Tusimsakame Zitto, Maamuzi ya Waziri kuhusu TANESCO mbali ya kuwa muhimu kuna makosa ya kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusimsakame Zitto, Maamuzi ya Waziri kuhusu TANESCO mbali ya kuwa muhimu kuna makosa ya kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Jul 30, 2012.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna mjadala ambao unaoendelea kuhusu sakata la wabunge kuhusu kupokea rushwa kuhusu sakata la Tanesco lakini katika sakata hili kuna baadhi ya wabunge mafisadi na wala rushwa lakini kuna baadhi wamewekwa kwa kundi hili kwa chuki au kusema ukweli kama Mh.Zitto,ukisoma makala hiyo hapo chini unaweza kuona ni nini Zitto alichokua anakitetea na msimamo wake "ufuataji wa sheria katika maamuzi"

  Waziri na katibu mkuu wa madini hatua yake ya kumfuza Mhando na kuipa tenda kampuni ya BP puma energy kwa harakahara tunaweza kuona ya kua wa kishujaa,lakini tukiutazama katika jicho la kisheria kunaukiukwaji wa sheria hapa zito alichokua anapigania ni ufuataji wa sheria.Kama waziri au kiongozi fulani ataibuka na na kujitolea maamuzi kwa kuvunja sheria zilizopo hata kama kwa faida ya Taifa haimuondolei msamaha kwa kuvunja sheria.

  Je waziri huyohuyo au kiongozi huyohuyo kesho kutwa akija na maamuzi ya kuliujumu taifa kwa kutumia cheo chake tutamdhibiti vipi?

  Inafahamika ya kua kampuni hiyo hiyo ambayo serikali ina hisa asilimia 50% katika tenda nayo pia ilikua na nia ya kuitapeli selikali kwa kutoa bei ya juu ya uuzaji wa mafuta lakini baaada ya kushindwa katika tenda kwa kupia mlango wa nyuma ikaenda na kukubaliana na serikali na kupunguza bei!Kwa manti kampuni hii inapashwa vilevile kuchunguzwa.

  FURAHA YA LEO KUHUSU UAMUZI WA WAZIRI WA MADINI NA NISHATI INAWEZE IKAGEUKA KILIO KESHO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.


  KUMBUKUMBU - Habari ya gazeti la Jamhuri la Julai 24, 2012 iliyoandikwa na Deodatus Balile

  Vita kubwa TANESCO


  Kuna kila dalili kuwa imeibuka vita ya wazi kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), huku Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO aliyesimamishwa kazi, William Mhando, akipigiwa debe la wazi na wabunge.

  Taarifa zilizopatikana kwenye ofisi za Bunge zinasema kuwa Kamati ya Nishati na Madini inajipanga kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO aliyesimamishwa kazi, Injinia Mhando, hatarejeshwa kazini huku wizara ikisisitiza kuwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wala hajafukuzwa.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

  "Unajua kilichopo ni mvutano baina ya Kamati (ya Bunge) na Katibu Mkuu (Maswi). Yeye anasema alikiuka Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa sababu ya uzalendo. Anasema mimi Munde na Sara Msafiri tunafanya biashara ya matairi na TANESCO, ndiyo maana tunaipigia debe TANESCO.

  Aliwaambia waandishi wa habari kuwa tangu alipoteuliwa aliwaambia wazi watumishi wa wizara hiyo kuwa anataka kurejesha heshima ya Serikali ndani ya Wizara ya Nishati na Madini, anataka kuondoa ubadhirifu na la mwisho ni kuwa na uwazi katika kazi zinazofanywa na wizara.

  "Nimewaambia wazi kuwa asiyeyaweza hayo afunge mizigo aondoke," alisema Maswi.

  Mhando adaiwa kuomba msaada wa Simbachawene

  Awali, Katibu Mkuu aliiambia JAMHURI kuwa Mhando alikuwa amepita kwa Naibu Waziri Simbachawene akimtaka amsaidie kumlinda, kwa maelezo kuwa Katibu Mkuu hampendi yeye (Mhando).

  "Mhando alikwenda kwa Naibu Waziri Simbachawene akamwambia anaomba amlinde kwani mimi simpendi. Simbachawene akamwambia Waziri Muhongo, Waziri akamwambia Simbachawene mwambie Katibu Mkuu, akaniambia.

  "Mimi nikamwita. Nikamwambia unasema sikupendi kivipi? Nikamwambia mimi Kama Maswi na wewe kama Mhando tunaweza kuwa marafiki lakini urafiki wetu si wa MD au Katibu Mkuu. Hivi ni vitu viwili tofauti. Nilimwita nikamuuliza mimi nikupende wewe unataka uwe mchumba wangu?

  "Tangu mwanzo niliwaambia wakurugenzi wote msijipendekeze kwangu. Mtu anayetaka kuja kwangu afanye kazi. Mhando akawa hafanyi kazi, anazunguka anatafuta jinsi ya sisi kukubaliana naye tumsaidie. Anatuma watu nimsaidie kufanya kazi, nimsaidie nini? Kufanya kazi ipi?

  "Siku moja nikamwita nikamwambia nikusaidie nini? Mimi nafikiri hunielewi. Nikamwambia wewe ni rafiki yangu kama Mhando na Maswi, lakini kama MD na Katibu Mkuu ni vitu viwili tofauti," alisema Maswi.

  Mhando atuhumiwa kumpa kazi mkewe

  Tuhuma nyingine anazochunguzwa nazo Mhado kwa sasa ni kwamba alimpatia mke wake zabuni ya kuuza stationery kupitia kampuni ya Santa Clara. Kampuni hii imepewa mkataba wa Sh milioni 800 kuiuzia TANESCO.

  Mke wa Mhando sasa anafahamika kama Eva Stephen William wakati zamani alifahamika kama Eva Stephen Mhando.

  Mikataba 23 inachunguzwa, lakini pia mitatu inayofanyiwa kazi mara moja ni ununuzi wa mita za Luku kwa bei mara mbili ya bei halisi, mkataba wa ku-supply stationery na ununuzi wa vifaa vyenye ubora usioridhisha.

  Mboma adaiwa kumpigia debe Mhando

  Wiki ya Juni 17, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Jenerali mstaafu Robert Mboma, anadaiwa alikwenda Dodoma na Mhando wakiwa kwenye gari moja kufanya uzengezi kuhakikisha Mhando anarejeshwa madarakani, lakini inadaiwa aligonga mwam ba. Juhudi za kumpata Jenerali Mboma zimegonga mwamba kwani simu yake inaita bila kupokewa.

  Maswi ahoji nia ya wabunge

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Maswi alihoji inakuwaje wabunge wanamtetea kwa kiwango kikubwa Mhando aliyesimamishwa kazi kwa utaratibu sawa na ilivyotokea kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege, lakini hakuna anayependekeza Ekelege aendelee kuwa kazini wakati uchunguzi ukiendelea?

  "Alikuja kwenye Kamati tarehe 17 Juni may be (labda) akidhani amepata kitu kinaschotaka kugawa wajumbe. Kama wajumbe, mimi nikawaambia wajumbe hawa ikithibitika nafanya biashara na TANESCO niko tayari kujiuzulu hadi ubunge. Hata hivyo, si kosa kufanya biashara isipokuwa unapaswa ku-declare interests (kutangaza mgongano wa kimasilahi).

  "Zedi akamwambia ulitaja majina ya wabunge wanaofanya biashara na TANESCO yeye akasema sikutaja. Mwenyekiti akamwambia Katibu Mkuu ‘nadhani una matatizo'. Sara akasema hafanyi biashara yoyote na TANESCO na akamtaka atoe vithibitisho… Katibu Mkuu akasisitiza kuwa hajawataja hao wabunge," alisema Tambwe.

  Mbunge huyo alisema Serikali inawachanganya, kwani wakati wizara inadai TANESCO wanaiba bilioni 60 kila mwezi, CAG amelipatia shirika hilo hati safi.

  "[Christopher ole] Sendeka akamwambia tatizo lako Maswi unataka ubabe na Sara [Msafiri] akamwambia Katibu ukiwa mchawi utakula watoto wa jirani unamaliza, kisha utakwenda kula wa kwako," alisema Tambwe akiwakariri wabunge hao wakimsihi Maswi aachane na mpango wa kumsimamisha kazi Injinia Mhando.

  Alisema bajeti ya mwaka jana iligomewa Serikali ikasema itawapa hela ya mpango wa dharura Sh bilioni 408, lakini hadi leo TANESCO wananunua umeme bei kubwa kisha wanauza kwa bei ndogo. "Nasema suluhisho ni kununua mitambo ikamilikiwa na TANESCO si kuendelea na utaratibu huu wa kukodisha," alisema.

  Hata hivyo, Tambwe alisema vita yote iliyopo ni kwamba wizara na TANESCO wanagombea kununua mafuta kwani huko ndiko kwenye ulaji.

  Msafiri amsema Maswi

  Mbunge wa Viti Maalum ,Sara Msafiri (CCM), alipoulizwa tuhuma dhidi yake alisema: "Hizo ni mbinu chafu zinazofanywa na Katibu Mkuu Maswi na Waziri wake kuwatisha, kuwaziba midomo na kuwagawa wabunge hasa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini.

  Kwenye kikao Katibu Mkuu wa Wizara alitakiwa kuthibitisha tuhuma hizo, walisema wanayo orodha ya majina ya wabunge wanaofanya biashara, lakini ndani ya Kamati ya Nishati na Madini hakuna yeyote anayefanya biashara na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

  "Aidha, si dhambi kwa Mbunge kufanya biashara, anachotakiwa ni kutangaza ili kuepuka mgongano wa kimasilahi."

  Zitto aitahadharisha Wizara, Waziri Mkuu

  Kwa upende wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, anasema anachopinga ni unyanyasaji dhidi ya watumishi wa umma na si vinginevyo.

  "Sijatangulizwa na mtu kumtetea Mhando, kwani ni wajibu wangu kama Mwenyekiti wa Bunge wa Kamati ya Mashirika ya Umma kuhakikisha kwamba mashirika yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni.

  "Philosophia ya ‘eyes on hands off' ndiyo inayotakiwa itumike. Sitaki micro-management (wizara kuingilia). Na hii si mara ya kwanza. Consolidated Holding nilimwonya [Mustafa] Mkulo kuingilia mashirika alipomsimamisha [Methusela] Mbajo nilihakikisha anarejeshwa kazini.

  "Mimi ni muhanga wa kuonewa. Mtu ambaye hajaonewa ndiye anayeweza asimtetee mtu anayeonewa. Katika suala la TANESCO, Waziri na Katibu Mkuu wako wrong (wamekosea).

  "Sina masilahi TANESCO, sina biashara TANESCO, sijahongwa, naongea kwa uzoefu. Hata Dk. Rashid wakati anashambuliwa nilisimama kumtetea kwa sababu naamini katika ukweli.

  Nimeiambia Kamati kwenye TANESCO ‘they are wrong' (wamekosea). Waziri Mkuu [Mizengo Pinda] nimemwambia action ya TANESCO is wrong. Inawezekana TANESCO kuna uchafu lakini hatua hazichukuliwi kwa njia hii.

  "Nikiwaacha Maswi na Muhongo kufanya haya bila kuhojiwa, itawazuia nini mawaziri wengine kufanya walichokifanya? Nimezungumza nao wote - Waziri Mkuu, Maswi, Muhongo, [George] Simbachawene - nikawaambia mrejesheni ofisini Mhando.

  "Kagasheki aliposimamisha watu waliosababisha faru kuuawa, sikusema kwani alifuata utaratibu. [Dk. Harrison] Mwakyembe alipomsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa ATC nilimuonya Mwakyembe kuwa ‘you are wrong' (umekosea), bahati yule Mkurugenzi Mkuu wa ATC alikuwa hajathibitishwa kazini ndiyo ikamuokoa.

  "Nilimzuia Mwakyembe kumsimamisha Mkuu wa Chuo cha Mabaharia (DMI), nikamwambia ukim-touch (ukimgusa) tutakumaliza. Inawezekana kabisa wanatetea haki lakini kuna taratibu za kufuata.

  "TANESCO walitoa tenda na BP wakabid, Camel Oil wakabid, lakini BP wakabid bei kubwa kuliko wote hawa. Walibidi Sh 1,900 kwa lita wakati wengine walibid Sh 1,800. Baadaye kwa mlango wa nyuma wakaenda ku-negotiate kuuza kwa bei ndogo. Kwa nini waliposhindwa tenda wakaenda mlango wa nyuma kuuza kwa bei ndogo?

  "Tunafurahi kwamba tumepata mafuta kwa bei ndogo, lakini Wizara ‘is a different procurement entity' (taasisi tofauti ya ununuzi), hata kama unafanya hayo manunuzi, kwa nini kwanza usingekwenda kuwafuata hao Oryx na Camel Oil ukasema tupunguzie wakakataa ndipo ukachukua hatua hiyo?

  "Katibu Mkuu si ‘procurement authority' (si mamlaka ya ununuzi). Kwa nini yalitumika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu na kampuni? Kwa nini hukuandika barua PPRA kuomba wakushauri? Nikamwambia hii ingekulinda.

  "Nimehoji matukio mawili yanatofauti gani? Edward Lowassa ameng'olewa Uwaziri Mkuu si kwa sababu amepewa hela, kwa sababu Richmond haikupewa hata senti tano bali sheria ya manunuzi haikufuatwa. Hilo tu ndilo lililomgharimu Lowassa… kwa nini leo tusema sheria ya manunuzi haiwahusu hawa? Kwa sababu si Lowassa au Rostam [Aziz]?

  "Baadhi ya wabunge wanataka Maswi na Muhongo waondoke, mimi nasema hapana.

  Isije ikawa kwa sababu tuna ubavu tuwatimue tu, ninachosema Mhando arudishwe kazini. CAG atafanya ukaguzi ukweli ujulikane. Mimi nimekwenda kufanya ukaguzi miezi miwili iliyopita nimekuta PPRA imetoa clean certificate kwa TANESCO. Kama tunahisi kuna uchafu ambao hawakuuona tufuate taratibu," alisema Zitto.

  Suala la wabunge kufanya biashara na TANESCO, alisema hata yeye amezisikia tuhuma hizo kuwa wabunge hao wanatumiwa na mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia (jina limehifadhiwa), kuuza matairi na bidhaa nyingine kwa TANESCO lakini hana uthibitisho wa taarifa hizo.

  Alimshangaa Waziri Muhongo kwa kusema TANESCO inakusanya Sh bilioni hadi 70 na inatumia bilioni 11 tu kulipa mishahara, hivyo akataka fedha zinazobaki wazitumie kulipa madeni.

  "Asilimia 86 ya mapato ya TANESCO yanalipa makampuni yanayozalisha umeme - Songas, IPTL, Symbion na mengine. Na hii mikataba imeingiwa na Serikali. Kwa mfano, Symbion sasa wana mkataba wa miaka 20. Mimi nilimwambia Katibu Mkuu kuwa mnawapa Symbion zabuni ya kuzalisha umeme megawati 300 huko Mtwara, hivi Marekani ikiamua kuiteka nchi hii tutatokea wapi?

  Zito aliwataka viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO kuacha vita ya kupitia kwenye vyombo vya habari, Mhando arejeshwe kazini na CAG afanye ukaguzi maalumu kwenye shirika hilo.

  "Sitaki Maswi aonewe, wala sitaki yeyote aonewe. Ninaumizwa mno na vurugu zinazoendelea kati ya wizara na TANESCO. Hii ni vita ya masilahi waachane nayo. Tunataka umeme hatutaki maneno," alisema Zitto.

  Zitto alikemea alichokiita utamaduni wa kuwaona watu wenye maoni fulani na waliyonayo baadhi ya watu kuwa wamehongwa. "Ni utamaduni wa hovyo sana."

  Zitto alisema inawezekana Katibu Mkuu Maswi amefanya uamuzi wa kununua mafuta kutoka BP/Puma kwa nia njema, kisha akamnukuu Mwalimu Julius Nyerere: "Njia ya kwenda Jehanamu imejaa nia njema'."

  Maswi aanika ukweli wa mambo

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Maswi, kwa upande wake jana alikutana na waandishi wa habari na kusema wabunge wajiepushe na upotoshaji usio wa lazima, kwani Wizara ya Nishati na Madini haikufanya ununuzi wa mafuta, badala yake wizara hiyo ililipa tu na kazi ilifanywa na Wakala wa Vizazi na Vifo (RITA) ambaye kwa amri ya mahakama ndiye mfilisi wa IPTL.

  "Ni vizuri ikaeleweka kuwa mwishoni mwa mwaka 2010/11 kulikuwa na mgawo mkubwa wa umeme nchini, hivyo Serikali kulazimika kuingilia kati kuhakikisha mgawo huo unaondolewa na kuitaka IPTL kuwasha mitambo yake katika kiwango cha MW 100. Aliyefanya hivyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO na si Wizara.

  "Ikumbukwe pia wakati IPTL ilipokuwa inasimamiwa na RITA kwa kuwa kulikuwa na amri ya kuifilisi (under liquidation)… TANESCO walipeleka barua RITA wakitaka mafuta ya kuendesha mitambo yapatikane. Ieleweke kuwa ili kuendesha mitambo ya IPTL kwa siku moja tunahitaji MT 500.

  "Tarehe 24 Juni 2011, Mtendaji Mkuu wa RITA aliandika barua PPRA yenye Kumb. Na. BD.27/249/01/19 kutoka mwongozo na ushauri juu ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL kwa dharura na barua hiyo ikajibiwa na Mtendaji Mkuu wa PPRA, tarehe 28 Juni, 2011 kwa kumpa njia na mwongozo wa kutumia wakati wa dharura kwa kufuata Sheria ya Manunuzi na bila kukiuka utaratibu.

  "Mtendaji Mkuu wa RITA kwa barua yake yenye Kumb. Na. ADG/OR/1/2008/IPT/VOL. II/47A ya Julai 2011 na kupokelewa wizarani siku hiyo hiyo, alionyesha mchakato wa manunuzi uliofanyika na taratibu zinavyotakiwa.

  "Baada ya kupokea barua hiyo na kutokana na hali ilivyokuwa, hakuna aliyekuwa tayari kuhangaika na IPTL wala mafuta hadi nilipoteuliwa kuja kukaimu hapa tarehe 22 Julai 2011 na kuanza kazi tarehe 25 Julai 2011. Fedha zinazosemwa zililetwa wizarani ni za Serikali na si za TANESCO, Afisa Mwajibikaji (Accounting Officer) ni wa Wizara si TANESCO," alisema Maswi.

  Alisema Kanuni ya Ununuzi wa Umma Na. 42 ya Mwaka 2005 inampa mamlaka afisa anayewajibika na fedha kufanya manunuzi hata nje ya mipaka yake kwa masilahi ya uchumi wa taifa.

  "Napenda ifahamike wazi kuwa hapa kilichofanyika ni kuwa RITA ndiye aliyefanya ununuzi, sisi wizara tulifanya kazi ya kulipa tu," alisema na kuongeza kuwa fedha zilizotumiwa ni za Serikali na hazikutoka TANESCO kama inavyoelezwa.

  Alisema suala jingine ni kwamba wakati kampuni zilizopewa zabuni awali kuuza mafuta TANESCO zilikuwa zinauza kwa gharama ya Sh 1,800 kwa lita, BP/Puma wanauza lita hiyo hiyo kwa Sh 1,460. Pia BP ni mbia wa Serikali kwa asilimia 50 kwa 50 tofauti na kampuni zinazong'ang'aniwa ambazo ni binafsi. "Kuokoa Sh bilioni 2.7 za walipa kodi si fedha kidogo," alisisitiza.

  Alisema kampuni zilizokuwa na zabuni ya kuuza mafuta TANESCO zilikuwa zikinunua mafuta kutoka BP, walionyimwa zabuni ya kuuza mafuta kisha zinaiuzia TANESCO, kitu alichosema kinahitaji kuchunguzwa kwa nini iwe hivyo.

  Mkopo wa Sh bilioni 408 kwa TANESCO

  Maswi alisema mkopo huo una riba kubwa na utalipwa na wananchi, hivyo Serikali imeamua kwa njia nyingine wakati taratibu za kufuatilia mkopo zikiendelea, yenyewe imekuwa ikitoa ruzuku kwa TANESCO na hadi sasa imekwishatoa zaidi ya Sh bilioni 222.4. Alisema hadi juzi Serikali imetoa ruzuku ya Sh bilioni 25 kwa TANESCO, hivyo watu wasiibe wimbo wa bilioni 408 ambazo ni gharama kubwa kwa walipakodi.

  Maswi asisitiza mambo makuu matatu

  Kama ilivyokuwa mwaka jana, siku chache kuelekea kwenye bajeti ya wizara hiyo ilipokataliwa, kuna kila dalili kuwa zamu hii suluba bado itakuwa kubwa kwa viongozi wakuu wa wizara hii; Waziri Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakimu Maswi, kwani wabunge wameshaanza kurusha mashambulizi.

  Kikao cha Kamati ya Bunge Julai 17

  Katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini cha Julai 17 kilichofanyika mjini Dodoma, imeelezwa kuwa kilijaa vijembe, maneno mazito na kutunishiana misuli kati ya wabunge na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini.

  Huku Kamati hiyo ikiwa na msimamo kuwa Prof. Muhongo na Katibu Mkuu Maswi wajiuzulu kwa wanachokiita kashfa ya kuipatia Kampuni ya Puma zabuni ya kuuza mafuta kwenye mitambo ya IPTL bila kufuata taratibu za ununuzi wa umma, wizarani nako kuna hisia kuwa baadhi ya wabunge wanajifanya kuitetea TANESCO, kumbe wanatetea masilahi binafsi yanayobanwa na uongozi mpya wa wizara usiokuwa tayari kuyumbishwa.

  Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe (CCM), aliliambia Gazeti la JAMHURI kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Maswi, alimpigia simu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleiman Zedi, na kumwambia baadhi ya wabunge wanafanya biashara na TANESCO ndiyo maana wanashinikiza Injinia Mhando arejeshwe kazini.

  ---
  Deodatus Balile,
  JamhuriMedia.co.tz  Source: Previous Posts - wavuti
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sijasoma yote nitarudi baadaye lakini kufuata sheria kwa kuiingiza nchi kwenye hasara ya bilioni 6 kwa mwezi bora hizo sheria zikakaa pembeni...nitarudi baadaye nimalizie kusoma....
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa maelezo ya Maswi hana hatia kwakuwa wizara walikuwa walipaji 2 na watoa tenda ni RITA Issue Zitto anatetea asichokijua kikanuni kuwa maswi ni mlipaji hafanyi manunuzi, Zitto analeta siasa za kifisadi za kucheza na maneno ya kulinda Ufisadi, Hili Hatoki asitafute Mchawi eti kutangaza kugombea nani angemteua agombee na ninani angemchagua kuwa Rais kwa sifa hizi za kulinda Mafisadi! Mwisho wa Ubaya Ni aibu!
   
 4. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nimeisoma yooote, kitu kimoja ambacho binafsi sikielewi ni kwanini kamati na wizara na management wanashindwa kukaa pamoja kama watu wanaojenga nyumba na kukubaliana

  Kingine kinachonitatiza na kuutilia mashaka umakini wa Zitto hongo or in absence of it...sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 imeweka bayana umuhimu wa mtumishi kusimamishwa kupisha uchunguzi iwapo mazingira yanaonyesha kuwapo kwake kazini kutavuruga ushahidi.

  Zitto Kabwe tafadhali sana elewa Mhando amesimamishwa kazi na mamlaka yake ya nidhamu ambayo ni bodi.

  Uchunguzi unafanywa na CAG ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali,sio layman

  Serikali haina pesa,TANESCO inahangaika kutafuta pesa,mtu anaokoa pesa ndio unataka asulubiwe ?! Ok nani amewapa kibali TANESCO kununua mafuta ?na ilikuwaje makampuni ya mafuta yakaweza kuagiza kabla ya contract period? I mean walishapewa award na TANESCO au ? Maana kuna taratibu za kusitisha award kisheria na TANESCO wanazijua

  mwaka juzi alisimamishwa afisa mkuu wa fedha na meneja mwandamizi manunuzi ili kupisha uchunguzi

  Watu hao wawili baada ya uchunguzi kukamilika na wakarudishwa kazini ulikuwa umeshachaguliwa kuwa mkurugenzi na ukawaondoa kwenye nafasi zao wakiwa hawajakutwa na kosa lolote

  Ningekuomba ustay put uchunguzwe kama msafi utarudi tu kwanini unalay dirty linen hivi
   
 5. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  ujue kujifanya mjuaji sana kuna madhara tatizo la zitto ni ujuaji na kujiaona yeye ndo yeye wenzake wanajenga nchi na kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa hili yeye amekalia kupiga majungu na kulilia urais eti anamwambia mwakembe ukim-touch tutakumaliza...yeye kama nani?
   
 6. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama unavunja sheria kwa kuisaidia nchi nazani ni ruksa na ndo viongozi tunaowataka.......ilo la kumwjibisha Mhando kama halikufuata taratibu labda twaweza ku laani but kuokoa fedha zetu japo ni haramu but ruksa
   
 7. F

  Fofader JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Aliyevunja sheria ni aliyeanzisha mgao feki ili mafuta yanunuliwe. Huyu ndio atueleze vizuri alikuwa na nia gani na watanzania maskini?
  Gharama yote tunabeba sisi kama wananchi kwa kulipia umeme au kodi. Wewe huoni kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria unamsakama mtu aliyetujulisha na kupambana na uozo pia wizi mkubwa unaofanyika? Kweli ukistaajabu ya.....
   
 8. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Wengi tunaweza kusoma,
  lakini hatuwezi kuchambua,
  na kujua maana ya kilicho,
  andikwa kwa undani.

  Kuna haja ya kujielimisha,
  zaidi katika uwanja wa,
  kuchambua hoja kwa,
  kwa umakini mkubwa,
  na kuuliza maswali ya,
  udadisi na kutaka kujua zaidi.
   
 9. M

  Mpalisya Imbogo Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Bravo Zito, napenda unavyodadavua hoja. Keep it up
   
 10. w

  watogo Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ngoja tuskie kesho zito ataongea nini? maana haya mambo yanapoelekea si mchezo
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du tutagundua Mengi kumbe kuna wenzetu wanakula Nchi kwa mirija nimelikumbuka Azimio la Arusha
   
 12. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Inabidi usome kwa umakini ndugu hayo manunuzi walikubaliana baada ya hiyo kampuni (BP) kupunguza bei kutoka Tshs 1,900/= na kuwa chini ya Tshs 1,800/= kwa lita kama hayo makampuni mengine yalivyo tenda, sasa kweli hata kama ni kuisaidia nchi kwa nini wasifanye maongezi na hizo kampuni nyingine kama Zitto anavyo sema? kwa mtazamo wangu waliochukua uamuzi huo wa kuipa BP hiyo tenda ndo wamechukua rushwa ili kupindisha sheria ya manunuzi na si vinginevyo. Bravo Zitto umeeleza kwa kina tatizo watu wavivu wa kusoma na hilo ni tatizo la Watanzania.
   
 13. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 823
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  haramu kwa lowassa na rostam lakini halali kwa muhongo na maswi.hii ndio double standard!
   
 14. M

  MKATA UFUTA Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!! ujinga mzigo. Watz tusiwe wepesi wa kuhukumu bila kutafiti na kuujua ukweli
  GAUTAMA BUDDHA-Mwanzilishi wa imani ya kibudha aliwahi sema" Usiamini jambo eti kwakuwa mtu maarufu ametamka,au mtu unayemuamini ametamka au vitabu vitakatifu vimeandika, amini jambo hasa kwakuwa umelichunguza na kuona uthabiti wake"
  Wengi wa wachangiaji JF na watanzania naona tayari mmeshamuhukumu ZITTO bila kuelewa undani wa sakata lenyewe. Sijui kama Zitto anamakosa au hana, chamsingi tujiulize ni nini anachokisimamia?
  Anachosema Zitto ni kuwa, Kitendo cha waziri kuwapa tenda PUMA (BP) hakikufuata utaratibu wa kanunu za ununuzi za serikali. Hapa haijalishi kuna unafuu wa bei au lah. Hiv, kwani kwenye unafuu wa bei hakuna ganji? Taratibu za ununuzi serikalini zinataka kushindanisha kwa tenda, hapa haijalishi mwenyejukumu la kununua mafuta ni Tanesco au Wizara
  WAZIRI MUHONGA, anajitetea kuwa mkataba wa mufirisi juu ya IPTL unaitambua wizara tu, kuwa ndo wanastahili kununua mafuta kwaajili ya IPTL.

  MASWALI YA KUJIULIZA WANAJF WENZANGU
  • hivi kwakuwa mafuta yalistahili kununuliwa na wizara,je kanunu za ununuzi ndo zisifuatwe?
  • kama kweli mkataba unaitambua wizara kununua mafuta ya IPTL, nikwanini waziri alimuagiza Muhando kununua mafuta kwanza?
  • kama puma, ilitenda mafuta kwa bei kubwa Tanesco baada ya kushindwa ikazunguka mlango wa nyuma na kutenda wizarani kwa bei ndogo, Je zile kampuni nyingine Waziri alikuwa na uhakika gani kuwa zisingetenda kwa bei ndogo zaidi wizarani kama zingeshindanishwa?
  Tuache ushabiki usio na mantiki, tusihukumu TUACHIE SHERIA NA TARATIBU ZICHUKUE MKONDO WAKE
   
 15. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 823
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  hana hatia? Wakati hakufuata sheria!ukivunja sheria una hatia tu.vinginevyo kwa nini tuwe na sheria.tufute sheria zote tuishi KWA KUTEGEMEA NIA NJEMA!
   
 16. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 823
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Historia inajirudia kwa njia ya kushangaza,wakati dowans inauza majenereta kwa bei nafuu dk rashid akataka kuyanunua kupunguza gharama alipingwa kwa sababu sheria wakati haikuruhusu serikali kununua vifaa vilivyotumika.tukaingia hasara wachumi wakatushauri 2ibadilishe hio sheria kwa sababu ilituingiza kwenye gharama kuununua umeme kutoka ktk mashine hiohio ilotumika kwa bei juu.LAKINI HAWAHAWA WALING'ANG'ANIA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE LKN LEO MASWI NA MUHONGO WANAVUNJA SHERIA WANAITWA MASHUJAA!
   
 17. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hivi wabunge wetu walikuwa wanashabikia nini kama ishu yenyewe iko hivi.hivi hizo kampuni zilizonyang'anywa tenda na kwenda mahakamani zikishinda kesi na serikali kuamriwa kulipa fidia bado watakuwa upande wa muhongo na maswi
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nsiande kama umesoma habari zote kwa makini huoni changa la macho?..Ebu tujiulize hivi huyu Maswi sii mwajiriwa wa Tanesco na madai mengi sana aloyatoa yanawaondoa tanesco kwa maswala ya wizarani lakini wao wako tayari kumsimamisha kazi mtu wa Tanesco ambaye sii mwajiriwa wao. Waziri yupo tayari hata kuvunja board ya Tanesco lakini tukirudi nyuma CEO wa Tanesco sii anateuliwa na rais?.. Sasa kama kuna ushahidi huo tosha kabisa kwa nini Waziri na makamu wake wasiende kwa rais na ushahidi wao, halafu TAKUKURU ili waajiriwa hawa wasimamishwe kazi wakati uchunguzi ukifanyika..

  Kuna sehemu utaona Maswi akisema hakutaja majina ya wabunge waliochukua Hongo, habari nyingine inasema kawataja.. Na hao waliotajwa wamemfuata kuomba ushahidi anadai tena hajasema hivyo na ushahidi asiiutoe. Jingine ni kwamba anazidi kusisitiza BP shell kuwa ndio PUMA energy wakati sio kweli kabisa.

  Puma walinunua share za BP na nakuhakikishia Puma energy International hawana mahusiano na BP hata kidogo na wanauza Franchize popote mwekzaji akijitokeza ukiwa na uhakika wa supply ya mafuta wanayosafisha. Kazi hii ingewezekana kufanywa na serikali ikiwa wameweza kuwa na share BP Shell kabla haijauza share zake kwa PUMA energy Tz ambayo ni sawa na Agent wa Toyota, GM, Sheraton au Mc Donalds hapo Bongo. Ukiona Gas Station ya BP Shell nyumbani usifikirie BP ndio wamiliki isipokuwa kuna mtu mwenye kumiliki duka hilo na anatumia vigezo na viwango vya shirika la BP katika kutoa huduma na kuuza mali zao.

  Sasa tujiulize hili shirika la Puma energy Tz ni nani analimiki? halafu tuangalie ilikuwaje serikali ilokuwa na Ubia na BP Shell wamekubali kuingia Ubia na shirika ambalo limenunua share za BP Shell kwa vigezo gani, na kwa nini BP Shell iliondoka. Na maadam Puma energy Tz wana share na serikali ina maana ushuru pengine hawana, hivyo mafuta yao yanatakiwa kuuzwa chini ya Tsh 1000 kwa litre.

  Binafsi yangu nashindwa kuelewa kwa nini waziri anaingilia ajira za Tanesco wakati yeye sio mwajiri. halafu inashangaza zaidi kwamba Mafuta ya Tanesco lakini yananunuliwa na Wizara kwa madai kuwa hizo ni ni fedha za wizara sio za Tanesco... How do you account for that? ikiwa Tanesco sio idara wala part of ministry utaziweka ktk fungu gani la mahesabu..
   
 19. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,962
  Likes Received: 37,508
  Trophy Points: 280
  Hivi mbona maelezo ya ziito yako wazi kabisa.Tutafakari haya mambo:-
  1.Kwanini PUMA walishusha bei kinyemela tofauti na sheria zinavyotaka?
  2.Hivi hata uamuzi wa Maswi wa kushusha bei na kuokoa fedha za serikali hauwezi kushawishiwa na rushwa?
  3.Maswi alihoji kama awali hiyo kampuni ya PUMA ilikuwa na bei ya sh 1900/= na baaadae kushusha baada ya kujua bei za makampuni mengine?
  4.Zitto kutaka taratibu zifuate na kupendekeza CAG afanye uchunguzi ndio kumlinda Mhando?
  5.Kama Maswi alijua kuwa PUMA walikuwa na bei ya sh 1900/= kwa lita na baadae kushusha bei kinyume na taratibu za tender alichukua hatua gani?Tender huwa ni siri mpaka zinapofunguliwa au mimi nakosea kusema hivi?
  6.Hivi mtu mwenye nia ya kukulinda kweli anaweza akataka uchunguzwe na mtu ambaye hata yeye hawezi akamuingilia ktk uchunguzi wake?

  Kwakweli kama taarifa hizi ni za kweli basi ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha sana kuona watu wanamshambulia Zitto ambae anaonekana wazi amesimama katikati na wala hana upande.

  Kwa kuzingatia matukio ya nyuma ktk maswala kama haya na wewe ukiwa kiongozi makini ukisikia mtu amekiuka kanuni hata kwa sababu kama hiyo kweli nafsi yako itakuwa haina hata chembe ya mashaka na ukataka kupata ukweli?Ni katika matukio mangapi sheria ya manunuzi ya umma imekiukwa kwa faida ya taifa ktk kipindi hiki?Kwa kuzingatia ukweli huu kuna nini cha kushangaza kwa zitto kutaka uchunguzi?Hivi ukiumwa na nyoka ukisikia jani linacheza utaacha kushituka?

  Inasikitisha sana sisi watanzania tuko hivi.
   
 20. U

  Uriria JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 744
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  Tutaskia mengi sana
   
Loading...