ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

kuna wimbo una maneno kama sijasahau... wanaimba wanasema "judy eeeehh eehh nikupe nini uridhike ,judy eeh chakukupa sina mama eehh... ufukara nilio nao..ufukara umekuwa kashfa ya mapenzi yangu...nlizunguka dunia nzima kukupenda....sijui waliimba akina nani na unaitwaje au nani anao
Ni wimbo wa Julie...Uliimbwa na Washirika Tanzania Stars Band... Watu njatanjata

Last edited by a moderator:
Balantanda we mkali sana. duh.. hapa najisikia moyoni kumepoa vizuri sana. hii thread ilipaswa iwe sticky why @mods halioni hili? na watu kama bantalanda walipaswa kupewa nishani za utumishi uliotukuka
 
Karibu mkuu...

Thread iko Sticky muda mrefu sana mkuu...
 
Last edited by a moderator:
Ningeliyasema bayana lakini naogopa kuzifufua chuki zilizopita
poza roho ndugu kwa yote yaliokupa kwa sababu ya kupenda
pendo limekuwa kama limepitwa na maji ndani ya ziwa ukabaki na huzuni
najua penzi ni donda la rohoni lakini usichukie eeeh
Ukutanapo na mwenzio tabasamu mfariji oooh ukiweza
Ukae ukielewa kupenda sio ndoto ya usiku mmoja mamaaa
 
Balantanda

hebu fanya uungwana wa Nyimbo hizi wallah...
Msondo - shida mpaka lini
msondo - ashibae.
 
Nimekumbuka mbali sana..nilikuwa naipenda Tancut Almas Orchestra..wana kinyekinye kisonzo tisa kumi mangala..Kyanga Songa na Kasaloo kyanga mapacha hao walikuwa moto wa kuotea mbali.
 
Mpenzi Luta nasikitika sheriee...yo yo yoo kuishi tena na wewe,mama yoo vituko vyako vimezidi,vimenichosha oh,mupenzi,nashindwa hata la kufanya,nilikuwa nikikuonya,hukutaka kunisikia najuta ooh ooh ooh..kuishi nawe masikini mie mamaa,kwa kweli sina raha.......... Kiranga hivi yule bwana aliyekuwaga pale ghorofa ya akina captain Aziz Mindu street opposite na Shamo alikuwa mwanamuziki gani?ni Kasongo au?
 
nimemkumbuka.Anaitwa Tshimanga Kalala Assosa!yule mzee anazeeka mwili sauti bado ya mtoto wa shule ya vidudu ha ha haa.Sijui siku hizi kajifunza kuvaa vizuri suruali?alikuwa anazivalia kifuani halafu anapenda kweli kumung'unya pipi.Watoto wakimuomba "mzee Asosa tupe pipi basi" anawaambia "ukuje kubeba iko mufukoni", inabidi usimamie vidole manake mifuko iko makwapani daah!.Ile Maquis ilikuwa balaa huku Nguza kule...daah!
 
Ana ngoma yake ya kuitwa Baba Wile...dah ni balaa
 
View attachment 274592

Ebu ongezea maneno kwenye SHIDA MPAKA LINI niweze kutambua ni wimbo gani wa Msondo.

mbwembwe anaanza kwa kusema bwana eeh ooh bwana weee, hali hii mpaka lini jamani, ukiamka na shida ya jana sherio na ya leo imeongezeka...

WOTE...
nyamaza ooh nyamaza ni ya Dunia mama bby sikia, shida hizi ulizo nazo zisikufanye usononeke, yakupasa ni kuvumilia mungu nae atakusaidia
 
Back
Top Bottom