ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Wakuu mi nataka kujua viwanja wanapopiga zilpendwa kwa dar..
Mi najua chaka moja tu la Tabata Mawenzi wanapiga Maquiz
 
Kumbe Maquiz ni Zilipendwa? Basi Nenda DDC kariakoo Utawakuta Sikinde Ngoma ya Ukae utauliza Ratiba zao watakupa zote
 
Nimekuwekea wimbo wenyewe na waliokuja kurudia.

Cc. Gang Chomba

View attachment 283219

View attachment 283220
Mkuu ukiniwekea Wimbo wa Sambe nitakuwa nimeburudika sana Uliopigwa na Balisidya pia...

Sasa yapata miaka miwili.....
Namtafuta rafiki yangu Sambe....

Sambe eenh yupo wapi Sambe eenh

Niliondoka nikiwa na khofu
Nikafika Hospitali Nilipomuona rafiki Sambe..
Nilitokwa na Machozi..

Sambe anaumwa ukimwi
 
Waungwana kuna mtu anaukumbuka wimbo uliopigwa na Six Manyara unaitwa Tabu, ambapo mmoja ya waimbaji wake
alikuwa Hassan Rehani Bichuka.
 
Heri ya Mwaka mpya wadau....

Za mwaka mpya safi mkuu. Kea sasa Tanzania hatuna Music, ni pigo kubwa sana!

Sikinde, Msondo, Vijana Jazz, Washirika Tanzania Stars, Bimalee, Polisi Jazz(mkote ngoma-Ashura),Bantu Group, Marquiz nk zilikua bendi zilizoitambulisha Tanzania abroad, ni kwa masikitiko makubwa nyingi ya bendi hizi zimekufa na hata magwiji wake wengi ni marehemu na wengine umri umewatupa mkono, na sioni dalili ya muziki mtamu kwa level ya miaka ya 80-1997. Mwaka huo wa 1997 ndiyo muziki wa Dansi Tanzania ulianza kufifia, mwaka huo wa 1996-97 Vijana Jazz walitoa Album yao ya mwisho kwa hadhi ya Vijana Jazz(Umaskini bye bye)! Katika Album hiyo wakongwe walimaliza kazi hiyo ni:Fred Benjamin, Toto Tundu, Shakashia,Shomari Ally,Suleiman Mbwembwe na wengine. Baada ya hapo Vijana Jazz ikapoteza dira, wakatoa Album ile ya Mabaa Medi na I Love You Mpiga Debe, ambayo kwangu mimi nasema haikufuata mitindo ile halisi ya Vijana Jazz tuliyoizoe na hapo ikawa mwisho wa Dansi za miaka ya 80-90!

Zilikuja bendi za dansi ya kisasa kama Twanga Pepeta, Double M, Mchinga Sound, Muungano Band, Tam Tam na T.O.T Band. Hicho ni kizazi cha dansi miaka ya 2000-2005 hivi, baada ya hapo zikaanza kutoweka taratibu, na leo 6/2/2016,ukiniuliza zilizobaki hata sijui zaidi ya Twanga Pepeta ambayo nayo miaka ya 2010 kuja huku mbele ikaanza kutofanya vyema.
Kwa kifupi Muziki wa Dansi umekufa na Bongo Flavor haina mwelekeo,tupo kama hatupo,inasikitisha kweli!

Nimalizie kwa kumbuka nyimbo hizi, kama Bantalanda ukinipatia Lyrics zake nitashukuru sana:-

1. Vijana Jazz(Top Queen,Shoga,Kapu la Mjanja, Janja ya Nyani)
2.DDC( Naomi, Naomba Tuaminiane)
3.Washirika(Penzi la Ulaghai, Nimekusamehe, Ukewenza-Kulala Sebuleni)
4.Marquiz(Leila, Makumbele)
5.MCA( Shida, Kasoro yangu)
6.Bantu Group(Baba Jane I & II)

Moja wapo ya nyimbo hizo nakuomba uniwekee Lyrics kwa wowote utakaofanikiwa kuupata kwenye Library zako ahsante

Chaza/Oyerster!
 
Acha Ujinga kwa kuongelea vitu usivyovifahamu wala kuwa na fani navyo DDC Sikinde Ipo na bado inaendelea kuwepo,Msondo pia... na watu bado wanakula radha ile ile Bitchuka yupo kama kawa na Sauti yake ile ile... Dede yupo Msondo kama kawa japo Maradhi ya Sukari yanamsumbua mara kwa Mara na umri yes umekwenda ila Jasiri haachi Asili... so wacha kuchulia watu wa Fani zao...

Zahoro anaendelea na Kazi zake
Kalala yupo Juniour
King Kikii Yupo
Kitime ndie alikuwa Vijana jazz Yupo akiweka mambo sawa huku na kule kuwaunganisha wanamuziki na kuwaweka kimakundi...
Band nyingi sana bado zipo japo zinahama hama kwa kubadilisha wamiliki... so nyingi zimekuwa zinapiga kwa Mikataba kwenye Kumbi na Hotel mbali mbali sababu Wanamuziki wa Band ndio Wataalam sana wa kupiga vyombo n.k yaani Music halisi tuseme Kila Zama na Zama zake lakini zipo... Utunzi ndio Changamato sana na haswa ile ya kufanya wimbo uheat ndio issue...
 
kuna ubishi wa kumbukumbu...
je kwenye wimbo Asha Bora wa sikinde solo limepigwa na nani?
1) Kasim mponda delashamshi
2) Mkanyia
 
Acha Ujinga kwa kuongelea vitu usivyovifahamu wala kuwa na fani navyo DDC Sikinde Ipo na bado inaendelea kuwepo,Msondo pia... na watu bado wanakula radha ile ile Bitchuka yupo kama kawa na Sauti yake ile ile... Dede yupo Msondo kama kawa japo Maradhi ya Sukari yanamsumbua mara kwa Mara na umri yes umekwenda ila Jasiri haachi Asili... so wacha kuchulia watu wa Fani zao...

Zahoro anaendelea na Kazi zake
Kalala yupo Juniour
King Kikii Yupo
Kitime ndie alikuwa Vijana jazz Yupo akiweka mambo sawa huku na kule kuwaunganisha wanamuziki na kuwaweka kimakundi...
Band nyingi sana bado zipo japo zinahama hama kwa kubadilisha wamiliki... so nyingi zimekuwa zinapiga kwa Mikataba kwenye Kumbi na Hotel mbali mbali sababu Wanamuziki wa Band ndio Wataalam sana wa kupiga vyombo n.k yaani Music halisi tuseme Kila Zama na Zama zake lakini zipo... Utunzi ndio Changamato sana na haswa ile ya kufanya wimbo uheat ndio issue...
Sasa wewe matako, ulichobisha ni kipi na uanachoandika ni kipi, muziki wa dansi kwa wanaojua muziki wa Dansi wa Tanzania hawawezi kukaa na kujivunia, pamoja na baadhi ya wakongwe wa Sikinde na Msondo hao uliowataja kuwa hai, bado kasi yao imeshuka ingawa sauti bado Dede, na Bitchuka zipo imara, ila haiwez kuondoa ukweli kuwa muziki wetu wa Dansi umefifia.

Kwa wadau na wachambuzi mahiri wanakiri kuwa muziki wa dansi umesuasu. John Jambele, Masoud Masoud, Zomboko,John Kitime, Mbazigwa Hassan et al, ukiwauliza naamini hawawezi kupata faraja kuona hali ya muziki wetu wa dansi ilivyo kwa sasa.
 
We kweli umebinuka nyuma... nundu lako ukitembea linacheza cheza.... Huo Mziki uliofifia labda kwenu ila sie kila unapopigwa huita watu na wanaenjoy... tatizo lako Taarabu imekukolea sana... Muzik ya zamani kwanza haijafa na haitakufa... ila waimbaji ndio watakufa au wesha kufa kitambo lakini ngoma bado ni mbichi kabisa wewe utakuwa kama bendera fata upepo... tu huyo kitine pia bado anadeal na miziki hiyo hiyo sasa umuite akuambie miziki yao imekufa????? kenge sana wewe.... kakojoe ulale huna hadhi ya kuzungumza na watu wazima.... ndio maana nyie Wahuni hamuwekewi Dhamana... mnatoroka tu..
 
  • Thanks
Reactions: bdo

Huyu atakua choko
 
Ktk mashindano ya bendi bora mwaka 1982 Sikinde walinyakuwa ushindi. Nyimbo bora iliowapa ushindi ilikuwa ni tangazia mataifa.
 
Mwaka 1983 Suleiman Mwanyilo, Abdalah Gama na Bathromeyo Mulenga walihama Sikinde na kwenda Bima Lee.
 
Mwaka 1985 muanzilishi wa bendi Abel Barthazal, Bitchuka na Ibrahim Mwinyichande nao pia walitimkia OSS
 
MWAKA 1987 KILA DALILI YA BENDI HII KUFA ILIONEKANA. KWANI ILIKIMBIWA NA WANAMUZIKI KAMA BENOVILA ANTONY, HAMIS JUMA, COSMAS CHIDUMULE, MAX BUSHOKE NA WENGINE WENGI...LAKINI CHIPEMBELE SAID, FRANCIS NADHIR LUBUA, HENRY MKANYIA, KASIM MPONDA DELASHAMSHI, ABDALAH RAMADHAN NA KAKA MKUU HABIB JEFF WALISIMAMA IMARA NA CHA KUSHANGAZA NGINDE ILIRUDI KTK UBORA WAKE ULEULE.
NGINDE IPO MPAKA SASA NA HABIB JEFF TANGU ALIPOINGIA HAJATOKA MPAKA HII LEO.
 
Kwa waliokuwepo Mwanza 1969 tukumbuke Orchestra Super Vea. Hapo alikuwepo pia mpiga rhythm mahiri Zahir Ally (Baba yake Banana) wakati huo tunamwita Zahoro "Zorro" na alikuwa kijana mtanashati sana. Tulikuwa tukipita Social Hall, karibu na Nyakabungo njiani kuelekea Isamilo toka Chopra Sec ilikuwa ni lazima tutulie kidogo pale na kuwasikiliza Super Vea mazoezini, walitamba sana na kibao chao cha Apollo kumi na moja. Vijana waliotamba enzi hizo Mwanza walikuwemo pia Martin (mchezaji wa Pamba Sports na mfanyabiashara wa madini). Zahoro alikuwa na uwezo wa kupiga gitaa wakati amelibeba nyuma ya kichwa, staili maarufu sana wakati huo. Baadaye nilikuja kukutana na Zahoro 1974 Dar es Salaam akiwa anafanyiwa audition na Bima Lee (bendi ya Bima wakati huo) kwenye jengo jipya la Kitega Uchumi pale chini (underground floor) kulikuwa na sehemu ya mazoezi kabla haijageuzwa kuwa Chinese Restaurant. Zahir hakufanikiwa kujiunga na Bima Lee lakini baadaye aliibukia JKT Kimbunga.
 
Back
Top Bottom