gharama za uzalishaji kwa Kampuni za madini, takribani asilimia 30 ni gharama za kuchimba].

  [Napendekeza kama ifuatavyo]

  Kuhusu Umeme; Sheria ya fedha iseme wazi kuwa mara baada ya migodi yote kupata Umeme kutoka TANESCO, msamaha wa mafuta utakwisha.

  Kuhusu Makandarasi wa ndani;
  Ama (a) Msamaha huu uendelezwe mpaka kwa kampuni za ujenzi katika migodi (local contractors [worst case scenario].

  Au (b) Katika Finance Bill, kuanzishwe (introduce) 15% withholding tax on technical services kwa kampuni za madini zitakazofanya "owner mining" (second best case scenario).

  Kwa kuwa local contractors wamatozwa 5% withholding tax on technical services, itakuwa ni rahisi (cheap) kwa kampuni za madini kutoa zabuni (tender) kwa kampuni za ndani. Hata hivyo pendekezo hili litaathiriwa na MDAs zilizopo.
  Kwa hiyo kuna haja ya kuwa na measures maalum ya ku-mitigate huo uamuzi ambao Serikali imeufanya [kurejesha msamaha wa kodi ya mafuta kwa kampuni za madini] na kwa vyovyote vile si uamuzi sahihi na uamuzi ambao haukufikiriwa vizuri.

  Mheshimiwa Naibu Spika, siungi Bajeti mkono.


  Mzitto
   

  Attached Files:

 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  A bunch of jokers wananyoosheana vidole kana kwamba miongoni mwao kuna mwenye muarobaini wa matatizo ya mtz.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama mama mwanae nae bure tu. Mlinzi wa mafisadi wa nchi hii. Kaingia serikalini kwa njia zile zile wanazoingizana watawala wetu. tu huyu eti mkuu wa wilaya. Si wampeleke kwao ukelewe kuliko kumuacha Kigoma? hamna lolote la maana pale!
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mh.Zitto,
  Mkuu shukran sana kwa mawazo yaliyotulia..Utachukiwa na wengi lakini inapofikia ktk maswala kama haya siku zote wewe husimama pekee..
  - Tuwasiliane...
   
 15. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mama Mongela anaweza kuwa na mapungufu mengi lakini hili la kusimamam wakati Zitto anaongea ni strategy ya kawaida ya CCM kumdistract na kujaribu kupunguza makali ya michango yake. Nashukuru kuona kuwa Zitto ameweza kulizoea hilo hivyo limekuwa halina athari katika mtiririko wa mchango wake kama ilivyojionyesha juzi. So ndgu zangu dont take it personal to Mama Mongela. Kama aisngefanya yeye angefanya mwengine. Ni mbinu ya kawaida ya kibunge ambayo hata CHADEMA nao kama wangekuwa wanaogopa mchango wa mwanCCM fulani basi wangeweza, na wakati mwengine hujaribu lakini ofcourse, CCM wana refaree upande wao. Ndio vimbwanga vya chama tawala hivyo....

  omarilyas
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  CCM hawana jipya - Yataka moyo mkuu kusimama na kukisemea chama hiki kilichokwisha ki fikra, chama kisichobuni mbinu mpya za kuwakomboa watu maskini hakitufai, akina mama wakongwe kama kina mongella unategemea watakuja na chachu mpya ya maendeleo na kupigania umaskini unaokithiri?. Mwendo mdundo Zitto.

  Najua ukweli alioutoa Zitto utawauma sana - Ningekuwa ni mbunge wa CCM ningejiuliza mara mbili mbili kabla ya kuchukua form kurudi tena jimboni kwangu eti kuomba ridhaa ya uwakilishi.

  Nimependa pale Zitto ameiita bajeti hii kama barua ndefu ya CCM kwetu sisi wananchi - Hongera Sana Mkuu kuthubutu kusema Ukweli - ninyi ndio vijana wenye uchungu na mtakaoikomboa Tanganyika Yetu, inayomogoka kila siku.
   
 17. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yes point nzuri omary....I agree with you ila kuna aina za watu ambao daima hupenda kuomba mwongozo katika hoja kama hizi.
  I mean kuna wabunge makini wa ccm ambao wakiona ukweli kama huu wanaamini ni ukweli na kamwe hawaombi mwongozo wa spika ili waharibu hoja.....lakini pia kuna wabunge aina ya kina mongela wao chama ni zaidi kuliko lolote kila mara hoja moto wao hupenda mwongozo ili baadae wakapongezwe kilimani.....ni watu wa matumbo yao zaidi...inauma unapoona wamekaa kwenye system muda mrefu....ukute mpango wa kuondoka hawana kazi yao ni kuomba muongozo wa spika...akapumzike


  Mix with yours
   
 18. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Inavutia kuona pale mbunge anapotafuta muda kufanya utafiti wake na kuandika kitu ambacho pamoja na kwamba hakijakamilika ila jitihada na nia njema zaonekana. Zitto may be many things but regardless of what you think of him by god that was a well constructed speech uncommon with the nauseatingly sycophantic political parlance used in our parliament.
   
 19. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Zitto hapo upongezwe.
  Wabunge wa upinzani hufanya kazi yao, naamini husoma kwa makini sana kabla ya kuchangia.

  Huko CCM wengi ni kuropoka (ndivyo nionavyo) tu! Hawasomi kabisa kabisa na wakikosa makofi huamua kusifia serikali ya CCM na hapo hupewa makofi kidogo.

  Mongella nilikutana naye mitaani akishindwa hata kushuka kwenye gari (overweight + age) kwa udhaifu huo hawezi kuwa alishaisoma bajeti ya nchi kabla ya hapo. Na ni mtindo huo huo naamini anataka arudi Bungeni.

  Jamani! Huko Ukerewe vipi? Mbona muna sifa ya kwenda shule kuliko wilaya yoyote nchini? Soooo many professors! Jitokezeni kikongwe apumzike. Au atatuma wachoma visu?

  Hogera Zitto.
   
Loading...