ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

15 Apr 2020
Nairobi, Kenya & Medellin Colombia

Historia ya Kassongo wa Kanema

Sauti ya mkongwe Kassongo wa Kanema aliyezaliwa Jean Claude mji wa Lubumbashi jimbo la Katanga nchini DR Congo (Zaire) na kuhamia Afrika Mashariki Dar es Salaam Tanzania na kisha baadaye kulowea Nairobi Kenya.

Kassongo wa Kanema Jean Claude huko Nairobi akaja kutambulika kama muimbaji tajwa kiongozi katika wimbo maarufu wakati wa mwezi Desemba na Mwaka Mpya inasikika ktk kibao cha gwiji wa bendi ya muziki ya Baba Gaston wa Orch. Baba National na kibao kilichovuma sana kwa jina Kakolele Viva Christmas iliyovuma Tanzania, Uganda, Zambia, Malawi, Zimbabwe mpaka Republic of South Africa .

Kassongo Kanumba pia alipata fanya kazi na kina Papa Mickey, Tshala Muana, Super Mazembe, Virunga, Santa Fe, Marquiz Du Zaire ya Dar es Salaam wakapata contract Mauritius kwa siku 45, Sheikh Yahya Hussein mnajimu maarufu mtanzania aliyekuwa akiishi Nairobi akaialika Marquiz Du Zaire kwa ziara Nairobi kisha wakarudi Dsm.

Na baadaye Kassongo wa Kanema mwaka 1975 Baba Gaston wa Nairobi achamchukua toka Dsm akahamia Nairobi, ........ Disc iliyobeba wimbo wa Viva Christmas ilipata tunzo ya Gold mwaka 1976 kabla ya hata ya gwiji wa muziki barani Afrika kipindi hicho Franco Makiadi kufanikiwa kuweza kupata tuzo hiyo ya juu ambayo Franco hatimaye naye alipata tuzo ya Gold kwa disc iliyobeba wimbo Marioo mwaka 1985...

Kibao kingine kilichomtabulisha Kassongo wa Kanema ni alipojiunga na Super Mazembe wakatoa wimbo ulioenda kwa jina Kasongo ambao ulifanya vizuri sana.


Source : Afrocolumbia

Mahojiano ktk lugha ya kiSwahili na Kassongo wa Kanema:

THE LIFE AND LEGACY OF KASSONGO WA KANEMA JEAN CLAUDE OF SUPER MAZEMBE

Veteran Nairobi-based Congolese musician Kasongo wa Kanema has passed on. The former leader of the legendary group Super Mazembe collapsed and died at his Lang'ata home in Nairobi Tuesday evening. Fellow musician Longwa Disco said he was informed by Kasongo wa Kanema's children, Morris and Chantal, of his death.

His death comes barely days after that of Kenyan musician Aziz Abdi, who died last weekend in Voi on Saturday evening.

Kasongo was part of an elite group of Congolese musicians who relocated to Kenya in the early 1970s, under the tutelage of the legendary Baba Ilunga wa Ilunga, in search of greener pastures when Kinshasa held little promise for the many bands.

Kasongo is best remembered for his lead vocals in the evergreen Kakolele Viva Christmas song. Kasongo, who was in his mid-60s, was recuperating from a mild stroke he suffered from a few years ago
Source : Africa Live TV

Orchestre Super Mazembe - Kassongo 1978

Source : Franco Pepe Kalle
 
The golden music of Super Mazembe band...The legend Kasongo

Video Courtesy of
Source : churchill show

Super Mazembe - Shauri Yako


Source : Franco Pepe Kalle
 
Published on 30 Sep 2020
EXCLUSIVE: KING KIKII AVUNJA UKIMYA/ATOA NENO ZITO KWA WATANZANIA



Mwanamziki mkongwe wa muziki wa bendi Kikumbi Mwanza wa Mpango (King Kikii), amekutana leo na waandishi wa habari wa Mwananchi Digital waliomtembelea nyumbani kwake Temeke, kujua undani wa hali yake ya kiafya kwa sasa baada ya upasuaji aliofanyiwa wa uti wa mgongo uliompelekea kushindwa kusimama na kufanya shughuli zake za kila siku.

Akizungumza na waandishi, mke wa mwanamziki huyo ameeleza kuwa dalili za ugonjwa wake zilipata kuonekana kama mwaka mmoja uliopita, lakini alianza kuugua rasmi wiki tatu zilizopita na ndipo walimpeleka hospital ya Taifa Muhimbili kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa daktari mwanamziki huyo mkongwe ataweza kuinuka tena mara baada ya kuisha kwa ganzi ya mda mrefu waliyomchoma wakati wa upasuaji huku mkewe akiongeza kuwa anaamini katika Mungu na mumewe atapona kwa uwezo wa Mungu.

Aidha mke wa King Kiki ameongeza kuwa, watu waache utapeli, na asitokee mtu kusema wanaomba msaada wa matibabu kwa lengo la kujinufaisha, ila wanaweka wazi kwa atakayeguswa kwa vyovyote ama kumtembelea,kumjulia hali na kumuombea.
Source : mwananchi digital

................................................................................

King Kikii - Kitambaa Cheupe

Source : thebigyosef
 
Naomba kujua jina la wimbo na mwi/waimbaji wa wimbo wenye maneno haya;
“Kule bagamoyo kulee,kule bagamoyo kuleee,kuna mandege meupe”

Msaada tafadhali!
 
Yondo Sister



Kuna mengi usiyoyajua kumuhusu mwimbaji mahiri wa rhumba Yondo Sister



Source : Radio citizen
 
Bendi mojawapo ya muziki iliyolikamata Jiji mikononi enzi hizo mpaka sasa nyimbo zao vijana tunazisikiliza: sikiliza simulizi Dar es Salaam na Tanzania ikiwaka moto huku inachemka kwa muziki wa dansi

Mwanamuziki Matuka Mwenda Bizoo wa Orchestra Safari Sound na mtindo wa 'Masantula ngoma ya mpwita' wimbo wa Mwaka wa Watoto


Source: MUZIKI NA WANAMUZIKI

Bendi hii ya muziki wa dansi Orchestra Safari Sound Ilianzishwa mwaka 1978 jijini Dar es Salaam Tanzania :

Hapa "GUGO WA MUZIKI" Adam Zuberi katika MUZIKI NA WANAMUZIKI, anaongea na mwanamuziki Mkongwe na Mahiri aliyekuwa mpiga magitaa ya Rhythm, Second Solo na Solo gitaa katika Bendi ya Orchestra Safari Sound Masantula Ngoma ya Mpwita, Matuka Mwenda Bizoo. Bizoo anatuelezea jinsi wimbo wa MWAKA WA WATOTO wa Bendi hiyo jinsi ulivyotungwa na pia anatutajia mtunzi wa wimbo huo pamoja na wanamuziki wote walioshiriki kwenye wimbo huo. Pia Matuka Mwenda Bizoo anatuelezea ni kwa kiasi gani wimbo huo ulivyokuwa ukipendwa na wapenzi wa muziki wa Dansi popote pale walipokuwa wakipiga. Ni matumaini ya channel hii ya MUZIKI NA WANAMUZI kuwa utaburudika pamoja na kuelimika vilivyo katika video hii. Kama utakuwa na swali, maoni, ushauri au hata ukosoaji, jisikie huru kutoa maoni yako ilimradi tu yasiwe na matusi. Nasi tutajibu kadri tukavyoweza pale inapohitajika kujibu.

Kundi hilo ktk bendi yupo: Twahir Mohamed sax1, Mzee Alex sax2, Matuka Mwenda Bizoo gitaa, King Kikii Mwanza Kikumbi mwimbaji, Dingi Tuka, Kababa Nkomba Gaby, Sammy Makasa solo gitaa, Mbomboka, Mpoyo Kalenga, Kaumba Kalemba, Kalonga, Singa Singa bass guitar, Yusuf Karanga, mzee Motoo, Monga Stan, Sony Tshianda, Forie, ....
Source : MUSIC AND MUSICIAN

Bendi ya Orchestra Safari Sound


Source : John Kitime
 

Mahojiano na mpiga gitaa zito barani Africa Ngouma Lokito



Shungu Omba almaaruf Ngouma Lokto ambaye alitueleza mengi kuhusiana na maisha yake katika muziki na namna ambavyo anaona muziki wa "enzi" alizoanza yeye na sasa. Je! Ameshirikiana na wasanii gani wa Congo katika maisha yake ya muziki? Je! Ni nini kinachomkera kuhusu muziki wa Congo hivi sasa? Mbali na kupiga gitaa la bass, anafanya nini katika muziki?
Source : Kwanza Production

Lokito Ngouma kafanya kazi na wanamuziki wakubwa akiwemo Pepe Kalle mfano kibao hiki: Pomoun Pak Bouger - Pepe Kalle & Empire Bakuba

 
Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....

Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.

Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael' na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....

Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....

Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....
Ibrahim Mwinyichande, Boniface Kachale
 
Back
Top Bottom