Zitto aanza ziara mikoa ya Pwani na Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aanza ziara mikoa ya Pwani na Kusini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 20, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ametinga wilayani Kibaha kuwaomba wananchi kumuongezea nguvu bungeni kwa kuwachagua wabunge wengi kadri iwezekanavyo wa kambi ya upinzani ili kwa pamoja waweze kwenda kuibana serikali ili iweke mazingira mazuri ya maisha wa Watanzania.

  Mgombea huyo wa ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini aliueleza umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa chama hicho kuwa katika kipindi hiki anahitaji wasaidizi wengi bungeni ili kila mmoja kwa nafasi yake akatetee maisha ya wananchi ambao wengi wao ni masikini na kwamba akiachwa yeye peke yake, atachelewa kukamilisha dhamira yake ya kuhakikisha kila mtu anakuwa na maisha bora.

  Zitto alitoa ombi hilo juzi kwenye viwanja vya Mwendapole wakati wa mkutano wa kampeni wa Chadema. Zitto, mmoja wa wabunge waliojipatia umaarufu kutokana na uwezo wa kujenga hoja na kuibana serikali, alisema amelazimika kusafiri kutoka Kigoma kwa ajili ya kuwaomba wananchi wamuongezee nguvu bungeni.

  "Ndugu zangu wa mkoa wa Pwani, hakuna asiyefahamu (kashfa ya zabuni ya ufuaji umeme wa dharura iliyokwenda kwa kampuni ya) Richmond na (wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje) EPA," alisema Zitto.

  "Haya mmeyajua baada ya kazi nzuri iliyofanywa na wawakilishi wenu ambao ni wabunge kutoka kambi ya upinzani, bila hao msingesikia na wala msingejua na mngeendelea kutafuniwa fedha zenu za kodi ambazo kwa sasa zingesaidia kuinua maisha yenu.

  "Hivyo, ili tuweze kuibua mengine, maana ninaamini yapo mengi tu, mniongezee nguvu kwa kunipa wabunge wengi kadri iwezekanavyo hapo Oktoba ili kwa pamoja tukafanye kazi ambayo muda si mrefu mtaona manufaa yake."

  Kiongozi huyo alisema miaka 50 ambayo serikali iliyopo madarakani imekaa imetosha kabisa kuthibitisha kuwa imeshindwa kutimiza matakwa ya watu wake na hivyo sasa ni kipindi cha mapinduzi na kuwataka wananchi wakiweke chama kingine chenye dhamira ya kuinua maisha ya watu wake, ambacho alikitaja kuwa ni Chadema.

  Monday, September 20, 2010

  Mgombea ubunge jimbo la kibaha mjini.  [​IMG]
  Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,kwa chama cha CHADEMA,Mh Zitto Kabwe jana alianza rasmi mzunguko wa nchi nzima kuwasaidia wagombea Ubunge na Udiwani wa CHADEMA katika majimbo na Kata zao.Jana alikuwa mjini Kibaha akimnadi mgombea Ubunge kwa jimbo hilo la Kibaha Mjini ,Bw.Habibu Mchange. ​


  [​IMG]
  Nikimnadi mgombea wetu wa ubunge Kibaha Mjini-HABIBU MCHANGE


  [​IMG]


  [​IMG]
  Wananchi walijitokeza  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]

  [​IMG]  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
  Nikimnadi mgombea udiwani Kata ya Kibaha-Patrick Kinunda​


  [​IMG]
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Dogo anafanya vitu vyenye akili sana
  huwezi kutarajia anakuja na ubunifu huu mzuri
  Zitto we backing you up just tuwakilishe vyema.
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Habari njema sana hizi... Zitto peke yake anatosha kufuta nyayo za mama Salma, Riizi wani na Dk Bilal... Njoo hadi Mbeya kwa Sugu braza Zitto.
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Nafikiri Zitto amepelekwa sehemu zenye vibandiko vingi kama sikosei Mbeya atatinga kamanda mwenyewe.
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Good plan Chadema..Zitto make the most of it..mwaga sumu, washa moto mkali october 31st kielewekeeee...
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huyu nitishio kwa wazee na vijana!
  You have my full support broda!
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jk naona kwa sasa ana hofu ya CCM kushindwa uchaguzi mbaya zaidi kushindwa uku yeye akiwa Mwenyekiti.
  Uchunguzi wa Synovate na vijana wa kazi usalama wa Taifa unatosha kumnyima usingizi.
  Mwendo sasa ni kuchakachua matokeo by any means
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  safi sana Zito.
  Kaitangaze CHADEMA kusini kwani familia ya JK imeipaka matope mno huko.
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kazi nzuri sana hii, ni kweli tunahitaji upinzani kukomaa Bungeni. Pia tunahitaji kiongozi mwenye calibre ya Dr. Slaa!!

  Go Zitto Go...!! Hamasisha wananchi wamchague Dr. Slaa na wabunge wa upinzani!!
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Safi saaana Zitto,

  Go ZITTO
   
 11. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tunakukubali zitto, endelea na kasi hizo. Tunasubiri october 31.
  Kwa sababu hawaoneshi kwenye Luninga, twende kimya kimya tutafika tu.
  Big up mzee
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Zito wa ukwe -e!!

  God Bless you Papii
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  chanja mbuga zitto
  mikakati yenu ni mizuri sana
  tumechoka hawa watu
  ukweli unahitaji makamanda wengi wa kukusaidia
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  NImeipenda startegy yako na chama Mkuu Zitto.
  Mnapita kule walikojihahakikishia ushindi na kuvuruga; hadi keleweke!!

  Go Zitto, Go Slaa....
   
 15. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  go zito gooooooooooooooooooooo
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  CHADEMA all the way......sisi hatutumii familia, tunatumia Vichwa ndani ya chama.
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wananchi walijitokeza  [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] Nikimnadi mgombea udiwani Kata ya Kibaha-Patrick Kinunda


  [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG]
   
 18. K

  King kingo JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hawa wananchi wamekuja wenyewe na wala hawajabebwa kwenye malori..
   
 19. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Good job Zitto
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Shukrani Zitto. Wote tuendelee kuwa support wagombea.
   
Loading...