Hata hivyo mwaka huu nimefanya kupunguza hiyo #7 ilikuwa zaidi miaka ya nyuma. Mwakani nitaongeza hiyo #6 angalau ifike 3,500,000 kama nitawezaNimependa #5 lakini nimesikitishwa na jinsi zilivyo pishana 5,6 na 7, kwamba starehe iko juu kuliko kujitoa kwako
Muhimu uzima tu, tujipange kwa battle nyingine mwakani
Kuna targets nilijiwekea ambazo zililazimu nijinyime kidogo so far atleast 89% nimetimiza, panapo majaaliwa mwakani nitapunguza kujinyimaroughly budget yako ya chakula ni tsh 7,000/= na starehe yako wastani kwa siku ni tsh. 3,000/= rekebisha hapa maisha ni mafupi sana kujibana kwa namna hii, utakaribisha magonjwa
Hii imekaa poa sanaMi natumia software ku track income and expenses, nilipoanza ilikuwa ni ngumu lakini sasa nimezoea, kila nikipata pesa na buget na kisha . Inanisaidia sana kujua wapi pesa inaenda. Mwaka huu matumizi makubwa yamekuwa kwenye ujenziView attachment 1624337kurecord matumizi yake
Mkuu tupe link na sie tupakueMi natumia software ku track income and expenses, nilipoanza ilikuwa ni ngumu lakini sasa nimezoea, kila nikipata pesa na buget na kisha . Inanisaidia sana kujua wapi pesa inaenda. Mwaka huu matumizi makubwa yamekuwa kwenye ujenziView attachment 1624337kurecord matumizi yake
Link hii:Quicken Personal Finance & Money Management SoftwareMkuu tupe link na sie tupakue
Bado umesahau kuhusu bank account umekopa bei gani? Matumizi makubwa sio kutusuhua katika maisha. Ni kuishi kwa ufahari mwisho wa siku ni stressMwaka 2020 ndiyo unaelekea mwishoni, huku zikiwa zimebaki siku 50 kuisha. Watanzania hatuna mazoea ya kuandaa bajeti zetu binafsi, lakini ni tool muhimu sana kwenye maisha yetu hasa unapotaka kuona maeneo ya kupunguza matumizi kama sio ya lazima
Hapa chini nimefanya tathmini ya matumizi ambayo nimefanya kwa mwaka mzima, inaweza isiwe exactly figures but i guess haitakuwa mbali sana na reality.
Hadi Oktoba nimetumia almost 55,396,000
- Kodi ya pango, kwenye eneo hili hadi mwezi Septemba nilikuwa nimetumia 2,700,000
- Chakula, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 2,100,000
- Gesi na Umeme hadi kufikia Mwezi Oktoba nilitumia 560,000
- Mavazi, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 1,060,000
- Michango ya Harusi na Misiba hadi kufikia mwezi Oktoba nimetumia shilingi 650,000
- Starehe na kufurahi, hadi kufikia Oktoba nimetumia 800,000
- Sadaka na michango yake kwa pamoja imefikia 600,000 hadi Oktoba, 2020
- Kupiga taff home na ndugu hadi Oktoba nimetumia 1,000,000
- Mawasiliano, hadi mwezi Oktoba nimetumia 400,000
- Investments(Viwanja, Ujenzi, Mashamba) hadi Oktoba nimetumia 38,020,000
- Matumizi ya nyumbani 1,670,000
- Safari na Lodge hadi Mwezi Oktoba nimetumia 740,000
- Afya na matibabu nimetumia almost shilingi 940,000
- Bodi ya mikopo hadi kufikia Oktoba nimetumia 1,856,000
- Kulipia ada vijana, hadi Oktoba nimelipa 2,300,000
Karibuni tupate experience zenu pia kwenye eneo hili, binafsi nimeona maeneo ambayo nahitaji kubana bajeti Mwaka ujao panapo Majaaliwa.
NB; Naomba tushare upande wa matumizi tu, upande wa Kipato ibaki ni SIRI ya mtu binafsi.