Enzi za RTD na TVT unakumbuka nini na ulikuwa wapi?

Tr Paul

Senior Member
Mar 18, 2020
170
157
Wanabodi habari zenu ,unakumbuka nini ,ulikuwa unajisikiaje ,ulikuwa wapi tulipokuwa na chombo kimoja cha kupasha habari Tanzania ,Radio na TV ambayo ilikuwa RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD) na kwa upande wa TV iliitwa Television ya Taifa (TVT).

Mfumo huu haukutoa fusa kabisa ya kuwa na chaguo la kusikilkiza radio mbadala au kutazama runinga mbadala (monopoly) ,ilikuwa ukifungua radio automatically huna haja ya kutafuta sation inakuja RTD hapo unatumia radio ya mbao a.k.a mkulima na Redio hizi nyingi zilikuwa Philips na National pia ukiwasha TV inakuja TVT maana ndo pekee iliyokuwepo,hapo unatumia HITACHI inawaka kama inaungua na mlio wake ‘’shaaaaaaaaaa’ na mchele wa kutosha.

Mara moja sana ilikuwa inashika radio ya Kenya iliyojulikana kama KBC ,ulikuwa hupati shida na kidude kimoja tu kilifanya kazi zote kwenye radio ukikizun gusha kwenda kulia unafungua,ukipeleka zaidi unapunguza sauti na ukizungusha kushoto unapunguza sauti ,kushoto zaidi unazima,siku hizi subwoofer vikorombwezo vingi hadi vingine inaweza usijue kazi yake na usivitumie kabisa.

Tulitumia sana betri aina ya
NATIONAL na BELL na betri zilipoisha tuliweza kuzianika juani na kuzitumia tena ,nakumbuka sana aina ya baadhi ya vipindi hasa cha michezo saa mbilim na nusu kama sikosei utasikia tu mlio ambao nafikiri hadi leo bado upo,kipindi cha harakati baada ya taarfa ya habari ya saa kumi jioni nilivipenda sana,kwa upande wa KBC nilipenda sana mahubiri ya PASTOR PIUS MWIRU kila jumamosi mishale ya saa mbili usiku,alikuwa na sauti nzito na ya kuvuta.

Nilivutiwa sana na baadhi ya watangazaji nianze na JF member
mwenzetu Paschal Mayalla, Samada Maduhu,Sekioni Kitojo, Khalid Ponera, Edda Sanga, Charles Hillary , Abdallah Idrissa Majura, Happyness Ngasala , Shabani Kisu (sina uhakika na spellings), kwa upande wa KBC namkubuka sana mtangazaji aliyeitwa Leonard Mambo Mbotela.

Pia kuna kundi/makundi ya watuma salamu kupitia radio ,namkumbuka sana sana WA JADI FUNDI WA JADI BINADAMU MASHAKA, EDWARD KABAMBA (huyu sio wa zamani sana),akimaliza kutuma salamumu utamsikia akisema “ujumbe maisha ni kutafuta na wala sio kutafutana, namwambia Fulani bin Fulani atafute laini”, wahenga zaidi yangu ongezeeni nyamanyama, I do stand to be corrected where I have unwillingly wronged.

NACHOMEKEA,naomba mhenga mwenye KUYAMANYA MABO anipe namna ya ngoma inayopigwa/zinazopigwa TBC hasa inapofika muda wa taarifa ya habari , ambayo najua ni recorded nimekuwa nasikia mengi mara kuna ngoma 12 ,mpiga ngoma alikuwa kipofu nk natamani sana kujua hili,
SHUKRANI.

Mwifwa asante kuni tag uzi huu.
Nitachangia.

Kwa kuanzia mleta mada ni dogo, hivyo nitasaidia kumuelimisha vitu vichache.

  1. Japo RTD ndio Redio kongwe kabisa Tanzania, iliyoanzishwa 50'a, enzi hizo pia pia kulikuwepo na Sauti ya Zanzibar, Radio za dini kama Sauti ya Injili na international radio kibao za Kiswahili kwenye SW kama BBC Swahili, DW, VOA, Radio Moscow, RFi, Transtel, RSA, NHK, All India Radio, Sauti ya UN, Sauti ya Kenya, Swiss Radio International etc
  2. Kwenye Television, TVZ ndio TV ya kwanza ya Rangi Africa, ilianzishwa mwaka 1971. Kwa huku bara TV ya kwanza ni ITV na CTN mwaka 1994. DTV 1995, TVT ilianza 1999 tena matangazo ya mwanzo ni Msiba wa Mwalimu, hivyo enzi ni enzi za RTD, TVT ni majuzi tuu!.
P
 
Nakiri mi dogo sana ,mkuu unajua vitu hadi basi ulivyoviandika vyote vipya kwangu ,shukrani mkongwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom