Acha hizo Mkuu; mtu akienda Corner Bar akamnunua mwanamke itaitwa mahari?
Taratibu, unaanza kudhirisha sura yako halisi ingawaje ulianza kwa unafiki wa kutokuwa na nia ya kukashifu! Kwahiyo kwa akili yako, hiyo aya ina viashiria ya uwezekano wa Quran kununua kahaba?! Hivi hudhani busara ingekuwa ni kuomba FULL VERSE au hata kuitafuta mwenyewe kuliko ku-conclude kwamba aya husika inaashiria uwezekano wa biashara ya ngono?!
Kama kweli ni Mfiaukweli kama ambavyo unajiita, basi wakati mwingine unatakiwa kuutafuta huo ukweli wewe mwenyewe, na endapo ungefanya hivyo, ungegundua mara moja alichotoa mdau, ni kipande kidogo tu cha aya mzima ambayo inasema:
Also (forbidden are) women already married, except those (captives and slaves) whom your right hands possess. Thus has Allah ordained for you. All others are lawful, provided you seek (them in marriage) with Mahr (bridal money given by the husband to his wife at the time of marriage) from your property, desiring chastity, not committing illegal sexual intercourse, so with those of whom you have enjoyed sexual relations, give them their Mahr as prescribed; but if after a Mahr is prescribed, you agree mutually (to give more), there is no sin on you. Surely, Allah is Ever All-Knowing, All-Wise.
Swahili version inasema:
Na pia (mmeharimishiwa) wanawake wenye kuolewa, isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairi ya hao, kwamba mwatafute kwa mali zenu, kwa kuwaoa bila ya kufanya zinaa, Na kwa ajili ya faida mnayoipata kwao, basi wapeni mahari zao zilizolazimishwa; wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) mahari. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.
Sasa hivi unaamini kabisa kwamba hiyo aya inafanana na madai yako ya kufananisha na ununuzi wa makahaba?!
Na ukiisoma Sura husika kuanzia aya ya 19-25 inazungumzia ni nani unaweza kuoa na kwa namna gani na yupi huwezi kuoa! Mfiaukweli utageuka kuwa Mfiaviroja ikiwa unaamini aya inayozungumzia suala la la yupi uoe na kwa namna gani basi itakuwa inazungumzia suala la kununua ngono!!!
Tatizo ni kuwa mnaosema aya hiyo unahusisha mahari mnasahau matumizi ya maneno "ujira/mshahara" kutokana na "raha aliyoipata mwanaume kwa mwanamke". Hiyo ndio tafsiri ya mahari?
Narudia, kama kweli wewe ni Mfiaukweli, basi jenga utamaduni wa kuutafuta ukweli kisha ndipo uusimamie! Si Quran wala Bible inasomwa kwa mtindo unaosoma wewe... kwamba, kutoka kwenye aya mzima, unanyofoa mstari wa mmmoja au miwili, tena kwa kuubananga bananga na kujenga hoja kupitia mstari husika!!!
Nakupa changamoto!!
Achana na Aya zote nilizoweka mimi lakini nakuomba wewe uniwekee aya zilizokamilika za mada husika!
Tuanze na hoja yako hii:
Tatizo ni kuwa mnaosema aya hiyo unahusisha mahari mnasahau matumizi ya maneno "ujira/mshahara" kutokana na "raha aliyoipata mwanaume kwa mwanamke". Hiyo ndio tafsiri ya mahari?
Weka hapa AYA ILIYOKAMILIKA ambako umenyofoa hayo maneno.
Na kwavile si Quran wala Bible ambazo mara zote unaweza kuzisoma kwa aya moja peke yake na usipotoshe, basi changamoto nyingine ninayokupa, naomba uniwekee na aya mbili za juu yake na mbili za chini yake ili tuzijadili na tuone ikiwa unachosema ni kweli!
Ukishindwa kufanya hayo, kimbia kanisani ukaungame au fanya ibada yoyote kwa mujibu wa imani yako ili ukatubie dhambi ya unafiki, kwa maana Matayo 23:27-28 anasema:
Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28 Hali kadhalika, nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
Huko kujifanya haupo kwa lengo la kukashifu wakati ndio lengo lako na ndio maana kila unachoambiwa hutaki; ndo huko ambako Matayo ameita:
makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu...