ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

wadau nautafuta wimbo unaimbwa hivi
watoto wamekuja juu ,wanadai nyumba yao
 
wadau nautafuta wimbo unaimbwa hivi
watoto wamekuja juu ,wanadai nyumba yao
Kila nilifanyalooo wao haliwapendezi na Wala hawakumbuki usia wa baba yaooo,
Marehemu aliusia ooooh wasinituptupe Wala wasinyanyase babaaaa ooooh mamaaaa!
Wengi wamenishauri eti nirudi nyumbani Sina baba Wala mama huko niende kwa naniiii
[emoji2400]Ni washirika band/Vijana jazz/Hamza kalala Sina hakika.
 

Kuna huu wimbo wa mama Jane. Unaimbwa "mama jane mke wangu kwaheri mama, mungu akulaze mahala pema peponi" . Wimbo huu ni wa kitambo sana ila sifahamu ni nani alieimba. Mwenye kuwa na wimbo huu tafadhali naomb uniwekee hapa nauhitaji sana.
 
1657009441616.jpg
 
Hapa tuko pamoja sana mkuu.....Sikinde daima(damu damu).....

Pia zamani nilikuwa mnazi wa Vijana Jazz wana Pambamoto kabla haijaanza kupotea na kufifia kabisa....

Kuna wimbo unasema…

Mimi na wee na wee na wee
Tumeamua tusiachane mpaka kufa
Mimi nasema nawe wasema twaelewana
Tusipate machonganisho ya pembeni
Tuwe na umoja pia na raha vyote sawa…

Tumefika Moroo, kwa Mbaraka Mwishehe, Moro kwa Salum Abdallah…

Ebana huu wimbo unaitwaje?!
 
Kuna wimbo unasema…

Mimi na wee na wee na wee
Tumeamua tusiachane mpaka kufa
Mimi nasema nawe wasema twaelewana
Tusipate machonganisho ya pembeni
Tuwe na umoja pia na raha vyote sawa…

Tumefika Moroo, kwa Mbaraka Mwishehe, Moro kwa Salum Abdallah…

Ebana huu wimbo unaitwaje?!

Balantanda nakuita tena Mkuu sambamba na Wakuu wengine mnaoweza nisaidia kuupata
 
kuna wimbo nautafuta sikumbuki kama waliimba vijana Jazz au bendi gani, kibwagizo chake kilikuwa hivi "enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa ee"
Dah umelenga mle mle.
 
Skärholmstorg Stokholms tour 2022
Sweden

DEKULA BAND : Song: Zinduna

Mtindo wa Sendema ya Moto ndani ya Sweden



Dekula Band Soukous Music: Song: Zinduna by Gaby K. Nkomba (live) Pakteatern skärholmstorg Stockholm Sweden 30/06/2022 Musicians:
  • Guitar/singer: Kahanga Dekula (Vumbi)
  • Guitar: Göran Larsson
  • Bass: Joseph Semafumu
  • Drums: Michigan Ngoy
  • Sax: Henrik Westerberg
  • Singer: Gaby Kababa Nkomba
  • Cameraman: Arwa Mzee Kobe Brayo
  • Quality images courtesy of Arwa-iCTv
Source : Dekula2 Band (official)
 
Hökarängens centrum Stokholms tour 2022
Sweden

Dekula Band mabalozi wa muziki wa dansi kimataifa : wapiga mtindo wa Zembelwa: wimbo: Usinicheke (maquiz original)



Msinicheke Kazi Ni Uhai Kwa Kila Binadamu, Kazi Ni Msingi Jamani, Sina La Kufanya Msinicheke ..... Hata Baba Mungu Aliumba Dunia Akifanya Kazi ...

Wakaazi wa jiji la Stockholm walisakata rhumba la muziki wa dansi kamanyola bila jasho lenye saxophone kali lilosindikizwa vizuri na ala zote za muziki pamoja na sauti ya uimbaji kiasi cha waliohudhuria tamasha la wazi jijini Stockholm kukumbwa na hisia kali kabisa kama vile wapo jijini Dar es Salaam

Dekula Band musicians are :
  • Guitar/singer: Kahanga Dekula (Vumbi)
  • Guitar: Göran Larsson
  • Bass: Joseph Semafumu
  • Drums: Michigan Ngoy
  • Sax: Henrik Westerberg
  • Singer: Gaby Kababa Nkomba
  • Cameraman: Arwa Mzee Kobe Brayo
  • Quality images courtesy of Arwa-iCTv
Source : Dekula2 Band (official)
 
Back
Top Bottom