Zitto aandika barua CHADEMA kuomba msamaha

Status
Not open for further replies.

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,378
Reaction score
139,286
Wakuu kuna tetesi zimenifikia jioni hii toka kwa mtu wa karibu na Mh.Zitto,kuwa aliyekuwa Kamanda kabla ya kupokonywa vyeo,ameandika barua nzito kwnda kwa katibu wake akiomba msamaha.Mtonyaji huyo nikamuuliza kuhusu tetesi kuwa Zitto anajiandaa kufanya mikutano kinyume na zuio la chama,mtonyaji alijibu kifupi ni kipi alichowahi kufanya ZZK kikafika mwisho na kufanikiwa.Mods msituzibe midomo kuhusu ZZK
 
Akifanya hivyo,itakuwa vyema sana. Bado ana nafasi ya kusonga mbele na wenzake chamani

Mzee Tupatupa
 
MM kishazikwa rasmi Mbeya

Ok CHADEMA Kumsamehe MM ni sawa na MaCCM yanayowasamehe mafisadi na magamba

M4C Daima
 
Zitto ameiandikia familia ya Mtei barua ya kuomba msamaha?
 
Kweli Maccm hamuwezi kuzibwa midomo. Mmeona nyota yenu imefifia mnaanza kuiwasha tena. Mnafikiri kuwa CDM tuna shida na mtu? Kwetu Chama kwanza mtu kesho.
ZZK hajanyimwa kuandika barua, aende hata TBCCM akapewe kipindi kule cha kujielezea, hatuna shida naye. Ajiunge upya hatuna shida naye, lakini, hapati ushirika tena humu. Hakuna kiongozi wa kubishana naye. Amemwona Shibuda? Nani anahangaika na ubunge wake? Tupa kuleeee.
ZZK is no longer an issue to us
 
Asamehewe ila awe chini ya uangalizi maalumu.

Hata hivyo,naamini uwepo wa huu uzi hapa jukwaani utategemea na ukweli wa habari yenyewe.
 
huyo ni nyoka kabisa

harudi hivihivi huyo

ngoja amalize ziara yake ya kusafisha kama alivyosema sixgates
 
Akae mbali nina hasira kama mbogo yani kinaona kimesha chemka kinazuga na msamaha Zitto hujaweweseka vizuri mpaka uchizi ukupitie ndio utapata msamaha vp kinana kakupa za uso?ngoja kwanza tumalize PAMOJA Daima ndio tutafikiria kukuzungumzia humu jamvini
 
Last edited by a moderator:
Atuambie kwanza lengo lake lilikuwa nini kutaka kukisaliti chama? alikuwa anafadhiliwa na nani? na kwa malengo gani?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…