Zima Moto Katika Ubora Wake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261


ZIMA MOTO KATIKA UBORA WAKE
Nimeikuta hii video mtandaoni na nikaiangalia kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Wakati mwingine nilikuwa nacheka peke yangu.
Kwa nini nacheka?

Kwani hili jambo la kuchekesha?

Hili ni jambo la kusikitisha na hakuna shaka katika hilo.

Lakini kuna wakati hata msiba badala ya kusikitisha ukachekesha.

Huyu aliyeweka hii video kaandika maneno haya chini ya video hii:
''Fire Brigade wamefanikiwa kuokoa mali baada kufika katika tukio na vya kisasa.''

Mwaka wa 1974 ilikuja movie jina lake ''The Toweing Inferno,'' na ilikuwa maarufu sana kwani ilisheheni waigizaji nguli wa nyakati hizo na hapa nitawataja wachache: Steve Mc Queen, Paul Newman, Fred Astaire.

Huyu Fred Astaire wanasema hapajatokea mtu aliyekuwa na kipaji cha kucheza dansi kumshinda.

Wakati senema hii inatengenezwa Marekani niliuwa na rafiki yangu anaitwa Credo Sinyangwe wakati huo akisoma huko na alishuhudia senema hii wakati wa shooting kwani alikuwa akifanya kazi jirani ya jumba lililokuwa linafanyiwa shooting ya hii movie.

Yeye kwa kujua mapenzi yangu ya senema alipokuja likizo akawa ananihadithia yote aliyoshuhudia katika kutengeneza senama hii kuanzia vipi alivyokuwa anapishana na hapo na hawa waigizaji nguli na kuwaona kwa karibu.

Lakini kubwa na ndilo ninalolikumba zaidi ni jinsi alivyokuwa ananieleza zima moto ya Marekani inavyofanya kazi kama alivyoshuhudia katika utengenezaji wa hii movie.

Hapa akawa ananieleza vifaa vya zima moto vya huko na vifaa vyetu.
Hii ilikuwa Tanzania ya mwaka wa 1974 yaani miaka 50 iliyopita.

Nusu karne.

Nilipokuwa naangalia hii video mazungumzo yangu na rafiki yangu Credo Sinyangwe yakanijia.

Huyu rafiki yangu ndiye kabla hajakwenda Marekani kusoma aliyenipa kitabu cha ''The Godfather,'' kilichoandikwa na Mario Puzo nisome na akanifungulia mlango wa kuwajua Mafia.

Toka siku ile nimekuwanao kwa karibu kwa kusoma kila kitabu kuhusu wao na kuangalia kila movie kuhusu wao.

Turejee tulikotoka.

Sote vijana wadogo tuko chumbani kwangu katika nyumba ya National Housing Corporation (NHC) Kinondoni, Mtaa wa Sekenke tunazungumza.
Nyumba hizi kwa zinaanza kupotea.

Nyingi ya nyumba hizi zimevunjwa na kujengwa nyumba nyingine zenye hadhi na zilizobaki kwa hakika ziko taabani.

Mimi nimekuwa na tabia ya kila ninapoikuta nyumba ya NHC basi nitaipiga picha.

Wakati Credo ananihadithia zima moto ya Marekani tayari nilikuwa nishaiona hii movie Empress Cinema kwa hiyo nilikuwa namuelewa vizuri anaponieleza uwezo wa zima moto ya Marekani.

Movie inapoanza mwanzoni ni gari za zima moto baada ya kupigiwa simu kuwa kuna moto katika jumba refu kupita zote mjini mjini San Francisco na vituo vya jirani vyote magari yanatoka mbio yanashindana kuwahi kwenye moto.

Scene hii inafurahisha kuiangalia.

Naangalia hii video ya zima moto imefika kuzima moto lori lililopaki natazama vifaa vya kuzimia moto...

Haya yanatokea leo nchini petu.

Nimechoka taaban sina nguvu na hapa ndipo nilipocheka lau jambo lenyewe ni la kutia huzuni.
 
Duuh! Sisi Waafrika bado tulitakiwa kuwa kule Ruaha National Park au Serengeti kama vivutio vya Utalii. Bado hatujawa binadamu kamili. Miaka 60 ya Uhuru bado uwezo wetu upo hivi.
 
Back
Top Bottom