R.I.P Field Marshall Halila Tongolanga, Utakumbukwa na Wanakusini na harakati za Ukombozi MSUMBIJI

nanjinji

Senior Member
Mar 23, 2017
151
250
Jumatatu, 5 Juni 2017
MWILI WA TONGOLANGA WASAFIRISHWA KUELEKEA TANDAHIMBA, BALOZI WA MSUMBIJI AJITOKEZA KUMUAGA


Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama Les Mwenge. Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko.

Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, mpiga bezi Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi Said Mahadula, mpiga solo Fadhili Ally, mpiga drums Hamza Waninga
Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA. Katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.

Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga

Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua.
Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.

Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji

Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.

Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga

Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari

John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, KumburuAdd caption


Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila
Sanduku likiingizwa kwenye gari
Credit to John Kitime
 

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,891
2,000
Innah lillah wainnah ilayh raaj'un.. Jabari la kusini Mtu pekee ambae ameimba nyimbo kwa lugha ya kimakonde ambayo kokote ukipigwa unajua hii ngoma kutoka kwa wamakonde
 

jozzeva

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,201
2,000
Pumzika kwa amani jembe..hulima shamba kubwa na kisha watu wakapata mavuno mazuri lakini msimu wa kilimo ukiisha jembe huwekwa stoo au juu ya dari..pumzika kwa amani mkuu Tongolanga.
 

Handsome man

JF-Expert Member
May 6, 2017
899
1,000
RIP shujaa tongolala, amekufa wakati bado anaudai madeni makubwa ya shilingi mziki aliokuwa anaufanya
 

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,404
2,000
Wanasemaga marehemu hasemwi vibaya,lakini mimi nina swali kidogo mtanisamehe, INASEMEKANA ETI hakuwahi kuwa na nyumba na hata kijijini kwao hakuwahi kuweka hata kibanda cha miti hii ni kweli au uzushi .......By the way r.i.p na poleni kwa wote waliokutwa na msiba huu na mingine mingi inayotokea.
 

nanjinji

Senior Member
Mar 23, 2017
151
250
Wanasemaga marehemu hasemwi vibaya,lakini mimi nina swali kidogo mtanisamehe, INASEMEKANA ETI hakuwahi kuwa na nyumba na hata kijijini kwao hakuwahi kuweka hata kibanda cha miti hii ni kweli au uzushi .......By the way r.i.p na poleni kwa wote waliokutwa na msiba huu na mingine mingi inayotokea.
Ni kweli mkuu, marehemu licha ya kuwa msanii mkubwa kwa upande wa kusini na nchini Msumbiji alikuwa analala kwenye kibanda flani hivi chumba-sebule "gheto" kama yale ya makahaba wa Tandika tena la kwake limechakaa kweli kweli kijijini kwao Mchichila.
Na kuumwa alianza akiwa Dar mama yake ambaye ana umri wa zaidi ya miaka 74 akamtumia nauli ili arudi kijijini akamuuguze na kwa msaada wa Khatani akarudi tena Muhimbili ambako ndiko alifariki.
R.I.P Tongolanga
 

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,404
2,000
Ni kweli mkuu, marehemu licha ya kuwa msanii mkubwa kwa upande wa kusini na nchini Msumbiji alikuwa analala kwenye kibanda flani hivi chumba-sebule "gheto" kama yale ya makahaba wa Tandika tena la kwake limechakaa kweli kweli kijijini kwao Mchichila.
Na kuumwa alianza akiwa Dar mama yake ambaye ana umri wa zaidi ya miaka 74 akamtumia nauli ili arudi kijijini akamuuguze na kwa msaada wa Khatani akarudi tena Muhimbili ambako ndiko alifariki.
R.I.P Tongolanga
Aksante sana mkuu kwa majibu yako na pia kwa kunielewa nini nilichokusudia kutaka kujua,maana mwingine angejifanya kunitukana na kujiona kama anauchungu sana.
 

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,322
2,000
R.I.P Halila Tongolanga...ila picha uliyoweka hapo juu sio ya Halila Tongolanga.
hqdefault.jpg

Huyu ndiye Marehemu Tongolanga.
 

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,322
2,000
RIP shujaa tongolala, amekufa wakati bado anaudai madeni makubwa ya shilingi mziki aliokuwa anaufanya
Ni kweli, jamaa alijitahidi sana ku promote Kusini kwa sanaa yake, ila ndio hivyo promo ilikuwa finyu.

Wimbo wa 'kila munu ave na kwao' ulikuwa mkubwa...na kusema ukweli ule wimbo ni mzuri kusikiliza hata kama Mtu huelewi kinachoimbwa...alianzia na huu wimbo Mwenge jazz enzi hizo ila alikuja kuurudia mpaka part 3 (nakubali kusahihishwa)...akiwa na Makondeko Musica...wimbo huu pia ulirudiwa na Shaa wa bongo flavour.

Sio wengi wa kizazi hiki wanaoujua mchango wa Tongolanga...nakumbuka hata alipofariki Che Mndugwao miaka kadhaa nyuma niliwasikia Watangazaji wa clouds (Hando au Musa) sikumbuki vizuri, walimtaja kama Chemndugwao ndiye aliyeimba wimbo wa 'kila munu ave na kwao'...na wakati huo Tongolanga alikuwa yupo...nilijiuliza hivi kwa nini Wana habari wasiulize wapate taarifa kabla ya kuongea redioni?...labda nijulishwe leo kama Marehemu Chemndugwao naye aliuimba huo wimbo.
 

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
May 3, 2012
2,440
2,000
Mkuu...Mbona picha uliyoweka sio ya marehemu halila tongolanga, picha uliyoweka ni ya mdogo wa marehemu halila tongolanga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Thread starter Similar threads Forum Replies Date
DMCT Mjue Bruce Marshall Mathers |||{Eminem} Celebrities Forum 37
Similar threads

Top Bottom