Zilipendwa za redio RTD

Nkolandoto

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
3,877
3,675
Habari wana JF,


Leo sijui imekuwaje nimekumbuka sana vitu ambavyo viliniliwaza miaka ya 80 -90+ hivi;

Kabla ya ujio wa Tido muhando na kuibadili RTD, TVT na kuwa TBC taifa,FM na TBC kulikuwa na vipindi vitamu murua kabisa.

Mfano ni kipindi cha mama na mwana nilikuwa nakipenda aki ya nani ni simulizi tu utoto bana tabu kwa kweli.

Taarifa ya habari na Jacob Jesha redio inaunguruma kama inataka pasuka.

Mpira Theki, Jongo , Hilary na matukio na mengine mengi.


Sijui mwenzangu unakumbuka yapi sikuzile za clabu Leo shoo.
 
sikuwahi kuisikiliza RTD
Mkuu yaani ilikuwa tamu unajua tena na redio kijijini zilikuwa za watu wachache

Ikifika kipindi cha mama na mwana watoto wanajaa nyumbani kusikiliza hata kama mlikuwa na mechi lzm isimame hata kama kulikuwa na ngumi za ugomvi lzm zisimame baada ya kipindi ndo mnaanza hivi tuliishia wapi

Teh
 
Nakumbuka tangazo la Rushes
"Rushwa ni mdudu hatari sana......"
Nilikua bado chalii sana Kipindi hicho nikawa sielewi rushwa ndo nini nikawa nadhani labda kuna mdudu kabisa anaitwa Rushwa
 
Nakumbuka tangazo la Rushes
"Rushwa ni mdudu hatari sana......"
Nilikua bado chalii sana Kipindi hicho nikawa sielewi rushwa ndo nini nikawa nadhani labda kuna mdudu kabisa anaitwa Rushwa
Kipindi hicho wanaita rushwa ni adui wa haki

Na maduka ya ushirika ya kupanga foleni kununua sukari na unga nk

Ilikua raha

Teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom