Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Muziki wa zamani ulikuwa na burudani ya aina yake. Mbali ya utunzi mahiri na uimbaji hodari, nyimbo nyingi zilitungwa kuelezea visa na mikasa iliyowahi kuwakuta wasanii husika.
Kupitia uzi huu tutakumbushana nyimbo mbalimbali ambazo zinasimulia visa hivyo vilivyowasibu ndugu zetu hawa. Lol!
Kwa heshima ya Jabali la Muziki, Marijani Rajab (RIP), nitafungua njia kwa kuelezea yaliyomkuta mpaka akatunga wimbo wake maarufu uitwao Aisha kama nilivyokuta ikisimuliwa na wadau fulani.
Ilikuwa hivi;
'Marijani alitembelea Mwanza, akakutana na kipusa Aisha. Binti mzuri, mtanashati wakati huo anatingisha Jiji la Mwanza.
Jabali la muziki akakolea, ikabidi binti akamuahidi Jabali kuonana nae Dar es Salaam.. Wakapanga siku ya kukutana pale Keys Hotel, barabara ya Uhuru, karibu na Mnazi Mmoja. Wakati huo Keys Hotel ndio ilikuwa Hotel janja na ya wajanja..
Siku ya ahadi Jabali akafika mapema kumsubiri.. Alisubiri mpaka usiku hakutokea. Kesho yake akasema abahatishe wapi.. Ndio akaamua kumtungia wimbo huo.
Huyo dada anaishi Marekani sasa hivi na anakadiriwa kuwa na umri wa takribani miaka 60'.
Wimbo wenyewe ni huu hapa chini;
Unakumbuka kisa gani cha kweli ambacho kilitungiwa wimbo?