Jitu la kienyeji
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,446
- 7,990
Ukienda kusalimia ukweni muda wa wiki moja kuna tabia ambayo shemeji zako wanazo wanaamka saa 11 alfajiri halafu wanasogoea karibu na mlango wa chumba ulicholala wanagonganisha majembe, hii ni ishara ya wewe uamke uwende nao shambani kulima.
Usiwe mzembe amka nenda nao shambani kapige jembe kweli kweli ili warudi kusimulia kwa wakwe zako na itakuwa heshima kwa mkeo Pia hakikisha unapunguza matumizi ya simu.
Uwapo ukweni usipende sana kukaa karibu na wazazi wa mkeo we nenda ndani kaa au eneo maalumu lilotengwa kwa ajili ya kupumzikia ucheze na watoto michezo itakakayowafanya wakupende huku ukiwapa na vihela vya kununua pipi mara kwa mara.
Usiende jikoni kumuuliza mkeo kama amechelewesha chakula we tulia mchatishe kwa simu atakupa utaratibu na mambo yatakuwa sawa pia hakikisha unakuwa wa kwanza kushiba hii itakusaidia sana kukuamini.