Zikiwa zimebaki siku 50 Mwaka kuisha, hii ni tathmini ya matumizi yangu kwa mwaka 2020.

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
10,396
32,081
Mwaka 2020 ndiyo unaelekea mwishoni, huku zikiwa zimebaki siku 50 kuisha. Watanzania hatuna mazoea ya kuandaa bajeti zetu binafsi, lakini ni tool muhimu sana kwenye maisha yetu hasa unapotaka kuona maeneo ya kupunguza matumizi kama sio ya lazima

Hapa chini nimefanya tathmini ya matumizi ambayo nimefanya kwa mwaka mzima, inaweza isiwe exactly figures but i guess haitakuwa mbali sana na reality.

  1. Kodi ya pango, kwenye eneo hili hadi mwezi Septemba nilikuwa nimetumia 2,700,000
  2. Chakula, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 2,100,000
  3. Gesi na Umeme hadi kufikia Mwezi Oktoba nilitumia 560,000
  4. Mavazi, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 1,060,000
  5. Michango ya Harusi na Misiba hadi kufikia mwezi Oktoba nimetumia shilingi 650,000
  6. Starehe na kufurahi, hadi kufikia Oktoba nimetumia 800,000
  7. Sadaka na michango yake kwa pamoja imefikia 600,000 hadi Oktoba, 2020
  8. Kupiga taff home na ndugu hadi Oktoba nimetumia 1,000,000
  9. Mawasiliano, hadi mwezi Oktoba nimetumia 400,000
  10. Investments(Viwanja, Ujenzi, Mashamba) hadi Oktoba nimetumia 38,020,000
  11. Matumizi ya nyumbani 1,670,000
  12. Safari na Lodge hadi Mwezi Oktoba nimetumia 740,000
  13. Afya na matibabu nimetumia almost shilingi 940,000
  14. Bodi ya mikopo hadi kufikia Oktoba nimetumia 1,856,000
  15. Kulipia ada vijana, hadi Oktoba nimelipa 2,300,000
  16. Service ya Kagari, Petroli hadi Oktoba, 2020 nimegharamia almost 1,710,000
  17. Gharama za kulipia boda boda au Bajaj hadi Oktoba nimetumia almost 360,000
Hadi Oktoba nimetumia almost 57,466,000

Karibuni tupate experience zenu pia kwenye eneo hili, binafsi nimeona maeneo ambayo nahitaji kubana bajeti Mwaka ujao panapo Majaaliwa.

Kwenye eneo la Bajaj/Boda boda huwa tunatumia fedha nyingi wakati mwingine kuliko tunachobajeti hasa kwa kuwa tunalipa 1,000 au 2,000 but zikiwa Accumulated unaweza kuta ni zaidi hata ya 1,000,000 kwa mwaka au zaidi.

Eneo lingine la kuangalia kwa makini hasa upande wa kubana bajeti mwakani ni eneo la michepuko, eneo hili ingawa nimeshindwa kutaja fedha iliyotumika(Bado najutia hela nilipoteza) trust me, linakula hela zetu nyingi sana. Mwakani panapo majaaliwa, nimepanga kuwa makini zaidi ikiwemo kutumia mbinu za kimedani kufanikisha mambo yangu.

Eneo la michango ya harusi pia nitaongeza umakini, yaani baada ya Covid 19 kadi za michango ninazo pokea zimekuwa nyingi hadi kuharibu bajeti zangu.

NB; Naomba tushare upande wa matumizi tu, upande wa Kipato ibaki ni SIRI ya mtu binafsi.💪
 
Starehe na kufurahi 800k, afya na matibabu 940k.... ni kwamba afya yako ni tiamaji tiamaji.

Ushauri:

Ongeza fungu la starehe na kufurahi, mwili hautohitaji matibabu.
Niliweka malengo ya kutotumia Sana eneo hilo la starehe, but next time nitaongeza matumizi pia.

Upande wa afya, ni kwangu na jamaa zangu hasa ndugu
 
Ni ujinga kujinyima starehe kisha pesa ikaishia kwenye sadaka na matibabu.
Sikuwa nimeplan kutumia hela nyingi kwenye starehe, but Mungu akipenda mwakani nitaongeza bajeti eneo hilo.

Hata hivyo si unajua kuna Christmas hapo December, huenda nikatumia nyingi
 
Sikuwa nimeplan kutumia hela nyingi kwenye starehe, but Mungu akipenda mwakani nitaongeza bajeti eneo hilo.

Hata hivyo si unajua kuna Christmas hapo December, huenda nikatumia nyingi

Christmas sio starehe, starehe ni tabia... tukio la siku moja haliwezi kurescue afya yako.
 
Christmas sio starehe, starehe ni tabia... tukio la siku moja haliwezi kurescue afya yako.
Sawa Mkuu ila nachojua matumizi yote yahusuyo Christmas huwa naya term kama starehe. But all in all, sitakiwi kujibana sana eneo starehe.

Unaweza kujibana then ukafa ukiwa hujafaidi ulichochuma juani, next time huo ujinga sitafanya
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom