Zitto afunga mjadala kuhusu yeye kugombea urais

Zitto afunga mjadala kuhusu yeye kugombea urais

Sasa bro Kabwe CCM watazungumza nini mana walikuwa wakikutumia kuchafua chama chako cha CHADEMA?Anyway bigup kwa kauli hiyo na endelea kujenga chama chako
 
Huu mwaka ndio bado mchanga kama ameanza hivi (kwa style nzuri inayoonyesha kukomaa kifikra) ni dhahiri mapambano kuelekea ukombozi yatakuwa swafi.
Lakini huyu Zitto siku moja akiwa Jimboni kwake mwaka 2010 kwenye kampeni aliwahi kuwaambia wapiga kura wake kwamba wampigie Kura za Ubunge mwaka 2010 na mwaka 2015 wampigie kura za Urais.

Na mimi nilikuwepo amesahau au amewahi kufuta kauli hiyo?
 
mwaka upo salama kabisa tena unamakubwa sana huu mwaka.Muda si mrefu watanzania watashuhudia maajuabu kwa kile wanachokitegemea kuwa ni salama kumbe kijiwe cha machinjio
Unaongea kimafumbo sana ,fafanua maana kila kitu siku hizi kipo wazi ndio maana kamanda Zitto ameweka wazi.
 
zittophobiasis wataishia kutoa povuuuu

Kwataarifa yako wewe ni mmojawapo wa wanaomuharibia sana Mh.Zitto kisiasa. Kama mwenzio ameamua kubadilika kwa dhati, nawewe jaribu kubadilika ama kukaa kumya.
 
Babu anatamani watu wenye kichuguu kama wewe hahahha!!!Pole sana naona zitto kakuzima unahaha na mm.

wewe ni mmoja kati ya wachumia tumbo mnayeharibu reputation ya Zitto kwa siasa za kitoto mkidhani mnamuongezea credibility kumbe mnamuharibia kabisa.
Sidhani kama uyo Zitto anafurahia hichi unachokifanya wewe na wenzako wote.
 
Last edited by a moderator:
Lakini huyu zitto siku moja akiwa Jimboni kwake mwaka 2010 kwenye kampeni aliwahi kuwaambia wapiga kura wake kwamba wampigie Kura za Ubunge mwaka 2010 na mwaka 2015 wampigie kura za Urais.Na mimi nilikuwepo amesahau au amewahi kufuta kauli hiyo?
Historia ina tabia ya kuwahukumu watu ,ila kwa wanafalsafa wanaamini kuwa ni vyema kuikumbuka historia na kujirudi kuliko kuikwepa historia ije ikuhukumu. Hapa ni step 1 kwa jemedari Zitto.Let us hope for the best.
 
Ee mwenyenzi MUngu parua vizuri mti wangu wa CDM ili ukachanue vizuri ukiwa umekua juuu
 
Vuka mto ukiufikia,hii ni kauli lowasa alipoulizwa endapo atagombea urais.
Zito najua umetafakari kwa kina na umegundua kuwa urais ni mchakato ambao unaanza ndani ya chama.
 
zittophobiasis wataishia kutoa povuuuu
Unajuwa wewe ni mjinga!! na nitakueleza ujinga wako ni nini, Zitto anawatumia kama Condom lakini alipoona mission yenu imefeshindwa yeye anarudi kwenye mstari anawaacha wajinga kama wewe muendelee kuumbuka na hatimaye mfutwe uanachama.

Hebu Msome Samson Mwigamba hapa.


Samson Mwigamba Mwampamba, I'm your friend and you know it. Mimi huwa si mnafiki. Nachukua fursa hii kushauri kwamba hiyo vita unayopigana lazima iwe na mipaka. Hata ungemchukiaje, Mbowe is still our party national chairman and some how the symbol of the party. Jaribu kuwa na heshima kidogo, si vizuri kupambana na viongozi kwenye mitandao. I did the same to Mamuya. Nilimwambia hata mkimuuliza leo. Sikubaliani na kitendo cha yeye kuja kwenye mitandao na kumtaja Naibu Katibu mkuu wa chama kwamba ni msaliti. Kama ana ushahidi angeupeleka kwenye vikao. Nilimwambia kama mwenyekiti wake wa mkoa kwamba hatafika mbali kwa staili hiyo. Na ningekuwa na uwezo leo ningefuta uanachama Mamuya, Ben Sanane, wewe, Gwakisa, and everybody anayefanya vita vya kichama kwenye mitandao. This is unacceptable. Wewe unajua nimeumizwa sana pale makao makuu huenda kuliko wewe. Kama wewe ulizuiwa kugombea mimi niliharibiwa maisha yangu na familia yangu. Mpaka leo sina kazi miezi minane sasa naishi kwa kuomba omba. But sijawahi kuingia kwenye mitandao na kumtukana kiongozi aliyenitenda. Huo ndo utu uzima Mwampamba. My young brothers, kuna maisha beyond uenyekiti wa BAVICHA taifa. Why are you driven mad to such extent. Kama mlionewa Mngetulia na kujipanga upya mkawa mnajieleza ndani kwa vijana ndani ya chama i'm sure next time mngepata hata kura za sympathy. Lakini hii vita yenu nilishawaambia msidhani mnamuumiza Slaa ama Mbowe bali mnatuumiza hata sisi kwa maana ya kuharibu chama. Mwisho wa siku mtafutwa uanachama na ndiyo itakuwa end of your story in CHADEMA. It's just a piece of advice from your dear brother. Mnaweza kuuchukua ama kuupuzia lakini msianzishe tena vita na mimi. Time will tell my young brothers!!!
 
Babu anatamani watu wenye kichuguu kama wewe hahahha!!!Pole sana naona zitto kakuzima unahaha na mm.
Kachukue Posho yako Lumumba.Ila tumeshakufahamu na huna muda mrefu utapotea na CDM yetu inazidi kuwa Juu.Mchumia Tumbo sasa Ben Saa Nane kashakuruka sijui Chakula na Vinywaji atawalipia nani wewe na Juliana.Polee yako.:majani7:
 
atoe kauli majina anataja au hataji.
urais atausikia redioni mtu wa kutuzungusha mara hili lile ikulu mahali patakatifu
Pia atoe kauli kuhusu panya wasio na hatia watakufa au wataishi.
Vile umasalia amevuka nao mwaka au vp
 
Kwa mimi binafsi simwamini sana huyu zito ila kama atakubali afungwe camera /cctv ili tuwe tunamuona anachofanya kwani hatabiriki na ni ndumilakuwili
 
Mi nikajua katoa kauli kuwa hatagombea!!!
kumbe kauli yenyewe hataongelea mambo ya uraisi....
Na tunamsifia kabisa...nonsense!!!!!
 
Hakuna ambaye anamchukia Zitto bila sababu, ila tatizo ni matendo yake ila naona Zitto kaanza kukomaa.

Pongezi kwako broda ila hatutafumba macho kwako.
Mungu akulinde Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Akitoa ufafanuzi kwenye page yake ya FB muda mfupi uliopiita Zitto ameweka wazi sasa amefunga mjadala kuhusu kugombea urais 2015

275673_100000321189166_1444157301_q.jpg
Zitto Kabwe

¨Ngoja niweke wazi kabisa. Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya kauli za wanachama waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala hilo. Jibu langu kwa wote wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba 'katika moja ya maazimio yangu ya mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa suala la Urais 2015. Hivyo sitaongelea suala hili. Sitasema kitu kuhusu suala hili mpaka baada ya Katiba mpya kupatikana na chama changu kuweka utaratibu na mchakato wake¨



Coongrats Zitto

hii ni kauli ambayo naitafakari kwa undani sana mimi
 
Back
Top Bottom