ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

"Enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa we"
Bata alileta kizaa zaa Hadi jamaa akalala kwa make mdogo tu wiki mzima.
Nautafuta Sana huo wimbo
 
Mimi bana sikinde tuuu, jamani sikinde watani wangu msondo mtaniwia radhi. Dah kuna vibao nikivisikia mpaka natokwa na jasho kuna kitu km Duniani Kuna mambo, wikiendi nalala kwa taabu, kwa ujumla sikinde you rock my heart!! ningekuwa na pesa ninge invest trillions pale basi tu sina kitu. haya kuna hawa marques du zaire enzi za kamanyola bila jasho kuna kibao kama dola mtoto wa Dodoma( yakaa yaka eeehn mwana mama ndimandimaeee mwana mama ...... mtoto wa dodoma) kuna kinanda flani kinapigwa mle na gitaa yaani ni raha tupu!! inanikumbusha sana dada yangu marehemu Mage jamani wakati niko Sumbawanga alikuja toka Dar basi anaziimba hizi nyimbo za makwizzz aaah jamani KAMANYOLA BILA JASHO! ikaja telemuka telemuka chekechaaaaaa
Enzi hizo nikiwa na Philips Radio weee!! Mjini Tarime juu! nilikuwa hizi nyimbo nasikilizia sana kwa mawazo!
1.ASUBUHI NJEMA!
2.JAMBOOO!OOO!
3.WAKT WA KAZI !
4.MCHANA MWEMA!
5.JESHI LEEETU LA POLISIII NI CHOMBO CHA WANANCHIIIII!
5.POLEE!
6.JIONI NJEMA!
& LALA SALAMA DOOO! RTD Weee! uko wapiii!..ila umeshahu ule wimbo wa jesca uko wapi!
 
Wana Jamii Forum. Habari zenu nyote wapendwa. Samahani naomba mwenye wimbo wa Lovy longomba unaitwa ELIE WANGU anisaidie kuupata maana nimeshahangaika sana bila mafanikio. NAOMBENI MSAADA WANA JAMII
 
Daah Balantanda nimekufananisha na Mzee Masoud Masoud anajua sanaa miziki ya zamani na Muziki kama muziki kwa ujumla.

Pia ni mchambuzi mzuri sana hasa akiwepo katika studio yake ile.
 
Mombasa Roots Band Live Performance

Mombasa Roots Band performing Black Magic Woman Cover song from Carlos Santana Mombasa Roots Band perform every
Source : Mombasa Roots Band
 
Zipo habari kuwa kwa Sasa Sikinde zipo mbili na zote zinafanya shoo kila moja kwa upande wake.
Kuna Nginde ya Fresh Jumbe na Benovilla Antony na ipo Nginde ya Hussein Jumbe…
Mwenye habari kamili anaweza kutujuza kupitia ukurasa huu…
 
Napenda kuuliza huyu mama Lady Isa (isabelle) alikuwa anatokea nchi gani kati ya DR Congo au Kenya?
Nyimbo zake
1. Kutereza si kuanguka,
2. Dunia ina mambo (lukumba lukumba)

Lady Isa ni msanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mkuu.
 
Kuna wimbo unasema "wengi wamelazwa hospitalini na kuwekewa P.O.P shauri yako Hawae,Hawae P.O.P aah P.O.P......"
Nani anakumbuka umepigwa na nani?
 
Msaada,kuna nyimbo naitafuta ila sijui kaimba nan na inaitwaje ila nakumbuk baadhi ya mashair yake km,
Ipo siikuuu_ mpenzi maua.
Nitakuja kwa wazazi wakoo_mpenzi upepoo.

Sina neno mm,kwakua najua,huyo n mzazi mwenzio mpenzi mauaaaa
Neema
 
Daah Balantanda nimekufananisha na Mzee Masoud Masoud anajua sanaa miziki ya zamani na Muziki kama muziki kwa ujumla.

Pia ni mchambuzi mzuri sana hasa akiwepo katika studio yake ile.
Aliwahi mwalika chidumule studio kipindi hicho akiwa redio Uhuru Masoud.

Chidumule alisema Kuna kundi lilitoka sikinde kwenda OSS,wakaahidiwa Mambo meengi mwisho wa siku hakuna walichopata,wakampiga vijembe boss wao wakamtungia wimbo,Home imenizidi-OSS.
Moja ya mstari uliosikika kwenye huo wimbo,,,ndugu zangu mlioolewa mjihadhari na wadanganyifu msiachane na wanaume zenu nawaambia.

Huku sikinde na chidumule wakawaimbia wimbo wenzao,,,,mtoto akililia wembe mpe.

Moja ya mistari yake inasema,,,hakuna nyumba Wala kibanda ulichoambulia,pole dada uliyataka mwenyewe.
 
Raha tupu kutoka kwa wale wazee. Daaah
 
Ina mstari unasema "Nimemuacha mume wangu eee nimeenda kwa leani ooo baada ya muda kanifukuza kasema siwezi kuishi nae.
 
27 November 2022

Ngouma Lokita interview ( in kiswahili) with Mfumu Kibangu

Nguma lokito is one of the best bass guitarist of our time,As he narrates in this interview he played with koffi olomide ,mayaula mayoni soukous stars among others great groups.Kindly subsvribe to this channel as you enjoy the coversation.
Source : mfumu Kibangu
 
Jamani natafuta wimbo wa OMARI MKALI wimbo wa kitambo kidogo unaitwa Kibuyu, hapa nina uhakika kuna kila aina ya watu natumaini nitaupata mwenye nao nauomba tafadhali.
 
Yote aliyofanya ndugu yangu Joseph Pauline ni sawaa au amekosea eeeh ni sawa au amekosea a eeeh .

Pauline kafanya mambo katuacha kwenye mataa ee Pauline .....
Katuacha tumeduwaa eeh
Vyombo......

Chorus. ......Jambo la kushangaza Pauline kafanya party la kuuga umasikini eeeh, Pauline oooh oohh laa la la laaa la.

Tumesukuma nae mikokoteni maskani ooohh oohh jama aa Pauline rafiki yetu la la la la

Chorus repeats!

Watu wengi walihudhuria pati hilo ooo

Fred Benjamini alikuwepo
Toto Tundu alikuwepo

Shomari Ally akikuwepo

Shakashia alikuwepo

Suleiman Mbwembwe alikuwepoooo

Mkuu nimekumbuka mistari hiyo japo kwa kujivuruga. Majina ya wanamuziki waliotajwa kwenye wimbo huu walikuwa mahiri sana wakati ule. Na ni katika Album hii Vijana Jazz ilianza kufifia. Wengi waliondoka na wengine walishatangulia mbele ya haki. Ni Album ya msimu wa 1996/97. Baada ya hapo Vijana haikutoa Album iliyohit kwani ilitoa I love you Mpiga debe miaka ya 1999 na Mabaa Maid miaka hiyo ya 1999/2000.

Sababu kubwa ni viongoz wa bendi yaani UVCCM kuipa sapoti kubwa TOT Band.
Album hiyo yenye wimbo ulioutaja ndo ya mwisho katika mtiririko wa Pure Vijana Jazz Air Pamba moto, Saga Rhumba! Ukiondoa wimbo huo, nyimbo zingine nzuri kabisa katka album hiyo ni Mama Samia, Mbuzi yake kamba nk. Naitafuta hii Album katika CD ila naikosa. Ninayo kwenye tape, bahati mbaya vifaa vyangu siyo rafiki tena kwa tape.

Ila Bantalanda ninashida sana na wimbo Kapu la Mjanja na Janja ya Nyani pamoja na Visa vya Mume.

Wimbo huu visa vya mume naupenda sana hasa pale wanaposema- Nikipika wali unasema una mawe e , nikipika ugali unasema una mabuja sema kinachokukera bwana eeeh. Ilikuwa ni combination ya hatari wakina Adam Bakari( sauti ya zege). Daa zaman kulikuwa na Muziki na Vijana Jazz ilikuwa ni noma. Ila nayo ilipata Upinzani mkali kutoka Washirika Tanzania Stars(Watu Njatanjata) na Bimalee.
Huu wimbo nimeutafuta toka 2005 mpaka leo sijaupata. vipi ntaupataje?!
 
Back
Top Bottom