Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Tume ya Kupambana na Rushwa ya Zimbabwe (ZACC), imetangaza kufungua upya jalada la Uchunguzi dhidi ya Mfanyabiashara Wicknell Chivayo kutokana na kuhusishwa kwake na masuala ya Rushwa na Ufisadi katika miradi aliyoifanya na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ZACC, imeeleza kuwa Maendeleo katika kesi zinazomkabili yalicheleweshwa kutokana na mchakato mgumu wa kupata ushahidi muhimu na usumbufu wa nje ambao ulizuia mahojiano ya wakati unaofaa kwa mtuhumiwa.
Soma > Chivayo 'Mwizi wa Uchaguzi’ na ‘Kipenzi' cha wanasiasa Barani Afrika, ameshatia mkono na kwetu?
Aidha, Tume hiyo imesema Kesi zote zilizowahi kufunguliwa awali zikiwahusu watu wote hata ambao wanaushirika na Viongozi wa Serikali zitachunguzwa upya bila uoga, upendeleo au kubagua mtu yeyote.