Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 11,150
- 34,325
Mwaka 2020 ndiyo unaelekea mwishoni, huku zikiwa zimebaki siku 50 kuisha. Watanzania hatuna mazoea ya kuandaa bajeti zetu binafsi, lakini ni tool muhimu sana kwenye maisha yetu hasa unapotaka kuona maeneo ya kupunguza matumizi kama sio ya lazima
Hapa chini nimefanya tathmini ya matumizi ambayo nimefanya kwa mwaka mzima, inaweza isiwe exactly figures but i guess haitakuwa mbali sana na reality.
Karibuni tupate experience zenu pia kwenye eneo hili, binafsi nimeona maeneo ambayo nahitaji kubana bajeti Mwaka ujao panapo Majaaliwa.
Kwenye eneo la Bajaj/Boda boda huwa tunatumia fedha nyingi wakati mwingine kuliko tunachobajeti hasa kwa kuwa tunalipa 1,000 au 2,000 but zikiwa Accumulated unaweza kuta ni zaidi hata ya 1,000,000 kwa mwaka au zaidi.
Eneo lingine la kuangalia kwa makini hasa upande wa kubana bajeti mwakani ni eneo la michepuko, eneo hili ingawa nimeshindwa kutaja fedha iliyotumika(Bado najutia hela nilipoteza) trust me, linakula hela zetu nyingi sana. Mwakani panapo majaaliwa, nimepanga kuwa makini zaidi ikiwemo kutumia mbinu za kimedani kufanikisha mambo yangu.
Eneo la michango ya harusi pia nitaongeza umakini, yaani baada ya Covid 19 kadi za michango ninazo pokea zimekuwa nyingi hadi kuharibu bajeti zangu.
NB; Naomba tushare upande wa matumizi tu, upande wa Kipato ibaki ni SIRI ya mtu binafsi.💪

- Kodi ya pango, kwenye eneo hili hadi mwezi Septemba nilikuwa nimetumia 2,700,000
- Chakula, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 2,100,000
- Gesi na Umeme hadi kufikia Mwezi Oktoba nilitumia 560,000
- Mavazi, hadi kufikia Mwezi Oktoba nimetumia 1,060,000
- Michango ya Harusi na Misiba hadi kufikia mwezi Oktoba nimetumia shilingi 650,000
- Starehe na kufurahi, hadi kufikia Oktoba nimetumia 800,000
- Sadaka na michango yake kwa pamoja imefikia 600,000 hadi Oktoba, 2020
- Kupiga taff home na ndugu hadi Oktoba nimetumia 1,000,000
- Mawasiliano, hadi mwezi Oktoba nimetumia 400,000
- Investments(Viwanja, Ujenzi, Mashamba) hadi Oktoba nimetumia 38,020,000
- Matumizi ya nyumbani 1,670,000
- Safari na Lodge hadi Mwezi Oktoba nimetumia 740,000
- Afya na matibabu nimetumia almost shilingi 940,000
- Bodi ya mikopo hadi kufikia Oktoba nimetumia 1,856,000
- Kulipia ada vijana, hadi Oktoba nimelipa 2,300,000
- Service ya Kagari, Petroli hadi Oktoba, 2020 nimegharamia almost 1,710,000
- Gharama za kulipia boda boda au Bajaj hadi Oktoba nimetumia almost 360,000