Yuzo mawe
JF-Expert Member
- May 31, 2019
- 494
- 550
"You spend what you earn",Kama ume spent 55M it seems una kipato kikubwa boss kutokana na maisha ya kitanzania,Mwaka 2020 ndiyo unaelekea mwishoni, huku zikiwa zimebaki siku 50 kuisha. Watanzania hatuna mazoea ya kuandaa bajeti zetu binafsi, lakini ni tool muhimu sana kwenye maisha yetu hasa unapotaka kuona maeneo ya kupunguza matumizi kama sio ya lazima
Hapa chini nimefanya tathmini ya matumizi ambayo nimefanya kwa mwaka mzima, inaweza isiwe exactly figures but i guess haitakuwa mbali sana na reality.
Hadi Oktoba nimetumia almost 55,396,000
- Kodi ya pango, kwenye eneo hili hadi mwezi Septemba nilikuwa nimetumia 2,700,000
- Chakula, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 2,100,000
- Gesi na Umeme hadi kufikia Mwezi Oktoba nilitumia 560,000
- Mavazi, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 1,060,000
- Michango ya Harusi na Misiba hadi kufikia mwezi Oktoba nimetumia shilingi 650,000
- Starehe na kufurahi, hadi kufikia Oktoba nimetumia 800,000
- Sadaka na michango yake kwa pamoja imefikia 600,000 hadi Oktoba, 2020
- Kupiga taff home na ndugu hadi Oktoba nimetumia 1,000,000
- Mawasiliano, hadi mwezi Oktoba nimetumia 400,000
- Investments(Viwanja, Ujenzi, Mashamba) hadi Oktoba nimetumia 38,020,000
- Matumizi ya nyumbani 1,670,000
- Safari na Lodge hadi Mwezi Oktoba nimetumia 740,000
- Afya na matibabu nimetumia almost shilingi 940,000
- Bodi ya mikopo hadi kufikia Oktoba nimetumia 1,856,000
- Kulipia ada vijana, hadi Oktoba nimelipa 2,300,000
Karibuni tupate experience zenu pia kwenye eneo hili, binafsi nimeona maeneo ambayo nahitaji kubana bajeti Mwaka ujao panapo Majaaliwa.
NB; Naomba tushare upande wa matumizi tu, upande wa Kipato ibaki ni SIRI ya mtu binafsi.
Lakini kwenye ku assess matumizi yako tu bila kujua kipato chako inakua ngumu.