Zilipendwa za redio RTD

Zilipendwa za redio RTD

Nakumbuka wimbo wa Ngoma naomba ujireekebishe, ni mwanaume gani anasuka nywele.
 
Kuleni kuku mayai mboga samaki maziwa na kujenga nyumba safi pakulala pawe bora
 
Na kipindi cha Afya kinaanza na wimbo wa "Kuleni Kuku mayai mboga samaki maziwa,kuleni chakula bora cha kujenga muili na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora"

Pia Mshamu alikuwa noma,halafu mzee Mundu mbishi kupindukia full mfumo dume! kuna akina Sijali ,Havijawa! Siwema binti mtayaona hadi raha!

Charles Hillary, mambo mpwito mpwito, mama Sarah Dumba - mama na mwana enzi hizo - RTD
Dah!!!!! Muhenga mwenzangu upo vizuri
 
Habari wana JF,


Leo sijui imekuwaje nimekumbuka sana vitu ambavyo viliniliwaza miaka ya 80 -90+ hivi;

Kabla ya ujio wa Tido muhando na kuibadili RTD, TVT na kuwa TBC taifa,FM na TBC kulikuwa na vipindi vitamu murua kabisa.

Mfano ni kipindi cha mama na mwana nilikuwa nakipenda aki ya nani ni simulizi tu utoto bana tabu kwa kweli.

Taarifa ya habari na Jacob Jesha redio inaunguruma kama inataka pasuka.

Mpira Theki, Jongo , Hilary na matukio na mengine mengi.


Sijui mwenzangu unakumbuka yapi sikuzile za clabu Leo shoo.
ilikuwa miaka ya 2000+ nilikuwa bado mdogo sana.....nakumbuka tuu kulikuwa na tangazo moja la Revola nilikuwa nalipenda sana nikilisikia lazima nifwatishe, mkaka anamuuliza mdada

"nieleze siri ya urembo wako" anajibu " sio siri ni revola" mkaka anauliza " "revola peke yake?" anajibiwa " ndio kwani maisha yake ni tulivu na huniweka fresh mchana kutwa"
kitambo sana yaani
 
Asbuhi kulikua na kipindi cha Jambo, ni kipindi cha salamu, zikienda Sambamba na burudani ya mziki, salumu zilikua zinatumwa kwa posta Card.
Mchana: mchana mwema, jioni: Jioni njema. Pia kulikua na kipingi cha mkoa kwa mkoa, kipindi kilichokua kikihusisha maelezo, Tamaduni za wenyeji wa mkoa husika.

Kulikua na Kipindi cha Misakato, Ombi lako, ni vipindi vya burudani ya mziki, kipindi cha zilipendwa ni miziki ya zamani, zaidi hii ambayo hivi sasa tunaita zilipendwa.
Kipindi hicho iliitwa RTD, ikimaanisha RADIO TANZANIA DAR ES ALAAM.
Kipindi hiyo Radio ilikua moja ikiwa na idhaa tatu,
1. Idhaa ya Taifa
2. Idhaa ya Biashara, kama sikosei matangazo yake yalikua yakianza alasiri kwa siku za kazi, siku mapunzi mchana.
3. Idhaa ya nje, hii matangazo yake yalikua yakienda kwa kiingereza.
Magazeti wakati huo, yalikua Matatu, Uhuru gazeti la kila siku, ispokua juma pili, sina uhakika.
Mfanyakazi, lilikua linatoka Juma tano na Juma mosi, pia kulikua na Mzalendo ambalo hutoka juma pili tu.
Magazeti haya yalikua yakichapwa na shirika la shirika la uchapishaji la serikali wakati huo KIUTA.
Hutuba ya rais Nyerere kipindi hicho ikianza, kama kuna mtoto anakohoa, huambiwa akae mbali.

Ila kulikua na maigizo kipindi hicho, iliitwa mchezo wa radio, kipindi cha mahoka, Pwagu na Pwaguzi. Kipindi hicho Taifa lilikua moja, inchi ilikua ya Kizalendo kwelikweli, mtaani huwezi kaa na mtu asiejulikana anuani yake kama hivi sasa, huko vijijini kulima, ilikua lazima kucheza karata, bao, kukaa vijiweni, kunywa pombe asbuhi, mnakamatwa,

Vijiji vilimaliki mashamba yao ya kijiji, yaliitwa Mfumaki,
Maduka ya vijiji maduka yalikua machache sana kipindi hicho.
 
Salamu kwa wagonjwa, mtangazaji anamwuliza mgonjwa nini shida yako hadi umelazwa hospitali, mgonjwa alikuwa mchaga akajibu, ndugu mtangazaji mimi ni fuu fundi umeme kweli siku ile nilikuwa natengeneza umee umeme kweli basi nilikosea nikaunganisha waya mwekundu na waya mweusi, bwana wee kililia kitu, shoti !!!.Niliungua vibaya ndo nikaletwa hapa.Mtangazaji akamwambia tuma salamu na chagua wimbo wa kukuburudisha.Kwa wimbo ningependa nipigiwe wa Pe wa Peter Tesha kweli ( Peter Tosh ).
 
Jogoo Amelia tuamke "wandugu tuamke watu wote tuamke kutafuta maisha Furaha ya dunia aaa haina mwisho"

Sijui unamkumbuka alikuwa nani
 
Nakumbuka tangazo la Rushes
"Rushwa ni mdudu hatari sana......"
Nilikua bado chalii sana Kipindi hicho nikawa sielewi rushwa ndo nini nikawa nadhani labda kuna mdudu kabisa anaitwa Rushwa
Kwaiyo sasaiv ushaelewa rushwa ni nn au sio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom